Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mwanangu yupo chekechea, simchangii mtu ng'o mpaka akaribie kuoa. Mimi nilioa kwetu magu kwa ng'ombe tu sikuchangisha mtu. Sitaki michango bado nalea. Nasubiri iwe nipe nikupe 20 years to come
 
jamani hii sheria landa ipite mimi nikiwa nimeshafunga harusi sio siri kipindi nipo home nimechangishwa saaana na nilikuwa natoa na majina ya woote ninayo yapo kama 60 hivi yaani nikianza matayarisho wa kuwaanzia ni hao na siku hizi viwango vimepanda ni tsh 70000 kuna kama 4,200,000/= ya haraka haraka hela ya ukumbi tayari hapo na mc najua linatuumiza sana ila hatuna jinsi.
 
Mbona Million 4.2 inatosha kabisa.
 
Kiranga huyo dada ana point.. kwa mila zetu za kiswahili... Utasikia watu wakisema " mama flani anaozesha mwanaye" mara nyingi wazazi ndio wanataka makuu.. wanaona fahari harusi ya bint/ kijana wao inapokuwa kubwa mno

Acheni maisha ya kupangiwa na wazazi, mtu mzima unaoa/olewa bado unapangiwa maisha na wazazi?

Tumefikia muda kuwapumzisha wazazi na kufanya shughuli hizi wenyewe vijana.Wazazi wenye hekima watashukuru.
 
Sijui ndo tuziite mila za Kiswahili ama Kiafrika...haijalishi.

Ila kama ni mila kweli basi ni zile mila za kipuuzi.

Ndoa yako mwenyewe halafu kupanga wakupangie wengine? Hicho ni kilele cha ujinga.
 
Hahahahaha! Kumbe mmeliona eeee! Mimi nilishaachana na hiyo biashara. Ni Upumba.. kabisa. Eti mtu anapanga chumba kimoja harafu hataki harusi inayolingana na uwezo wake? Shen.. kabisa. mimi siku hizi sikatai kadi za michango ila zote zinaishia dust-bin. Tumezoea sana watanzania kugawana umaskini. Bora ndoa zenyewe zinazoharibu budget zetu zingekuwa zinadumu basi, mwaka haujaisha watu wameachana harafu eti tuendelee kuharibu budget? Kudadade..
Nimetafuta LIKE kwenye mchina wangu siioni. Ngoja nitafute laptop ni log in.
 
Tatizo m2 akikuletea kadi hlf ukampotezea kamati nzima ina ku-mind.
Yaani unaongeza list ya maadui, lo! Inakulazimu utoe hata kama home hali si shwari.
 
Mwanangu yupo chekechea, simchangii mtu ng'o mpaka akaribie kuoa. Mimi nilioa kwetu magu kwa ng'ombe tu sikuchangisha mtu. Sitaki michango bado nalea. Nasubiri iwe nipe nikupe 20 years to come

Mkuu ni kweli michango ya harusi imezidi usipokuwa makini mshahara wote unaweza kwisha
 
wakati wa mwalimu ilikuwa ni ndg wanakuja na makapu yaliyojaa vyakula maarufu ktk mji huo, wakiwa wamejipamba kiasiri na nyimbo za kitamaduni. Leo hii kadi kima cha chini laki! Wizi mtupu!!
 
Acheni maisha ya kupangiwa na wazazi, mtu mzima unaoa/olewa bado unapangiwa maisha na wazazi?

Tumefikia muda kuwapumzisha wazazi na kufanya shughuli hizi wenyewe vijana.Wazazi wenye hekima watashukuru.

Sijui ndo tuziite mila za Kiswahili ama Kiafrika...haijalishi.

Ila kama ni mila kweli basi ni zile mila za kipuuzi.

Ndoa yako mwenyewe halafu kupanga wakupangie wengine? Hicho ni kilele cha ujinga.

nimewaelewa binafsi sikubaliani na hili jambo hata kama nikija kupata mchumba na kuoa nisingependa harusi iwe kubwa vile lakini hili jambo likishafika kwa wazazi wakuu espicially wazazi wa kike "mama" anakuwa exicited sana tu na pia kuna usemi kuna usemi "kawaida ni kama sheria" .. watanzania walio wengi hii kawaida washaifanya ni sheria! itachukuwa muda kuja kuachana na hili jambo
 
Ndiyo maana tunabaki masikini.

Tunafanya kawaida sheria hata pale inapoturudisha nyuma.

Hata hizo sheria zisizo maana hubadilishwa, itakuwa hiyo kawaida?

Mpaka jamii zetu zitakapojifunza kuwa practical, na kuacha kuishi kwa ajili ya kuonekana na watu, tutaendelea kuwa masikini.

Kila mtu atafanya maamuzi si kwa sababu yako practical, bali kwa kuangalia "jirani atanionaje, rafiki atanionaje, wazazi watanionaje".

Tutakuwa hatuishi kufanya harusi za kifahari halafu kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa harusi madeni mengi, stress, hata ndoa inakosa amani.

Jambo la neema linageuka such a big unnecessary production.
 
Tatizo m2 akikuletea kadi hlf ukampotezea kamati nzima ina ku-mind.
Yaani unaongeza list ya maadui, lo! Inakulazimu utoe hata kama home hali si shwari.

Tujue kusema "hapana, sina hela, bajeti yangu hainiruhusu"

Ama sivyo utaua watoto bure kwa kuogopa kusemwa vibaya.
 
jamani hii sheria landa ipite mimi nikiwa nimeshafunga harusi sio siri kipindi nipo home nimechangishwa saaana na nilikuwa natoa na majina ya woote ninayo yapo kama 60 hivi yaani nikianza matayarisho wa kuwaanzia ni hao na siku hizi viwango vimepanda ni tsh 70000 kuna kama 4,200,000/= ya haraka haraka hela ya ukumbi tayari hapo na mc najua linatuumiza sana ila hatuna jinsi.

Kwa hiyo wewe unachangia watu ili ufanikishe harusi zao au unachangia watu kama unawekeza na wewe wakuchangie?

Kama unachangia na wewe wakuchangie, ashakum wakifa kabla ya wewe kuoa utafanyaje?

Kwenye misiba hii watu wanalia mengi, wengine wanalia mtu kafa, wengine wanalia kafa kabla ya kuwachangia mchango wa harusi.
 
Mwanangu yupo chekechea, simchangii mtu ng'o mpaka akaribie kuoa. Mimi nilioa kwetu magu kwa ng'ombe tu sikuchangisha mtu. Sitaki michango bado nalea. Nasubiri iwe nipe nikupe 20 years to come

Miaka 20 ijayo unajuaje kama harusi zitakuwepo bado kama leo? Inawezekana kutakuwa hamna harusi bali za watemi tu.

Watu wengine wote inaelekea watatia akili na kuchukuzana tu.Usishangae ukapewa utambulisho tu ukakoma na roho yako mwenyewe.
 
sawa sio lazima uchange lakini unakuta ofisini kuna watu km wanne hv wanaoa na kuolewa,then mtaani huko nako km umepanga mtt wa mwenye nyumba naye anaoa umeletewa kadi bado marafiki zako nao wanakuomba uwachangie... yaani kasheshe kwakweli.maisha yanazidi kuwa magumu na hii michango... alafu siku hz ukitaka kuchangia unaambiwa kianzio 70000 tena hapo kakufanyia kishigaji tofauti n ahapo ni 100000.duh tutafika kweli?
Kipindi cha ada za shule kama ume note, michango inakuwa mingi sana mara ujenzi wa kanisa,harusi, na mingine mingi! Yote ni namna ya kukusanya ada na mambo mengine, maisha yamekuwa magumu!
 
Kwa hiyo wewe unachangia watu ili ufanikishe harusi zao au unachangia watu kama unawekeza na wewe wakuchangie?

Kama unachangia na wewe wakuchangie, ashakum wakifa kabla ya wewe kuoa utafanyaje?

Kwenye misiba hii watu wanalia mengi, wengine wanalia mtu kafa, wengine wanalia kafa kabla ya kuwachangia mchango wa harusi.

mkuu kufa ni matokeo ila kama kuna ukweli hapo. ha ha ha ha ha
 
nimewaelewa binafsi sikubaliani na hili jambo hata kama nikija kupata mchumba na kuoa nisingependa harusi iwe kubwa vile lakini hili jambo likishafika kwa wazazi wakuu espicially wazazi wa kike "mama" anakuwa exicited sana tu na pia kuna usemi kuna usemi "kawaida ni kama sheria" .. watanzania walio wengi hii kawaida washaifanya ni sheria! itachukuwa muda kuja kuachana na hili jambo

Hutakiwi kusubiri watanzania wengi waliache. Wewe fanya yako vile unavyotaka, watanzania wengine waache wafanye watakavyo. Uhuru wa mawazo huanzia ngazi ya familia, kama hata harusi yako mwenyewe hupati uhuru wa kuipanga usitegemee uhuru wa kuamua kuhusu mambo makubwa zaidi ya jamii.
 
nina kadi 4 mezani..naenda zitia moto.. Hata kujenga bado sijaanza
 
nadhani sasa m2 akitaka kuoa au kuolewa,wajipange sio kuchangisha watu cz ts becaming too much.ela yote yaishia kwenye michango mpk unashindwa kufanya maendeleo yako... au wadau mnasemaje?
Yaani mimi kwangu mku ndio usiseme,ninachangia harusi tokea mwezi June mfululizo,imefikia mpaka sasa nabana bajeti ya home ili nichangie harusi it's too much!
 
Back
Top Bottom