Huku mtaani kwetu napata kadi 3 mpk 5 kwa mwezi. Nyingine za ubatizo wa mtoto, Mara ubarikio, kuna kitu kinaitwa mbesii (wenzangu na mie wananielewa), kuna harusi, kuna ndoa (watu wameishi miaka zaidi ya kumi wamepata watoto watatu wengine wapo secondary eti wanabariki ndoa nao wanataka wachangiwe) This is so stupid kwa kweli. Hatutaweza ht kujenga kibanda cha kuku kwa mtindo huu.
Halafu sasa ikitokea mtu mgonjwa anahitaji 50,000 tu akatibiwe hapo ndio utaona utamu wake, kila mtu anamuonea tu huruma mgonjwa ht mia hachangii.
Au mtoto karudishwa shule umekosa kahela kidogo tu kumalizia ada, utahangaika weeee kupata msaada. Tubadilikeni jamani
Cku hizo nipo makini sana ktk kutoa michango. Kwa mwaka naweza kuchangia sherehe mbili tu. Nyingine napotezea