Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

kadi ya mchango wa harusi sio invoice...u can contribute nothing or anything u like...ndo utamaduni wetu huo tuendelee nao tu
utamaduni wako na nani????? au nini maana ya utamaduni????
 
Sasa mtu mzima unaliazimishwa wakati hela ni yako? hapa tatizo sio mchango itatakua ni wewe mwenyewe!
 
Hivi unajua maana ya neno hiari?????? ukichanga unapewa kadi.... usipochanga basi na kadi hupewi Je hiyo ni hiari???????

ni hiari sio lazima...hata kwenda kwenye harusi ni hiari sio lazima..hata kukaribishwa ni hiari ya mwenye harusi sio lazima
 
Sasa mtu mzima unaliazimishwa wakati hela ni yako? hapa tatizo sio mchango itatakua ni wewe mwenyewe!

Kulazimishwa sio mpaka ushikiwe bunduki????? ukipewa conditions (ukichanga utapewa kadi.... usipochanga kadi hupewi..... na harusini huwezi kwenda)
 
utamaduni wako na nani????? au nini maana ya utamaduni????

Ni utamaduni wetu mimi na wewe
 
Kulazimishwa sio mpaka ushikiwe bunduki????? ukipewa conditions (ukichanga utapewa kadi.... usipochanga kadi hupewi..... na harusini huwezi kwenda)
Sasa we unataka kwenda kula wenzako walivyochangia..Agrrrr!! Chako chako chetu chako?
 
Baba_Enock huwa hachangii HARUSI - Bali huchangia Ada au gharama za matibabu!
 
Sasa we unataka kwenda kula wenzako walivyochangia..Agrrrr!! Chako chako chetu chako?

Mkuu huyu atakuwa na kadi nyingi kipindi hiki na mambo ya mwisho wa mwaka haya sasa anatafuta faraja...akiwa na hela anachanga na unakuwa sio utamaduni wa kipuuzi...akibanwa unageuka kuwa wa kipuuzi

Duh
 
hahahaha namshangaa anavyosema analazimishwa! maana ukizoea kulazimishwa hii hatari sana!:A S-alert1:
 
Acheni kulalamika tu chukueni hatua, acheni kuchangia. Mimi nilishaacha kuchangia harusi huu mwaka wa tatu sasa na watu wemeshanijua na wala hakuna anayeniletea kadi.
 
Huu utamaduni si wa muhimu kabisa maana watu wanachangishana na wanahakikisha wamekula pesa zote ingekuwa afadhali katika michango yote iliyochangwa maharusi wanatengewa fungu lao hapo kama asilimia 20 hivi la kuanzia maisha.

Inabidi pia tuanze kuchangishana kutafuta ada za shule na si harusi
 
GY ishu za ma journals unaziweza? au tumuite Teamo?

Baba hebu msome huyu mtu hapo kwenye red...halafu anasema kuchangia ni upuuzi...reading between the lines, ni timing tu ya kadi amekuwa nazo nyingi hasa kipindi hiki cha sikukuu...tukimshauri asichange kwani sio hiari, anaanza mambo ya definition

duh!
 
Hivi maharusi wanaanza maisha baada ya kuoana sio? duh kazi kwelikweli
 
Kwakweli ni upuuzi na upumbavu. Watu wanataka kufanya mambo makubwa. Mwanamke anataka awaoneshe mashostito zake kwamba na yeye sasa anaolewa na ndio maana wanaume wanajiminya sana katika harusi.
Mi itabidi nifunge ndoa ya mkeka. Sitaki gharama.
 
Mkuu huyu atakuwa na kadi nyingi kipindi hiki na mambo ya mwisho wa mwaka haya sasa anatafuta faraja...akiwa na hela anachanga na unakuwa sio utamaduni wa kipuuzi...akibanwa unageuka kuwa wa kipuuzi

Duh

kwahiyo wewe unaona kama una wajibu wa kutoa msaada, mpaka mtu akukumbushe kwa kadi?????, wewe kama unajua jamaa yako anafanya sherehe je mpaka usubili akukumbushe kwani wewe huoni???, fanya issue yako kwa uwezo wako.... kama uwezo wako mdogo usitake mambo makubwa..... michango kwa kawaida ya culture ya kitanzania (hutoa ndugu wa karibu), watu wengine hutoa shukrani zao kama zawadi kwa maharusi sio kuchangia bia na vyakula ambavyo wanakwenda kuvila wenyewe......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…