Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Huku mtaani kwetu napata kadi 3 mpk 5 kwa mwezi. Nyingine za ubatizo wa mtoto, Mara ubarikio, kuna kitu kinaitwa mbesii (wenzangu na mie wananielewa), kuna harusi, kuna ndoa (watu wameishi miaka zaidi ya kumi wamepata watoto watatu wengine wapo secondary eti wanabariki ndoa nao wanataka wachangiwe) This is so stupid kwa kweli. Hatutaweza ht kujenga kibanda cha kuku kwa mtindo huu.

Halafu sasa ikitokea mtu mgonjwa anahitaji 50,000 tu akatibiwe hapo ndio utaona utamu wake, kila mtu anamuonea tu huruma mgonjwa ht mia hachangii.

Au mtoto karudishwa shule umekosa kahela kidogo tu kumalizia ada, utahangaika weeee kupata msaada. Tubadilikeni jamani

Cku hizo nipo makini sana ktk kutoa michango. Kwa mwaka naweza kuchangia sherehe mbili tu. Nyingine napotezea
 
Ni desturi yetu pale mtu anapotaka kuoa au kuolewa huambatana na vikao vya sherehe vikiongozwa na kamati teule kwa ajili ya kufanikisha na kufana kwa sherehe husika vikao, hivyo siku hizi vimegeuka mateso na kero kwa ndugu na jamaa watu wamekua mara nyingine wanaacha kazi zao zinazowaingizia kipato na kwenda kwenye vikao.

Unakuta vikao vinaendeshwa takribani miezi mitatu na wakati mwingine ndugu na jamaa husafiri toka mbali kwa ajili ya kuudhuria vikao. Maisha yalivyo magumu unakuta nauli tu kwenda na kurudi kwenye kikao ni 10000, sasa fikiria mtu atapoteza shilingi ngapi kama nauli ya kwenda kwenye vikao kwa mda wa miezi mitatu watu wanaendelea kuwa masikini na hapo bado hujaanza michango yenyewe dah vibaya sana.

Kwenye michango watu hutoa kiasi kikubwa mfano wanakadiria kaalika wageni 500 siku ya sherehe wanaoukuja ni 100 tu vyakula na resources nyingine zinaishia kuharibika vibaya sana tena. Kwanini tusiwe na njia nyingine kufaniksha harusi na sendoff bila watu kupoteza fedha na mali kusafiria vikao? Hapo ni rafiki au ndugu mmoja unakuta mtu anaudhuria vikao vitatu kwa style hii watu watakua masikini daima kwa sababu kila siku watu wanaoa na kuolewa.
 
Labda iwekwe sheria na serikali lkn watu hawasikii ila hii culture naichukia sana. Inagombanisha sana watu ndugu marafiki kwakweli" Bdo cjaoa ila I wish time yng ikifika nisipitie process hizo za kuangaisha watu.
 
Jumapili iliyopita nilikuwa kwenye kikao cha harusi ya jamaa mmoja,ndugu zake kabisa hawatokei kwenye vikao tunaotokea ni jamaa wa pembeni tu,halafu tukafika kwenye kipengere cha ahadi kuna jamaa wanadaiwa hawajamalizia ahadi zao.Basi ripoti ya kikao kilichopita ikasema,KIKAO CHA TAREHE X ILIAZIMIA KUWAKUMBUSHA "WADAIWA SUGU" KUMALIZIA/KULIPA MICHANGO YAO.Aiseee hapo pa wadaiwa sugu paliniudhi kweli bahati nzuri kumbe kuna mdau alikereka na hili.neno akaomba lilekebishwe mapema
 
Mi siku hizi sichangi kabisa hiyo michango yao ya harusi!maana unashangaa watu wanaoana hawana gari lakini harusi ikipita tu gari inanunuliwa!mmeshafanya mtaji sasa tumewashtukia
 
Ndio maana nawapenda ndugi zetu wakenya - ukitangaza harusi - mambo yote yanakuwa ni juu yenu Bwana hrusi na Bibi Harusi - mtajuwa wenyewe kama mtakopa au mtapata wapi pesa. Hivyo harusi zao zinakuwa simple sana - zinaanza saa tisa mchana mpaka saa kumi na mbili; watu wananyeshwa soda na maji tu. Hivyo gharama kidogo sana. Sio sisis tunawasumbua mpaka watu wasio husika - huu ujamaa huu.... Wenzetu wanachangiana kupeleka watoto kusoma UK - sio kunywa pombe.
 
Kama una sherehe fanya kwa uwezo wako mi sichangi wala kupoteza muda wangu mambo mengine upuuzi mtupu
 
Mi siku hizi sichangi kabisa hiyo michango yao ya harusi!maana unashangaa watu wanaoana hawana gari lakini harusi ikipita tu gari inanunuliwa!mmeshafanya mtaji sasa tumewashtukia

Ukweli mtupu. Yaani mi nimedata kama sio kuvurugwa! Hapa kazini kwetu kuna my fellow staffs 6 wote wanaoa august this year, wameniletea kadi nashindwa hata nijipange vipi?. Khaaa mi sichangiii bwana!
 
Ukweli mtupu. Yaani mi nimedata kama sio kuvurugwa! Hapa kazini kwetu kuna my fellow staffs 6 wote wanaoa august this year, wameniletea kadi nashindwa hata nijipange vipi?. Khaaa mi sichangiii bwana!
Watu wanakera sana!siku hizi imeshakuwa mtaji
 
Tuna safari ndefu sana,ila zinatoa ajira kwa watu wa decoration,catering,kumbi muziki na ma MC wanapiga hela kichizi.Kumbi za sherehe zinazidi kuongezeka
 
Tunaweza kupendekeza vikao vifanyike kupitia mitandao ya kijamii kama whatsup au ata skype. Tuishi kwa tija hasa kwenye miji mikubwa ambako foleni na vurugu za usafiri ni kubwa.
 
Nashndwa kuelewa ce wabongo tukoje,mtu kajikalia tu huko kapata wazo la kuoa,anaanza kusumbua watu na vitext vya kukumbushia mchango..mke ni wako,na utakae mfaidi ni wewe.iweje tusumbuane aisee?
 
si lazima ,.. ila ni lazima kutokana na utamaduni wenu... kama vipi usitoe tu
 
Nashndwa kuelewa ce wabongo tukoje,mtu kajikalia tu huko kapata wazo la kuoa,anaanza kusumbua watu na vitext vya kukumbushia mchango..mke ni wako,na utakae mfaidi ni wewe.iweje tusumbuane aisee?
Ni shughuli ya kijamii ndugu, na ni hiyari hujisikii acha...
 
Back
Top Bottom