Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

muda si mrefu hapa moshi... mzee mmoja aliyekatwa mguu huko india kwa kusumbuliwa na sukari na mpaka kuwa anajipiga insulin ku control sukari na hata sukari kuanza ku affect macho yake...ameniambia amepona na tangu arudi ana siku nne hajui dawa wala insulin vipo wapi na macho yanapona .... mashuhuda ni wengi wengi waliopona .... JWTZ wameweka kambi zao za matent kuhudumia wanaotafuta tiba .. naambiwa pia red cross wapo njiani .... jana kulikuwa na watu zaidi ya elfu hamsini na magari 2000
 
Hili ni Taifa la watu wenye dhiki sana kwasababu ya viongozi wao wamewafikisha pabaya; mahala ambapo wengi wao na familia zao hawana uhakika wa kupata hata mlo mmoja kwa siku, hivyo kuzidiwa na maradhi ya kila aina. Katika environment kama hiyo ujue wazi mtu yeyote atakayejitokeza na kuwatia faraja katika matatizo waliyonayo huyo watamuamini; ndio maana siku hizi tuna madhehebu mengi ya dini na pia waganga wa kila sampuli. Hizi zote ni ishara za watu waliokata tamaa juu ya uborweshaji wa maisha yao.
 
Ni juzi tuu mkuu mmoja wa serikali alitangaza kua ugonjwa kama wa kisukari hauna dawa kabisa, leo gazeti la Mwananchi linatoa taarifa kua kuna mchungaji anatibu kisukari, ukimwi na magonjwa mengine sugu. Kinachishtusha sana ni kuona akili za waTanzania wengi namna gani zinaweza kukinaishwa maramoja.

Ugonjwa kama ukimwi kisukari nafikiri sio ugonjwa wa mtu kupewa kikombe kimoja cha dawa na kufika kwenye conclusion kua mtu ameshapona, tunaribu kua reasonable, hivi ni vitu vinahitaji muda kidogo ili kujua kua kweli dawa hiyo inatibu.

Upande mwingine ni ule wa mtu kudai kua ana mawasiliano na God hili nalo linahitaji kuangaliwa vizuri. Kinachoshtusha zaidi ni kusikia watu ambao tunawaamini kua ndio viongozi wa taifa letu kama wabunge mawaziri wanamiminika huko na mkuu wa mkoa anaiomba serikali ifacilatate mazingira ya watu kwenda. Hii ndio Tanzania yetu. Mungu ibariki dunia, Afrika na Tanzania
Is this material from the septic Tank?...
Lengo lako nini kuandika takamwili hizi?
Unashangaa mawaziri kwenda huko...my hairs!..Hivi kuumwa kuna uwaziri?
Kwanini usimshangae mkwere aliyekuwa wa kwanza kwenda?
 
Acha wenye Matatizo waende, Hata mimi ningekuwa Arusha ningekuwa mmoja wa Wamiminikaji
 
Ukishakuwa masikini upeo wa kufikiri unapungua. Hii issue nimeisikia lakini nionavyo mimi ni kwamba watanzania sasa tuko desparate! Unakuta taifa na wananchi wake hatuna mwelekeo.. and we think anything (hata kama ni super natural powers) zitamaliza matatizo yetu. Hivi hujawahi kujiuliza mtu anakwambia eti anaenda kwa mganga apate dawa ya kuwa tajiri? and people tena wasomi believe it! Unakuta kiongozi anakwenda kwa waganga kusudi ashinde uchaguzi...most of these things defeat logic! Well
 
Ni juzi tuu mkuu mmoja wa serikali alitangaza kua ugonjwa kama wa kisukari hauna dawa kabisa, leo gazeti la Mwananchi linatoa taarifa kua kuna mchungaji anatibu kisukari, ukimwi na magonjwa mengine sugu. Kinachishtusha sana ni kuona akili za waTanzania wengi namna gani zinaweza kukinaishwa maramoja.

Ugonjwa kama ukimwi kisukari nafikiri sio ugonjwa wa mtu kupewa kikombe kimoja cha dawa na kufika kwenye conclusion kua mtu ameshapona, tunaribu kua reasonable, hivi ni vitu vinahitaji muda kidogo ili kujua kua kweli dawa hiyo inatibu.

Upande mwingine ni ule wa mtu kudai kua ana mawasiliano na God hili nalo linahitaji kuangaliwa vizuri. Kinachoshtusha zaidi ni kusikia watu ambao tunawaamini kua ndio viongozi wa taifa letu kama wabunge mawaziri wanamiminika huko na mkuu wa mkoa anaiomba serikali ifacilatate mazingira ya watu kwenda. Hii ndio Tanzania yetu. Mungu ibariki dunia, Afrika na Tanzania

mkuu mimi nilianzisha sredi kuhusu hili lakin sijui iko wapi,viongozi wetu ni mazezeta.lakini hiyo title ya thread ni kali sani edit kidogo haswa hapo kwenye ukimwi iwe magonjwa sugu.
 
Is this material from the septic Tank?...
Lengo lako nini kuandika takamwili hizi?
Unashangaa mawaziri kwenda huko...my hairs!..Hivi kuumwa kuna uwaziri?
Kwanini usimshangae mkwere aliyekuwa wa kwanza kwenda?

Mkuu inaonekana umeshtuka sana uko njiani unakwenda? Kilichoshtusha sana ni the way of thinking ya watu wetu. Lengo langu hasa ni kuhimiza watu kuthink reasonable na ninashangaa mawaziri kwa kua ndio wasimamizi wa taifa sasa kama hivi ndivyo wanavyofikiri tunadhani kua kutapatikana ufumbuzi wa changamoto tulizonazo
 
Takamwili na wivu wa kijuaji ndo umepelekea uharishe ulichoharisha mkuu. Pole na acha watanganyika wapate tiba kwa bei nafuu kwani yale ma ARV yenu wananchi hawawezi afford diet yake, au wewe ni cheap labour kwenye mataasisi ya ukimwi una hofu na kazi yako?
 
Waacheni jamani wapone psychologically na phisyologically labda nchi itapona.:blah:
 
Unajua mi nipo Arusha Jiji la JENIVA YA AFRIKA,takribani wiki mbili habari ambazo haziishi hamu ni kuhusu Mbabu wa Loliondo na maajabu ya dawa.Nauliza ametokewa na mzimuu ama maajabu ya Munguu???Ee ndugu zangu JF tufike mahali tujiulize mbona kama babu anatibu kwa sh 500 iweje wafanyabiashara wa mabasi watoze 80,000 hadi 100,000 kwa nauli wakati masharti ya dawa sh500 je huoni hapo Wataenda matajiri tu ?Na ndiyo maana nauliza Mbabu wa Loliondo katokewa na mzimu ama Maajabu ya Munguu?Babu anapunjika na wafanyabiashara wananufaika wagonjwa walioletewa neema ya dawa wanateseka na wanatamani waka muone Babu ila wakijisachi nauli wanazidi kukonda na ugonjwa unazidi.Wale jamaa wanaosimamia nauli sijui SUMATRA hivi hawataki tukamuone babu ndo maana bado nauliza Mbabu wa Loliondo ametokewa na mzimu ama na maajabu ya Munguu?Jamani wale watakaobahatika kwenda kesho mkienda mwambieni babu ashushe maajabu nauli kwenda huko kwake iwe sawa na malipo ya dawa jamaniwengi tunataka tuje tupate dawa
 
sioni tatizo mtu kuamini katika kikombe kimoja cha dawa kuwa kinaponya na akatumia muda wake kutafuta tiba hiyo. Vitu vingi hufanikiwa kwa imani. Tusiwakatishe tamaa wanaotafuta ufumbuzi wa matatizo yao ya afya.
 
kuwa na akili na ufahamu mzuri ni kitu kizuri sana.......... yule mzee wala jajui watu wanafikaje pale...kikubwa kawaambia kuwa gharama ya dawa ni tsh.500 basi hayo mambo ya nauli sijui na nini ni mgonjwa mwenyewe na nduguze...

unamuonea mzee wa watu... hajakurupuka , na hata siku moja hajawaji kuto tangazo kuwa anatibu ila waliopona ndio wanasabaza taarifa na hivy watu kumiminika huko........
tangi mwaka 1991 june huyu mzee ameanza kuota ndoto .....hadi mwaka jana mwezi wa kuni akaanza kutibu......

tumia akili na utashi unapoweka thread humu
 
Kebehi sio poa . Mambo mengine ni beyond our imagination. Dont try this at home
 
muda si mrefu hapa moshi... mzee mmoja aliyekatwa mguu huko india kwa kusumbuliwa na sukari na mpaka kuwa anajipiga insulin ku control sukari na hata sukari kuanza ku affect macho yake...ameniambia amepona na tangu arudi ana siku nne hajui dawa wala insulin vipo wapi na macho yanapona .... mashuhuda ni wengi wengi waliopona .... JWTZ wameweka kambi zao za matent kuhudumia wanaotafuta tiba .. naambiwa pia red cross wapo njiani .... jana kulikuwa na watu zaidi ya elfu hamsini na magari 2000

ni kungonoka tu sasa kunywa bia kula sana nyama dawa zote c zpo.
 
"Jamii inayorudi na kuamini zaidi mambo ya imani kuliko mtizamo wa kitaalam ni jamii iliyokata tamaa" poor Tanzanians
 
Waambieni redcross wapeleke mahema. Mimi naenda kujenga danguro a.k.a guest house hapo jirani sasa hivi.

mi nadhan kuna muda wautani, chukulia wewe au mama yako au baba yako mngekua na tatizo hili ungecomment upuuzi kama huu kwel? Muda mwingine 2we 2najua nini 2nafanya.
 
Back
Top Bottom