Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mi mwenywe natafta nikipata mwanaume asiependa harus nitashkuru sana make kaz ya kutafta michango mi hapana

Hivi unadhani kuna mwanaume anayependa haya mambo ya sherehe..? Mara nyingi sherehe huwa zinapendwa na kina dada na mwanaume hauna jinsi ni kumridhisha mdada
 
vipi, wewe ni bubu au uwezo wa kujadili ndiyo utata?!!
Trolling.jpeg
 
Hii ni kero ya taifa...halafu kwingine unakuta michango ishachangishwa siku ya sherehe unasikia ooh mara vinywaji vimesitishwa, mara viti havitoshi jamani?!! Si mseme tu kuwa "oya wadau nichangieni nipate kutoka!"
 
kumbe waliokerwa ni wengi sana, hata mimi naona kero kubwa sana bora mtu aniombe chochote nitamsaidia ila sio MCHANGO WA HARUSI personally harusi yangu itakuwa kubwa lakini sintamchangisha hata mtu mmoja ikifika tu siku ya harusi nawapa watu wangu kadi za mwaliko basi ili na wao waogope kukupa kadi zao.

JK alisema ukitaka kula na wewe uliwe...ukichangisha wenzako na wewe watakuchangisha tu sawa na aliyekopa bank
 
Labda sijaeleweka wadau, maana ya kusema mimba na michango ya harusi ni kwamba, watu wengi huwa wanakurupuka kuanza michakato ya kuoa/kuolewa baada tu ya kushika/kupeanda mimba, na ndiyo maana nimechukulia mfano siku hizi vijana wengi huwa wanaanza usumbufu wa kutubana tuwachangie baada ya kupeana mimba, yaani wenyewe wanashindwa kujipanga au kupanga mambo yao vizuri wao wanakurupuka tu pale ambapo mimba imeshaingia na kuficha aibu ndipo wanapotaka harusi ili watu tusishtukie kilichotokea, THIS IS NOT GOOD AT ALL.
 
Huko mainland ndo kunachokeshaga hapo tu....hivi budget ya 30mil kwa nn usiwakabidhi maharusi waanzie maisha?? Wanamaliziaga hela yote kwenye konyagi..jamani!!
hizo story za michango ziishie huko huko aisee.
 
Mi sichangii harusi ng'o, na wengi wananinunia eti kisa sijachangia harusi zao shenzi wala sina habari ukinuna nuna tu.
a
hujitambui mzazi,jaribu kubadilika,Kama unatabia hiyo basi hata kwenye misiba uwa haufiki wala kutoa mchango.
 
a
hujitambui mzazi,jaribu kubadilika,Kama unatabia hiyo basi hata kwenye misiba uwa haufiki wala kutoa mchango.


Najitambua mkuu ndio maana nafanya ninachoona kinafaa na si jamii inachoona kinafaa. misiba naenda na nachangia sana, mambo yote ya ugonjwa na shida niko mstari wa mbele kuchangia lakini kama inahusu sherehe ya aina yoyote ile birthday, kipaimara, harusi. sitoi senti yangu kabisa
 
Tuacheni wenye pesa zetu tule raha ya kuchanga na kuchangiwa,sherehe ya harusi raha jama nisiseme uongo.Msiyelijua hili poleni.
 
HARUSI MOJA MICHANGO LUKUKI
  1. Kapu la mama
  2. Kicthen party
  3. Bachelor's part
  4. Send-off
  5. Hrausi
  6. Michango ya zawadi ofisini
  7. Michango ya kugharamia wawakilishi wa ofisin, kama harusi inafanyika mbali na kazini

Irresponsible life/corruption behaviour! halafu jitu zima linakununuia kwa sababu haujamchangia moja ya vipengele hapo juu, kwani unaniolea mmi? she....zi na Pum...fu zenu!

mkuu unafikiri ni kwa nini wa africa ni maskini? ni kwajili ya upuuzi kama uhu mbaya zaidi siku hizi mnapangiwa kiasi cha mchango, chini ya kiwango hupewi kadi.mbaya zaidi mnachangia siku2 mlio wachangia wamesha hachana. uhu ni umaskini wa kujitakia tusipo badilika.nawapongeza sana ndugu zangu waislam ila nawao kwa sasa wameanza kuiga kuchangishana na sio kama zamani chai na maandazi ndoa tayari. mimi nimepiga mrufuku michango isiyo kua na tija.
 
jaman salamu.. hiyo mada imenigusa sana. Ki ukweli tunaishi Dunia ambayo ina changamoto sana. unajua hata mimi natarajia kufunga ndoa hivi karibuni na nilishawahi kusema kuwa sitachangisha mtu ispokuwa awe wa karibu yangu sanaaa. wakati ulivyofika nikatoa zangu kadi kwa watu ambao najua wao ni wa karibu zaidi. Cha kushangaza nikaanza kupokea malalamiko ya watu(kupitia kwa hao niliowapa kadi). malalamiko yenyewe ni:
Mbona hakunipa kadi au ameniona mimi masikini siwezi kumchangia au ananichukulia mimi sio mtu wa karibu sana? au hataki tuhudhulie sherehe yake? watu hawa hawajui nimepanga nini, maana unaweza kumpa kadi ya mualiko mtu hata kama hajachangia cha muhimu umejipanga vipi.
Kingine nilipanga kuwa sitawapotezea muda watu kuwaita kwenye vikao kila wakati. lakini kadri siku zilivyosonga nikaanza kulaumiwa tena, mbona hatuitani kwenye vikao au hutaki tuvae vi ua vya wanakamati! mie hoi...nikasambaza message kuwaita hapo ndo nikachoka hakuna hata mmoja kati ya wale vimbelembele! sasa hizi ni changamoto ambazo usipokuwa makini utapata taabu sana kipindi cha harusi.
Kuna mwingine aliamua kuchua likizo akaenda zake kwao mkoani huko akafunga zake ndoa akarudi na pete. unajua kilichotokea! kuna jamaa alimshikia bango mbona hujatuchangisha, huonyeshi ushirikiano kabisha na wenzio maana hayo ni mambo ya kijamii! kuja kuuliza kwa watu, huyo jamaa ni namba moja kwa kutoa kiasi kidogo.. hapa ninapoongea wenzie karibu wote wameshanichangia yeye bado!
hitimisho langu: whether utachangisha au hutochangisha, lawama kwenye mambo kama hayo ambayo ni ya kijamii hayakosekani so wewe angalia best side of yours!:A S 103:
A%20S%20103.gif
 
Back
Top Bottom