Moja ya kero kubwa na ambayo kwa mtizamo wangu inaweza kuwa kikwazo kwa wananchi wa kawaida kuendana na kaulimbiu ya hapa kazi tu, ni namna tunavyoendesha sherehe mbalimbali za kijamii, kama vile harusi, send-off party, kitchern party na sasa imeongezeka sherehe zingine kama ubatizo, kipaimara, graduation na engagement party.
Raia maskini hulazimika kuchanga pesa nyingi na wengi hulazimika kuingia kwenye mikopo ambayo huwatesa mno, mtu hulazimika kuchangia hata kama hana pesa kwa kuogopa kutengwa na jamii.
Tatizo la pili ni muda ambao sherehe hufanyika. Nyingi huisha usiku sana, "sherehe inaisha saa saba usiku au saa nane, unafika nyumbani saa tisa usiku, kupata usingizi saa kumi alfajiri, asubuhi unatakiwa uwepo kazini saa moja asubuhi. Hivi hapo ufanisi utakuwepo kweli?"
Tatizo la tatu ni siku za sherehe, ukiondoa harusi, sehemu kubwa ya sherehe zilizobakia hufanyika katikati ya wiki, jambo ambalo hupunguza kwa kiasi kikubwa utendaji kazini na wakati fulani huathiri mahudhurio ya wafanyakazi.
Ili kuendana na kauli mbiu ya hapa kazi tu, napendekeza wizara inayohusika na ustawi wa jamii ifanye yafuatayo;
- Ipige marufuku michango yote ya sherehe, na atakayechangisha aadhibiwe vikali
- Sherehe zote zifanyike weekend au siku za mapumziko
- Mwisho wa sherehe zote uwe saa kumi na mbili jioni, adhabu kali itolewe kwa atakayezidisha muda
Familia ziendeshe sherehe kwa gharama zao wenyewe, wasiruhusiwe kuchangisha kwa mtu asiye mwana familia, nchi nyingine kama Zambia wameweza, kwanini sisi tushindwe. Kama nawe unakerwa na jambo hili, toa pendekezo, huenda wahusika nao wakapitia uzi huu.
Alamski!