Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Mjadala: Kero za michango ya Sherehe katika jamii ya Watanzania

Michango si kodi.

Usilaumu michango kuzidi, jilaumu wewe mwenyewe kwa kushindwa kukataa michango.

In general, wabongo tumezidi unafiki wa kulalamikia pembeni, wakati watu wanaleta michango hatuwaambii kwamba tumezidiwa.

Kila mmoja angesema ukweli kuhusu hii michango ingepungua, na watu wangefanya harusi realistic zaidi. Tatizo tunailea wenyewe.

Moja ya vitu ambavyo sitakaa kufanya maisha haya ni kumchangisha mtu mchango wa harusi yangu.

wala sijalaumu ndo ukweli wenyewe na wakuleta mabadiliko ni mimi na wewe tuangalie zaidi katika kusaidia mtu anapokuwa anaumwa, ada za shule na kusaidia watoto yatima. sio kusubiri mpaka mtu anafariki ndo tunatoa michango kwa kujionyesha pamoja na harusi. Changes ni mimi na wewe nafikiri umenisoma.
 
Kuna harusi mama alichangia million 5,
Shemeji million 10.mimi sikutoa kitu na sikwenda nilikuwa mbali.
Ata mwaka aikupita ndoa ikafa. Uyo binamu yangu wa kiume alikuwa kicheche na mlevi. Na uyo binamu alikuwa choka mbaya tu kila kitu amefanyiwa wala awez kuona uchungu.
 
Nilihudhuria moja nchi za wenyewe Magharibi, nilijinunulia msosi na vinywaji tu. wahusika bride&bridegroom walikuwa wame save for their wedding for about three years. they never imposed any burden not even to their own parents!

Tanzania tubadilike! Mgonjwa anahitaji operation costing 10M We don't give a dime! Mtoto anahitaji scholarship 20M, nobody cares! Harusinya 80M Mlimani City tunachanga 1M as if it was only 10k! Very sad indeed!

PP
 
Nafungua kampuni ya bima ya ndoa,yani kwa maisha yalivyo sasa ivi ni bora tuwe na bima ili ikivunjika unaweza pata compasation!#fursa#
 
Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni, licha ya kabila la Wazaramo kutupiwa kila lililobaya lakini tunapaswa kujifunza kitu kutoka kwao.

Hawa Wazaramo sendoff ni jukumu la wazazi wa kike na wedding party ni jukumu la muowaji fullstop.

Haijarishi parry ni kweny disco vumbi au rusha roho barazani kwa wakwe but marriage is done na ukiwa na laki 5 unafanya bonge la sherehe ya kufa mtu.

Tatizo la mitanzania anataka sherehe yake ifanane na ya muuza sembe. Inshort sichangii harusi kwa sasa baada ya last michango yetu kwenda kulipia ukumbi pale quality center a lot of money wakati Msimbazi center Cardinal hall ni only one million na mbaya zaidi watu wanapiga pesa ndefu kwenye kamati na kwenye kutoa tenda. Pesa ya dharura inapangwa kama million 1 na hakuna dharura inayotokea na mpaka kamati inavunjwa hakuna pesa inayorudishwa.

Mtu yeyote akiamuwa kusema basi na utaheshimika na hutofatwa kwa ajili ya upumbavu.

Michango yangu sasa inaelekea kanisani zaidi na School fees period.

Kama una shida tutasaidiana pesa lakini siyo kupigana mizinga hovyo, nimepita kwenye difficult time sipendi uppuuzi na wala siupi nafasi.
 
Kwa hiyo laki yako moja inanunua miaka mingapi?

Toa milinganyo kabisa watakaotaka kukaa mika 60 kwenye ndoa wajue wakuchaji milioni ngapi.

Kwamba "jamaa anataka kwa laki yake moja tukae kwenye ndoa angalau miaka mitano, sisi tunapanga kukaa miaka 60, 60/5 = 12, kwa hivyo "mchango" sawa wa kudai ni laki mara 12, shilingi milioni 1 na laki 2".

Hapo vipi?
Poa tu! Isipotimia si kuna refund ya difference!

Au tuweke in installment basis (the rate at which i'm coming up with these ideas i should get copyright protection!) Kwa mfano mchango wa harusi ni laki moja for 5years. Mikmaliza hizo 5 years mnafanya sherehe tena tunawachangia 150!! Mkimaliza hizi 10 years tunawachangia kilo 2!

If i say so myself this will be the best way to maintain marriages!!Watu kila mkifikiria kuachana mnakumbuka incentive/compasation mtakayopata mkimaliza 5 years. Lol.
(People this is light talk, sio muanze ku get personal hapa na matusi!)
 
Kuna harusi mama alichangia million 5,
Shemeji million 10.mimi sikutoa kitu na sikwenda nilikuwa mbali.
Ata mwaka aikupita ndoa ikafa. Uyo binamu yangu wa kiume alikuwa kicheche na mlevi. Na uyo binamu alikuwa choka mbaya tu kila kitu amefanyiwa wala awez kuona uchungu.

Mi nilishawaambia watu pesa yangu sio kwa ajili ya harusi. Hicho ni kitu cha hiari so akinipa kadi asitegemee kwamba lazima nimchangie. Ila akiniomba nimsaidie ndugu yake anaumwa niko tayari kumlipia gharama zote za matibabu. Harusi ni upuuzi sana siku hizi.
 
Jamani hivi kuchangia harusi sasa imekuwa lazima?

Nahisi sasa harusi zinatuletea umasikini, yani mtanzania wa kawaida nina kadi tisa mpaka sasa.

Bado natafutwa na jamaa yangu mwingine, yani simu imejaa meseji za watu wanakumbushia michango.

Jamani hatuwezi kuwa na utaratibu mbadala kwenye hili swala? Tupungiziane stress.

Halafu na hii tabia ya mtu anakutumia tu ujumbe uje siku fulani mahala fulani kuna kikao cha harusi, kumbe kesha kuweka kwenye kamati ya harusi we bila kujua afu ukifika wanaweka kiwango cha kila mwanakamati kutoa.

Nadhani tuhitaji mbadala wa hili.
 
hakuna maana yoyote kuchangia harusi,wakati tunashindwa kuchangia masuala muhimu kama elimu na afya.

mlo wa kunywa kwa siku moja mamilion yanatekea,kama mtu anapenda kufanya harusi kubwa eti ili asifiwe e bwana harusi yako ilikuwa baraa, inabidi agharamike ye mwenyewe.kwa sasa kila mtu na mzigo wake mambo ya kusumbua watu na vitu visvyo na tija kama sherehe ya harusi tuwaachie wenye uwezo.
 
Kuna sehemu mmeambiwa ni lazima kuchangia?????!!!!
Umewahi kumjibu mtu kuwa hutaki kumchangia na akaendelea kukukumbusha???!!!


Michango sio taabu mnafiki ni wewe uliyepokea kadi ya kwanza mpaka ya tisa halafu unakuja kulalama huku
 
Kuwa na msimamo mmoja tu wa kutochangia. MIMI nilichaacha hayo makitu kitambo na ndugu zangu na marafiki huwa hawajisumbui kunipa kadi za mchango, sababu wote wanajua msimamo wangu. Kama kuna tatizo jingine sina tatizo. Ndoa ufunge wewe fedha tukuchangie sisi kwa starehe zako. Big NO.
 
Wewe chuna tu, mie nsha acha upuuzi huo wa utitiri wa harusi na michango. Nawashauri nyie mnaotaka kuoa, fanya harusi unayoweza kumudu wewe na familia yako, halafu alika watu kiasi unachoitaji. Kuomba mtu akuchangie, tena kwa kumbugudhi ni ujinga tunalea ktk jamii yetu. It begins with you, acha kuchangia harusi kama hauko tayari, watakuelewa tu.
 
Tatizo mtu anakupigia simu halafu anakuuliza hivi siku hizi unafanya kazi wapi??
Ukimtajia tu anakukadiria na kiwango cha mshahara unachopata halafu anakukandamizia na mchango hapo hapo.......
 
Back
Top Bottom