Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Habari za leo,

Jamani hili swala la michango harusi naona limekuwa jipu, tena jipu lililoota kwenye paji la uso.
Mtu anakuomba mchango wa harusi, alafu anakuwekea kiwango cha chini kuchanga.
Mwisho wa mwezi huu wa tano imenitoka Tsh 950,000 kwa michango mbali mbali. Sasa najiuliza kwa mshahara upi enzi hizi za JPM??

Usipochanga, muomba mchango anajenga uhasama mbaya, hata salamu hapokei

Hivi kwa mwendo huu, na kwa kipato chetu kidogo, maisha yatakuwaje.

Jamani tubadilike
Heh wee bado unachangiaga, labda nikupe elfu 5
Dahh
950000
Ungeweza kununua ata till za tigo pesa, mpesa, airtel money, kwa 500000 zote nyingine zikawa mtaji
Ukaweka mwamvuli na kuajiri mdada
Kwa mwezi zote ungepata 500000
Kwa mwaka zaidi ya 6000000
Kwa miaka kumi 60,000000
Siyo lazima ziwepo cash ila ungeweza kusolve matatizo ya zaidi ya sh 60,000,000 ata zaidi kwa mtaji huo
 
Hahaha easy as that, ushawahi fanya biashara ya mpesa, tigo pesa? Au uko bize na RIFARO
 
Watu wengine wanapofuatilia hiyo michango mzigo ya harusi kwa kukupigia simu ukiwajibu kuwa umeshindwa kabisa kupata hiyo pesa ya mchango utasikia anasema "haya bhana" na kukata simu. Baada ya hapo ni kununiana tu kiaina. Nuna upasuke, unataka nikaibe ili nikuchangie?!
 
Heh wee bado unachangiaga, labda nikupe elfu 5
Dahh
950000
Ungeweza kununua ata till za tigo pesa, mpesa, airtel money, kwa 500000 zote nyingine zikawa mtaji
Ukaweka mwamvuli na kuajiri mdada
Kwa mwezi zote ungepata 500000
Kwa mwaka zaidi ya 6000000
Kwa miaka kumi 60,000000
Siyo lazima ziwepo cash ila ungeweza kusolve matatizo ya zaidi ya sh 60,000,000 ata zaidi kwa mtaji huo

I LIKE IT
 
Bado hatujielewi,kiukweli inakera sana hasa kwa sisi wafanyakazi unakuta huna kitu lakini kundi fulani lenye kiherehere linakutangaza ofisi nzima kuwa unajitenga,yani ni jipu tena yale ya kwenye makwapa.
 
Jifunze mitusi, tena ile mizito au kama hujui siku ukichokozwa na wapuuzi hao nitafute.

Kama mtu anataka kuoana, huo ni mpango wake. Mfikirie kwa mujibu wa sera na kipato chako. Mimi kipato changu kinaishia kwenye mambo ya muhimu, hiyo ya yeye kuoana, kugegedana na baadaye kupena mimba ni mipango binafsi na demu/mume demu wake.
 
Bado hatujielewi,kiukweli inakera sana hasa kwa sisi wafanyakazi unakuta huna kitu lakini kundi fulani lenye kiherehere linakutangaza ofisi nzima kuwa unajitenga,yani ni jipu tena yale ya kwenye makwapa.
Kwa kweli kwenye hili suala la michango ya harusi ni kero kwa watu wengi. Tumekuwa wehu na wendawazimu wa kushabikia mambo yanayorudisha nyuma maendeleo ya watu. Ukitaka kuwaudhi watu pitisha mchango wa jambo lolote kama ada za shule, kuuguliwa mgonjwa nk halafu uone utakavyochangiwa kwa masononeko.
Jamani tuwe wakweli hii karaha inatuudhi, halafu maharusi wenyewe baada ya siku si nyingi utasikia wametengana na mke kivyake na mume kule!
 
Mie yamenikuta na hivi ninavyoongea yapo motomoto, kuna mwalimu wa shule ya msingi ni kabila langu ana sendoff ya mwanae, ameniomba mchango wa kamati nikamwambia wazi kuwa mimi sina mpango wa kumchangia kwa kuwa nina majukumu yangu mengi ya kifamilia, nikiwa na maana kuwa tayari nimeweka vipaumbele vyangu katika malengo yangu kwa mwaka huu, yaani huyu dada kaninunia na hakuishia hapo amekwenda hadi kunishitaki kwa walezi wa chama cha kabila letu hapa nilipo, jana nikaitwa na hao wazee wakanihoji kwanini nimemjibu mwenzangu kwa lugha kavu namna hiyo!!!!!
 
Bora kuwa muwazi kuliko kufichaficha. Upo sahihi wala usihofu. Mimi nimeamua kuanza kuwakatalia watu maswala ya michango. Nachangia ndugu tuuuu. Kitchen party sichangiii kabisaaaaa hata kwa ndugu sichangii.
 
Na mie ninameweka msimamo huo huo, yaani hapa nilipo ni majanga unakuta unaletewa kadi hata 4 halafu zote sherehe ni mwezi Septemba mwaka huu, nimetafakari nikaona huu ni ujinga, hata mie siku nikiwa na shughuli yangu nitaifanya kulingana na uwezo wangu wala sitamchangisha mtu zaidi ya wana ukoo
 
Mimi pia nimeshaamua hivyo, ninaamini watu watanizoea tu, hamna namna nyingine, mtu unaletewa kadi zinazidi hata mshahara wako!!!! Hili jipu ni kubwa mno kulitumbua. Mimi mwenyewe kwenye shughuli yangu za wanangu nitafanya kwa uwezo wangu na zaidi nitashirikisha ndugu zangu ambao tumekuwa tukisaidiana kwenye shida na raha. Kwa ujumla ndoa haina gharama, bali gharama zinaletwa na ulimbukeni wa watu kutaka makuu na wengine wanataka wapatie mitaji humohumo kwenye michango ya watu.
 
Ndoa mpange nyie kwa mapenzi yenu wenyewe,
Mchango nikatoe mimi,
Hell No!!

Kama zawadi okay nitatoa,
Ila sio mchango na zawadi juu,
Tena unakuta harusi zngn zinafanyika mbali, ujigharamie na usafiri, khaaaah!
Toooo much pilipili.
 
Nikikupa mchango wa Harusi ujue Mke mtarajiwa atakuja kunisaidia shida yangu siku moja.....
 
Back
Top Bottom