Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

ha ha ha hata hizo sambusa alikopa. angekuwa kwetu wa kwetu angechezea vitasa hapo hapo
 
Hicho kipande cha maneno ya muoaji kimenichekesha sana.....Tuwe na utamaduni wa kutoa bila kutaraji kitu, chukulia kama umewasaidia maharusi au uliyempa.
 
mi nshagakataa kutoa michango inayozidi elfu kumi na tano. Nampa mtu kama sadaka hata nsipoenda harusin siumii sana. Ujinga sana mtu anakuchangisha elf hamsin na kuendelea alafu huduma zero. Watu wanachangsha hela za harus wanaenda kufungua biashara, kusoma masters etc.
 
BAADA ya matukio ya harusi ya Jumamosi iliyopita natoa onyo ole wake atakayeniomba mchango wa harusi, sitaki utani. Labda kwanza nikueleze jinsi tulivyopata misukosuko sana kwenye uchangiaji wa ile harusi, maana siku hizi hakuna pa kukimbilia, kila asubuhi unaamshwa saa kumi na mbili na meseji kwenye simu;
“Ndugu, rafiki na jamaa wa familia ya Pingapinga inakukumbusha kuwa harusi ya mtoto wao imekaribia hivyo mchango wako unahitajika”, baada ya wiki meseji huwa kali zaidi;“Siku zinaisha kwa nini hautoi mchango, unajua familia ya Pingapinga ina shughuli ya harusi ya mtoto wao, toa upesi au la usitulaumu.”

Basi hizi meseji zilikuwa nyingi kuliko zile za kampuni yangu ya simu inayobuni namna ya kunitoa mkwanja kila wiki. Hatimaye nikatoa faini, maana nisiite mchango, maana mchango haulazimishwi.

Sasa Jumamosi ndiyo ikawa siku ya harusi, kadi nililetewa mapema , nikahakikisha koti langu la kuendea harusini nalicheki vizuri, maana haya makoti yanayokaa kabatini miezi ni muhimu kucheki vizuri maana unaweza kukuta panya kazalia kwenye mfuko halafu wakatimka kutoka kwenye makazi yao wakati uko katikati ya kucheza mduara wa harusi.


Kweli tukaingia ukumbini viti vilikuweko swafi, meza zimepambwa kwa maua na MC alitukaribisha kwa maneno mengi yaliyojaa vichekesho visivyochekesha, au vichekesho vingine vimesharudiwa na kila MC hapa mjini halafu akawa analazimisha watu wapige vigelegele!

Yote bure watu walikuwa wamenuna maana hakukuwepo na dalili ya hata chupa moja ya kinywaji, ila ahadi kibao zikawa zinatolewa na MC, mara ‘Roli la bia linakuja toka breweries, mara shampeni leo inatoka Ufaransa kwa helikopta.”

Ghafla wahudumu waliovalia vikofia kichwani wakapitisha sambusa mojamoja na kinywaji round moja kwa kila mtu, wakisindikizwa na MC akituhamasisha tule tufurahi na bwana harusi. Kwa kweli hela yangu ikaanza kuniuma, kwanza nililazimishwa kulipa, halafu sioni chochote hawa jamaa vipi?

Wakati ukumbi mzima ukiwa umeendelea kununa utadhani kikao cha msiba, MC akatuambia eti bwana harusi ana machache kabla ya kutuaga kwenda kupumzika na mkewe. Pamoja na kisirani tulikuwa na hamu kumsikia mshenzi huyu anataka kusema nini.

Bwana harusi akasimama hata suti aliyovaa ilikuwa haijamkaa sawasawa, akakohoa kidogo akaanza, “Asante MC, kwanza naomba nimshukuru Mungu kwa kumuumba mke wangu, kwa hilo Mungu uko juu, kiukweli hapa nimepata mke mtulivu, mpole asiye na makeke, yaani najisikia nina bahati sana.

“Naomba niwashukuru wakwe zangu kwa kukubali kupokea robo tu ya mahari na kuruhusu ndoa hii ifanyike. Pia nishukuru kwa zawadi zao za kitanda, godoro, kabati na makochi asante sana.

“Naomba nitoe shukrani kwa bosi wangu kwa kunipa likizo fupi ili nikamilishe shughuli hii, pia wafanyakazi wenzangu kwa zawadi yenu ya jiko la gesi. Namshukuru mke wa kaka yangu kwa kutuazima gauni la harusi, na kaka yangu kwa suti hii niliyovaa. Natoa shukrani kwa mtengeneza keki, nitairudisha keki kwako kesho kama tulivyokubaliana.

“Nawashukuru wazazi wangu kwa kuja na kikundi cha ngoma toka kijijini, kweli kimeziba pengo la burudani katika harusi hii. Naishukuru kamati ya wazee wa kanisa kwa kufanikisha kumshawishi mke wangu aolewe na mimi, niwape aksante kwa akina mama waliopika sambusa hizi tulizokula kwa kweli zilikuwa tamu sana, kwa kweli leo ni furaha tupu. “MC wewe ni rafiki yangu nashukuru kwa kukubali kuwa mc wa shughuli hiikwakweli upo vizuri, aksante sanaaaaa!

Yaani inamaanisha ela zetu za mchango sijui zilinunua nini maana kila kitu almost kilikuwa bure.. mnaoowa karibuni poleni msinihesabu.

Ha! Ha! Ha! Nyambaf mmezoea mkichanga mnataka mje kula hadi kusaza halafu baada ya shughuli maharusi wanalala na njaa. Big Up sana bwana Harusi hiyo michango kaanzie maisha.

Tatizo wabongo mkiambiwa mchangie mambo mengine mnakuwa wazito lakini harusi aah fasta mkono mfukoni hiyo ndio dawa yenu.
 
kwani michango huko ulipo ni lazima? mi huwa sichangi hata nikipewa kadi labda awe ndugu wa karibu sana.
 
Tuliwahi kuchangishwa ofisini hivyo hivyo kwa mkwara mzito, halafu ofisi nzima kadi ya mwaliko akapewa mtu mmoja eti atuwakilishe wote, kisa ilikuwa imepangwa bwana harusi apewe zawadi ya gari!
 
hongera tumejua una kabati languo na koti la suti sjui na suluali yake unayo au? mi nampa hongera hiyo hela akaanzie maisha
 
tatizo lako huna subira.
mpago mzima upo siku ya kuvunja kamati wee subiri mualiko tu utapenda.
 
usiombe mtoto wa boss ofisini ndio awe anaoa utajuta maana kuna watu kwa kujipendekeza kwa boss hutoa hata laki 5 ya mchango...
 
Hahahahahahahahaaaa!!!!!!! michango hii itatuua
 
Back
Top Bottom