Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Katika dini ya kiislam ww unaingia kwenye kundi la wanafiki. Wanafiki wana sifa kuu tatu, mojawapo ni Akiahidi Hatimizi ahadi. Jiepushe na ahadi. Wambie watu kuwa nikipata fursa nitachangia kuliko kutoa ahadi.
Hayo majibu nimetoa sana lakini watu bado wanang'ang'ania basi naishia kuwambia sawa.
 
Hayo majibu nimetoa sana lakini watu bado wanang'ang'ania basi naishia kuwambia sawa.
Ni kweli wakati mwingine watu hawa wanakera maana wanatuma sms kama vile anakudai. Anakufuata hadi ofisini kwako kukumbushia. Mimi sasa hivi nimeamua mtu akija akinipa kadi naweza nikapokea nikaitia kwenye droo au nikiamua namwambia tu kuwa huwa sichangii harusi na sherehe nyingine. Kama ana mgonjwa akikwama anifuate nitakuwa tayari kumsapoti.
 
Hili ni jipu kubwa sana kwa sasa. Ningefurahi kama serikali ingepiga marufuku. Na ndio maana ndoa nyingi zinavunjika. Jitu linachangiwa kuoa, unakuta limekopa na gari then linakopa na kujenga... Baada ya hapo maisha yanaanza kuwa magumu. Mwanamke anadhani zile pilika pilika za harusi ni kila siku maisha yanakuwa mazuri.

Unakuta vitu vya ndani mnapewa na kamati kutokana na michango ya watu. Mkiingia ndani mnaona hii siyo.....

wengine waliochanga huwa wanapenda kurudisha gharama zao hivo wanaanza kumuwinda bibi harusi.

Fanya kitu unachoweza. Kilicho ndani ya uwezo wako, sio kutaka kufanyia honey money huko serengeti SERENA. HOTEL ambayo huwezi kwenda kwa mfuko wako.
 
Inabidi tubadilike, mwenye awe harusi yake awe na zaidi ya 50% ya budget ya sherehe yake ndiyo aje kuomba mchango, ni jambo la kipuuzi kabisa unakuta eti mtu ana chini ya 5% ya budget ya sherehe, iliyobakia eti anategemea achangiwe. Hivi ukifanya sherehe ya watu 50 tu (na wewe na bi harusi inclusive) hiyo haitakua ndoa?kuna haja gani ya kupanga kufanya sherehe ya watu 300 wakati hata sherehe ya watu 100 inakushinda? Tutaendelea kupenda ufahari hadi lini?
 

Agreed agreed
 

Mkuu ulichoo leta jukwaan ni suala ambalo kwa kweli inabidi tubadilike. Inabidi watu kuandaa budget wanayoiweza na kufanya sherehe Yao Hii biashara ya kusumbuana Mara double elf 70 single 50 sio nzur kwa kweli: ndo maana mm nishasema sku ya harusi ni kadi ya mwaliko tu na hakuna ya mchango wala nn: utakuta watu wanacgangisha ml. 10 kwa mfano kwa ajili ya sherehe na wanatumia zote afu wanaenda kuanza maisha hawana kitu no bora hizo Pesa wangeweza hata kununua kiwanja au wakapata mtaji
 
Hao jamaa hata usipokuwa nchini, watatafuta namna tu wakutoe kiasi. Hawana aibu wala pride hata kidogo linapofika suala la kuzidai hizo. Mi ikifika zamu yangu, nta-demand from my old folks tu, wengine njooni na zawadi. Please return the favor.
Mpendwa fanya fanya uoe aisee.. haiwezekani mtunza sadaka huja"wowa"
 
Hahahaah hao wametisha aisee....
 
Tuweke vyama vya kusaidiana kwenye harusi kama tunavyofanya kwenye vyama vya kusaidiana kwenye msiba, kuwe michango fixed kila mwezi na kiwango ambacho ni flat rate atakachopewa atakakapokua na sherehe.
 
Acheni ubahili hebu changieni...

Hamjui mnachangia hata mapato ya serikali kwenye kodi

Mnachangia ajira za mc, caterers, waiters, magari, mapambo, keki, ndafu, maduka kwa zawadi???


(Ila mimi msinichangishe nilishaacha kuchangia)
 
Mbaya zaidi hata wanaoishi na wanawake na wana watoto nao wanaitisha vikao wanapotaka kupasha viporo vyao !!
 
Teh!
 
Chuki yako ni kwa pombe sio michango, hizo pombe ndo zinalipa kodi, ndio mcjango mkubwa kwa bajeti, na hayo masoda mnayokunywa kama maji ya sumu kiasi gani?

Pole sana mlevi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…