Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

mkuu kuwa kama mimi tu sitaki kadi niambie unaoa au unaolewa niamue mwenyewe kuchangia au lah.. usinipe mkadi wako ukanitia stress na watu wengi wanaelewa hivyo huwa wananifanyia hivyo so sina kadi .... me sitachangisha mtu kwenye sherehe yoyote.. tukutane kwenye michango muhimu ya kufiwa, maradhi na nk nitachangia
[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15]
 
Neema iwe kwenu.
Michango ya harusi inanirudisha nyuma kimaendeleo. Nina kibarua mahali na ninalipwa hela ndogo tu wala haizidi laki 8, sasa kila nikiibajeti kufanya mambo yangu nakutana na kadi ya mchango wa harusi (kitchen party, send off etc). Halafu cha kushangaza ni kwamba hizi kadi za michango zinatoka nyingi kwa wanawake ambao ni ndugu, jamaa na marafiki. Katika kadi za mchango tano naweza pata labda moja tu toka kwa mwanaume.

Hapa kwa kweli nikiangalia na kutafakari kutusua itakuwa ngumu sana, niko social hivyo wigo wangu ndugu, jamaa na marafiki ni mkubwa na hawasiti kunipa kadi.

Wenzangu mlio katika hali kama yangu mnafanyaje?
HAKUNA NAMNA NI WATANZANIA KUBADILIKA NA KUACHA KABISA MFUMO HUU WA KUENDESHA HARUSI ULIOPO
IRUDI KAMA ZAMANI HARUSI IFUNGWE KANISANU/MSIKITINI WATU WAENDE NYUMBANI WALE PILAU NA MAJI,WATAWANYIKE.
 
Kwanini unachangia mkuu? Wakati unajua huna uwezo wakuchangia?
 
Kuna mambo nitafundishe wanangu hapa:
Kwanza kuchangia harusi ni 'inborn character' ,kama una roho ya Korosho-uchoyo hata mchango wa shilingi 100 hutachanga.

Pili,Kwa kutoa. ndio utapokea,hiyo ni kanuni kuu,usitegemee kupokea tu' mwanamke anapokea manii anatoa mtoto'

Hela huzikwi nazo,unapokea ili utoe 'thats life'

Kama una roho korosho kaa pembeni pisha wachangiaji!

Fiesta mliimbishwa 'imooo' usiku kucha huku umesimama na umelipa elf 20 na kinywaji ukajinunulia alafu kamchango ka elf 40 (single) tena unaombwa miezi mitatu kabla ushindwe?
 
Wandugu,

Leo napenda kuwakumbusha kuwa kwa kujidai wewe ni mwema kwa kuchangia kila harusi iliyo mbele yako, unajimaliza mwenyewe (nakulinganisha na mtu anayepiga punyeto a.k.a punyere kwa kuangalia picha za utupu mtandaoni).

MBINU YA KUKWEPA MICHANGO
Usiwe na maneno ya diplomasia kwa anayeomba mchango, mjibu live kuwa mi sikupi mchango na usinisumbue *****! Kwa jibu hili atapanic na hatarudi tena kwako, kisha chukua hiyo 100,000 au 200,000 kaweke akiba kuwa na malengo baada ya mwaka una akiba ya kutosha.
 
Wandugu, leo napenda kuwakumbusha kuwa kwa kujidai wewe ni mwema kwa kuchangia kila harusi iliyo mbele yako, unajimaliza mwenyewe (nakulinganisha na mtu anayepiga punyere a.k.a punyere kwa kuangalia picha za utupu mtandaoni).
MBINU YA KUKWEPA MICHANGO
Usiwe na maneno ya diplomasia kwa anayeomba mchango, mjibu live kuwa mi sikupi mchango na usinisumbue *****! Kwa jibu hili atapanic na hatarudi tena kwako, kisha chukua hiyo 50,000 au 100,000 kaweke akiba kuwa na malengo baada ya mwaka una akiba ya kutosha.
Mimi nagombana na dada yangu kuhusu kufunga harusi. Yeye anataka nifunge harusi ila mimi sitaki.
Hoja zangu ni
1. Kuishi na mwanamke kama mke na mume ndio ndoa yenyewe.
2. Harusi haifanyi ndoa iwe imara au isiwe na matatizo..
3. Sina uwezo wa kugharamia harusi kwa 100% kwani nikitaka kamati ndo kujiingizi kwenye chama kisicho rasmi cha kuchangiana harusi. Maana hawa watu awe anakujua au hakujui ili mradi anajua au kaambiwa alifanya harusi lazima utaletewa kadi.
Hoja za dada
1. Kufanya harusi kunafanya jamii ielewe kuwa huyo ni mkeo. Swali langu ni Je nikihama hapa Kyela na kwenda kuishi sehemu nyingine itanibidi kufanya harusi nyingine?
2. Ni utaratibu wa kiMungu. Swali/maswali yangu Wapi imeelekezwa katka kitabu cha Mungu kwamba tufanye harusi yuoapo? Baba wa Imani Ibrahim alifanya harusi wapi? Je mfalme Suleiman na wanawake zaidi ya 700 alifanya harusi?

Kufanya harusi ni kujiingiza ktk seke seke la uchangiaji wa harusi kwenye chama kisicho rasmi cha waoa kwa harusi.
Nitafanya harusi iwapo tu nitaweza kugharamia harusi yangu mwenyewe, sitaki kutembeza bakuli.
 
Mkuu umeniwahi kuanzisha uzi kama huu, nilikua nawaza kuuleta humu, Ingawa si vizuri kutumia maneno harsh lakini hii michango imezidi sana na watu hawajalishi uko umbali gani ilimradi kuna WhatsApp na fb anakuforwadia tu card anataka mchango na msg za kukumbusha kila siku mbaya zaidi unakuta huyo mtu hamjawasiliana miaka 3 au 4 nyuma aakutafuta kwenye mchango tu.
Unakuta watu wamekaa miaka 5 wanapika na kupakua ila mwisho wanataka harusi mpaka honeymoon waende.
Ni ulimbukeni mkubwa nadhani sisi vijana tufike pahala tufanye vitu kulingana na uwezo. Funga ndoa rudini nyumbani mnywe chai na mikate kama kawaida au ugali nyama kwa sababu hata ufanye harusi ya aina gani hakuna atakaekusifia. Siku hizi naona watu wanachofaidika nazo ni zile picha zinazopigwa siku ya harusi watu wanazipost kama wiki kwenye mitandao ndio furaha inayopatikana.
 
Hauna tofauti na anayesema "usingekua unakunywa ungekuwa unamiliki ghorofa" wanasema kutoa ni moyo si utajiri....
 
Tokea mwaka jana niko katika harakati za kuacha kwani nimekuwa natoa 0.5 tu ya kiasi kinachoombwa. Na kuanzia mwaka huu naanza kutoa robo ili mwakani niachane kabisa hata kutoa senti yangu. Niliokwisha kuwachangia wanatosha make siwezi kutoa pesa as if sina kazi za maana za kufanyia. Ndugu zetu wagonjwa sie tuko busy kuchangia harusi, wazazi hawana pesa ya kutumia wewe uko busy na kuchangia harusi tena kwa mamia ya maelfu ..michango haivumiliki tena
 
Mkuu umeniwahi kuanzisha uzi kama huu, nilikua nawaza kuuleta humu, Ingawa si vizuri kutumia maneno harsh lakini hii michango imezidi sana na watu hawajalishi uko umbali gani ilimradi kuna WhatsApp na fb anakuforwadia tu card anataka mchango na msg za kukumbusha kila siku mbaya zaidi unakuta huyo mtu hamjawasiliana miaka 3 au 4 nyuma aakutafuta kwenye mchango tu.
Unakuta watu wamekaa miaka 5 wanapika na kupakua ila mwisho wanataka harusi mpaka honeymoon waende.
Ni ulimbukeni mkubwa nadhani sisi vijana tufike pahala tufanye vitu kulingana na uwezo. Funga ndoa rudini nyumbani mnywe chai na mikate kama kawaida au ugali nyama kwa sababu hata ufanye harusi ya aina gani hakuna atakaekusifia. Siku hizi naona watu wanachofaidika nazo ni zile picha zinazopigwa siku ya harusi watu wanazipost kama wiki kwenye mitandao ndio furaha inayopatikana.
Kuna wadada tulisoma wote chuo miaka minne imepita sasa tumeonana barabarani huko...eebwana kumbe wanatembea na kadi ambazo hawajaandika majina ile timesalimiana kumbe kanisahau jina maana tulikuwa hatuna mazoea, nikaulizwa jina langu eti nimkumbushe..nikamtajia akawa anatoa kadi eti mwenzio nafunga ndoa akaandikia jina palepale na kunikabidhi yaani hadi namba ya simu alikuwa hana.....kwenye michango watu wanapenda kumshirikisha kila wanaemuona mbele yao. Wengine SMS kila mara utafikiri akioa atanipa huyo mke wake.....mm nina makadi mengi huwa nayaweka ndani pasipo kuchangia bahati nzuri nasafiri mara kwa mara so hainipi shida
 
Mimi nagombana na dada yangu kuhusu kufunga harusi. Yeye anataka nifunge harusi ila mimi sitaki.
Hoja zangu ni
1. Kuishi na mwanamke kama mke na mume ndio ndoa yenyewe.
2. Harusi haifanyi ndoa iwe imara au isiwe na matatizo..
3. Sina uwezo wa kugharamia harusi kwa 100% kwani nikitaka kamati ndo kujiingizi kwenye chama kisicho rasmi cha kuchangiana harusi. Maana hawa watu awe anakujua au hakujui ili mradi anajua au kaambiwa alifanya harusi lazima utaletewa kadi.
Hoja za dada
1. Kufanya harusi kunafanya jamii ielewe kuwa huyo ni mkeo. Swali langu ni Je nikihama hapa Kyela na kwenda kuishi sehemu nyingine itanibidi kufanya harusi nyingine?
2. Ni utaratibu wa kiMungu. Swali/maswali yangu Wapi imeelekezwa katka kitabu cha Mungu kwamba tufanye harusi yuoapo? Baba wa Imani Ibrahim alifanya harusi wapi? Je mfalme Suleiman na wanawake zaidi ya 700 alifanya harusi?

Kufanya harusi ni kujiingiza ktk seke seke la uchangiaji wa harusi kwenye chama kisicho rasmi cha waoa kwa harusi.
Nitafanya harusi iwapo tu nitaweza kugharamia harusi yangu mwenyewe, sitaki kutembeza bakuli.
Mkuu, Mtu akiugua watu wanachanga elfu (2,000) lakini harusi wanakuletea kadi elfu(50,000).Mm nilishajitoa kwenye huo mfuko,,,,!
 
Tatizo wengi wanapenda harusi sio ndoa. Yaan lile bonge la sherehe,mbwembwe nyingi bila kujali wanafilisi watu(waalikwa)shela kali,suti bomba,zawadi baada ya hapo maisha ya maharusi huwa sio yanayotegemewa.kuta zinaficha mengi.
 
Kuna wadada tulisoma wote chuo miaka minne imepita sasa tumeonana barabarani huko...eebwana kumbe wanatembea na kadi ambazo hawajaandika majina ile timesalimiana kumbe kanisahau jina maana tulikuwa hatuna mazoea, nikaulizwa jina langu eti nimkumbushe..nikamtajia akawa anatoa kadi eti mwenzio nafunga ndoa akaandikia jina palepale na kunikabidhi yaani hadi namba ya simu alikuwa hana.....kwenye michango watu wanapenda kumshirikisha kila wanaemuona mbele yao. Wengine SMS kila mara utafikiri akioa atanipa huyo mke wake.....mm nina makadi mengi huwa nayaweka ndani pasipo kuchangia bahati nzuri nasafiri mara kwa mara so hainipi shida
Hahah huyo ungempa jina la uongo tu mkuu
 
Back
Top Bottom