Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Amua tu mkuu, weka msimamo, na isikusumbue watu wengine watakuonaje.Nikupe mfano, mimi hiyo biashara ya kuchangia harusi nilishaona haifai ..... nimeiacha siku nyingi sana .....sichangii, saaaana nikiamua kukupa mchango ni shilingi za kiTanzania elfu ishirini tu. Sababu ni kuwa siamini ktk dhana hiyo.Nachangia mambo mengine ya muhimu na maendeleo zaidi.Ila kama na wewe unaamini na unategemea kuwa utawahitaji waje kukuchangia harusi yako siku zijazo ............

Mkuu, mie nilioa siku nyingi sana! Sikuwachangisha, na wala by then hawakuiona thamani ya ndoa yangu! Hivyo hata hongera zao sijawahi kusikia wakinipa tangu nimeoa, hata kuulizia watoto wangu ambao ndiyo matunda ya ndoa, sijawasikiaga!
 
michango ni jambo la hiari, na kutoa ni moyo wala sio utajiri. cha muhimu usimchangie mtu ikiwa moyo wako hauko radhi na wala usichange zaidi ya uwezo wako kwa kutaka ufahari au kumridhisha mtu.
 
jamani nina olewa mwezi wa nane naombeni mnichangie msinichanganye hapa wala nini!! mbona ulabu mnapiga kama kawa.
 
Hiyo makitu niliacha muda sana na uzuri wote wanaonizunguka wanajua msimamo wangu, kwamba sichangia harusi.
 
nani anakulazimisha ndugu yangu? Kama urafiki ni kuchangiana michango ya ndoa basi hamna haja ya urafiki wa namna hiyo!!!
 
Hapo hamna hata urafiki lolz.. Ni kulazimishana tu..

Sichangi .. Akinuna anune tu for gud.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Utakapo oa wewe utajua umuhimu wake, vinginevyo funga ndoa ya mafungu
 
Unajua hii michango inaumiza sana ni bora jamii ikabadili mtazamo . Harusi unaifanya mwenyewe kwa kadiri ya uwezo wako. Mimi huwa nachangia sana elimu na maendeleo mengine kwenye harusi nilishaga toka manake kuna watu wanadai hadi unajisikia vibaya. Nakumbuka mwaka 2011 tuliifanya shereha ya mdogo wetu na hatukuchangisha mtu na sherehe ilikua nzuri tu . So tujitahidi kufanya sherehe kwa kadiri ya uwezo wetu pasipo kuumizana. Tuwezeshane kifamilia ili matukio kama ya harusi yajapo basi tuchangishane kifamilia na marafiki wachache.
 
michango ya harusi ni KERO .. inabidi tubadilike tu ndugu zangu... funga ndoa .. fanya kasherehe kakishikaji picha za ukumbusho Beach , m.city au kwenye bustani za jiji maisha ya endelee .. sas unakuta harusi bajeti 10M .. hiyo si unapata gari ya kuendea kazini na chenji inabaki...
mimi hii kitu naipinga nantaipinga kwa nguvu zote.. michango ya harusi ni kiashiria cha umaskini hakuna jipya..
 
hata mie siipendi hii mambo ..vikao ni npesa utafikiri tunaenda kutokomeza umasikini Afrika nzima
kweli dunia ina mambo sana ....narudia sipendi mimi sitachangisha watu ntaita washikaji na ndugu watakaotaka kisela sio harusi kama mnataka kufanya mapinduzi makubwa siafiki na sitafanya ila ntachangia kidogo usinipangie kama vile natoa mahari naoa kwa watu wapenda hizo harusi nikiwa na bajeti zingine tusilaumiane
 
Kwanza kabisa, wakuu hongereni kwa sherehe za miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar! Pili, nitangulize samahani iwapo nita-sound vibaya kwa baadhi yetu kwani binadamu tumeumbwa tukiwa na mitazamo tofauti ktk masuala mbalimbali.
Leo nazungumzia juu ya MICHANGO YA HARUSI, hasa za siku hizi, nalisema hili bila kumung'unya maneno, utakuta mtu yuko Lindi, na wewe uko Mwanza, anadai kakuweka kwenye kamati kuu ya harusi yake na hivyo kadirio la chini utapaswa kuchangia Tsh. 100,000 na itakubidi uhudhurie sherehe hizo Lindi ukitokea Mwanza! Piga picha, utakuta mtu mwenyewe ulikutana nae Advanced Level miaka minane iliyopita na wala haujakutana nae tena zaidi ya kuongea naye kwa simu kwa interval ya mara moja kwa mwaka huku mkikumbushiana yalopita!
Harusi imekaribia utapokea sms mara tano kwa kutwa unakumbushiwa juu ya mchango wako! Usipotoa atanuuuuuna, atakuseeeeema.....! Hii imekaaje wakuu?
Naomba kuwasilisha.

Kama mlikuwa na urafiki wa kutosha enzi hizo na uwezo unao au kama yeye alikusaidia kwenye shughuli zako kama hizo unaweza kujitahidi kumchangia. Vinginevyo, unaweza kupima mwenyewe kwa kusukumwa na uwezo na upendo wako dhidi yake.
Ila siku zote kama una uwezo wa kumsaidia mtu, jaribu kumsaidia huenda mnaweza kukutana tena katika maisha au utafutaji. Milima haikutani bali binadamu hukutana.
 
Aliyeanzisha huu utamaduni wa kuchangiana harusi alaaniwe!

Bora hata tungekuwa tunachangaian mahari mtu akapate mke.
 
Utakapo oa wewe utajua umuhimu wake, vinginevyo funga ndoa ya mafungu

Mkuu mie nishaoa zamani saaana! Lakini pia sikuwahi kumchangisha mtu kwani nilijua kuwa hiyo ni kero, najua kila mtu ana mipango mingi na pesa zake!
 
Unajua hii michango inaumiza sana ni bora jamii ikabadili mtazamo . Harusi unaifanya mwenyewe kwa kadiri ya uwezo wako. Mimi huwa nachangia sana elimu na maendeleo mengine kwenye harusi nilishaga toka manake kuna watu wanadai hadi unajisikia vibaya. Nakumbuka mwaka 2011 tuliifanya shereha ya mdogo wetu na hatukuchangisha mtu na sherehe ilikua nzuri tu . So tujitahidi kufanya sherehe kwa kadiri ya uwezo wetu pasipo kuumizana. Tuwezeshane kifamilia ili matukio kama ya harusi yajapo basi tuchangishane kifamilia na marafiki wachache.

Well said, asante mkuu!
 
Aliyeanzisha huu utamaduni wa kuchangiana harusi alaaniwe!

Bora hata tungekuwa tunachangaian mahari mtu akapate mke.

Haahaaaa... Kweli mkuu! Au utakuta mtu kwenye msiba wa rafiki yake anatoa ulfu kumi, wakati kwenye harusi alimchangia laki moja.... Nonsense!
 
Back
Top Bottom