Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Jamani wanajamvini, imenibidi tu nije nitoe dukuduku langu huku jamii forum, kiukweli kuna huu mtindo wa kufunga ndoa ambapo huwa unaambatana na sherehe kubwa inayogharamiwa na michango ya hiari toka kwa ndugu na marafiki. Huu utaratibu umekuwa ukiathiri watu mbalimbali kiuchumi nikiwemo mimi, ambapo unakuta mtu kila mwezi unapata kadi c chini ya 6, na kila moja ni 50 elfu kwenda juu, hii inatokana na jamii ya kijamaa tuliyonayo watanzania ambapo tunakuwa na ukaribu na wetu wengi.
Kiukweli nimechanga nimechoka, na ninaomba tu litoke tamko kuwa kila mtu anaetaka kuoa basi agaramie harusi yake. Mana imekuwa kero. Unachopata kidogo wanataka uwape halaf wewe hufaidiki na kitu chochote yani ni kama umetupa hela. Huu utaratibu kwa nchi za wenzetu hamna. Wao wanachofanya ni kuchanga tu kizawadi tena co lazma.

Kwa usawa huu maisha magumu halaf unakuja kutuomba tukupe ela ukanunue mwanamke(kuoa) hapana . Watanzania tubadilike.

Mtu kodi sijalipa. Nadaiwa mikopo na wewe eti unakuja nataka kuoa unichangie mfyuuuuuuuuu matulu yako
 
That is the cost of being social. If you want social acceptance you pay for it. Wengine tumeamua ku dump marafiki wote na kujikita huku JF kwa kuwa marafiki wa huku huwa hawachangishani 🙄🙄🙄.
Mimi hizo habari nishazikataa. Unachangia watu pesa nyingi alafu umepanga kwenye chumba kimoja. C bora hizo pesa uwanyime ukazitumie kupanga nyumba nzuri...
 
mh!mtoa mada kama umeniona vilee!toka mwezi Wa 4 mpaka mwezi Wa 10 kwenye mshahara wangu inapungua kama sio elfu 50 basi ni tsh 100000!

ila sasa nimeamua kuwa kuanzia mwaka mpya 2018,sitachangia wala kushiriki kwenye kamati ya harusi ya MTU!ukitaka harusi make sure umejipanga mwenyewe!mi niitwe kukushangilia tu!

mi mbona kwenye ndoa yangu sikusumbua mtu?na niliamua tu kuwa iishie garden, SAA tatu usiku sherehe iliisha!
 
Usichange mkuu hakuna atakaye kuuliza ila nawewe ukitaka kufunga ndoa na hilo jishangazi usituchangishe pia
 
Afadhali mtu kama ungekuwa unapata pesa za kifisadi kama singa singa senge sigh au rugemarila ambazo hata ukitoa haziumi
 
Back
Top Bottom