Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Kuna kuwa na akili ... na kuelimika kiakili....
Lakini hiyo isisaidie chochote kwenye maswala yanayohitaji.. Hekima, nidhamu wala uwajibikaji..

Wasomi wengi hawana upeo kamili wa kihekima, nidhamu na hawajibiki kwa mioyoni mwao...

Serekali ni kipofu kwa maswala hayo ya kibinaadamu zaidi kuliko kiakili....

Akili na vyeo peke yake...si msingi wa uongozi ..bora

Swala la Loliondo linahitaji kupevuka kiutu zadi ya kiakili..

Lakini Utu wa serekali ..umelala...

CCM imelala ..iko kiakili tu..!! ubinaadamu na utu wa CCM na serekali yake...umezorota!!

Tusubiri janga juu ya janga...
 
Kuna nini kinachoendelea huko plz wadau tujuzeni sio wote tupo bongo!
 
Kuna nini kinachoendelea huko plz wadau tujuzeni sio wote tupo bongo!

Kuna mchungaji anadai ametokewa na mungu,anatibu magonjwa sugu km kansa,ukimwi na mengine. Sasa hivi tunavyoongea kuna watu kama elfu moja hivi wako pale wanasubili tiba.hakuna choo,hakuna huduma ya chakula,hakuna pa kulala.ni hatari tupu.
 
Huko Loliondo kuna maelfu ya watu, hakuna choo,maji,hotel, na magonjwa ya mlipuko yakitokea itakuwa janga la Taifa.

Kwa nini serikali ipo kimya ikasaidia kuweka utaratibu?

Msalaba mwekundu waende huko ili watoe huduma
Serikali iko likizo, haiwezi kutatua matatizo ya wananchi kwani hata marais waliotangulia walishindwa kuyamaliza. Mkuu ana pesa zinazotosha tu kutalii pande zote za dunia kwanza na kuwaombea misaada ili watu wasife njaa, labda pesa zikibaki ndo atafikiria kuwasaidia watu wa Loliondo.
 
Si kuna kamati ya MAAFA ya TAIFA, hilo jina tu wee utaelewa nini? hivi kwanini isingeitwa kamati ya kusaidia na kuokoa? ulishawahi kujiuliza swali kama hilo? haya utajiju
 
Hivi wewe unauliza serikali gani? Swala la kijamii sio swala la serikali..labda wasikie watu wameshakufa ndo utawasikia wakitoa tamko..wao wapo tayari kupambana na tatizo na sio kuzuia tatizo lisitokee! Wapo busy kujibu mashambulizi ya CDM

Penye highlight: Majibu gani wanmeshatoa? Wanachofanya ni kutishia tu.
 
we need a photo to see how does the place look like!!!!!!!!! can any 1 upload them?
 
Niko na mtu aliyetoka Loliondo sasa hivi, anasema kuna magari takriban mia saba na watu zaidi ya 5000. Kuna mabasi, malori, malandcruiser ya kukodi na private cars.

Hali si nzuri hata kidogo. Inakulazimu kusubiri siku 3-4 ili uweze kupata matibabu. maisha ni ghali sana na huduma za jamii ni mbaya sana. Loliondo is a very small town and its in the middle of nowhere. I cant get picture of the town with 5000 people!!!! I am sure the town has never hosted a delegation 100 people before, its an abandoned town.

What I can predict - is epidemic disease, uwizi na vifo.
Nafikiri kuna ulazima wa serikali kuangalia jinsi ya kuzibiti
 
Huko Loliondo kuna maelfu ya watu, hakuna choo,maji,hotel, na magonjwa ya mlipuko yakitokea itakuwa janga la Taifa.

Kwa nini serikali ipo kimya ikasaidia kuweka utaratibu?

Msalaba mwekundu waende huko ili watoe huduma

unajua unachosema??? naona umeweka vipande vya taarifa kwa vile hausomeki vizuri
 
ndugu yangu ana kansa ,kapelekwa huko leo, yaan nashindwa kuamini au kukataa ila namuombea apone tuu km kweli hiyo dawa inatibu
 
Unajua mi nipo Arusha Jiji la JENIVA YA AFRIKA,takribani wiki mbili habari ambazo haziishi hamu ni kuhusu Mbabu wa Loliondo na maajabu ya dawa.Nauliza ametokewa na mzimuu ama maajabu ya Munguu???Ee ndugu zangu JF tufike mahali tujiulize mbona kama babu anatibu kwa sh 500 iweje wafanyabiashara wa mabasi watoze 80,000 hadi 100,000 kwa nauli wakati masharti ya dawa sh500 je huoni hapo Wataenda matajiri tu ?Na ndiyo maana nauliza Mbabu wa Loliondo katokewa na mzimu ama Maajabu ya Munguu?Babu anapunjika na wafanyabiashara wananufaika wagonjwa walioletewa neema ya dawa wanateseka na wanatamani waka muone Babu ila wakijisachi nauli wanazidi kukonda na ugonjwa unazidi.Wale jamaa wanaosimamia nauli sijui SUMATRA hivi hawataki tukamuone babu ndo maana bado nauliza Mbabu wa Loliondo ametokewa na mzimu ama na maajabu ya Munguu?Jamani wale watakaobahatika kwenda kesho mkienda mwambieni babu ashushe maajabu nauli kwenda huko kwake iwe sawa na malipo ya dawa jamaniwengi tunataka tuje tupate dawa

Mbona ulichoandika na title haviendani??????????????
 
Hivi wewe unataka nauli ya kutoka Arusha hadi Loliondo iwe Tshs 500? Ukiweka gari mafuta hata ya Tshs 1000 haliwezi kukufikisha hata Burka kutoka mjini bila gari kuzimika.
Miujiza anafanya Babu na hajamlazimisha mtu kwenda huko ila kutokana na matatizo waliyonayo watu elfu 80 inaonekana ndogo kama watu wakiamua kuwachangia wenzao wagonjwa. Mbona harusi tunachangai mamillioni tushindwe kumchangia mtu elfu 80?

Pia kumbuka babu hana magari useme atafanya muujiza mafuta ya shilingi 500 yatoshe gari kutoka Ar hadi Loliondo.
 
Kuhusu huyo Askofu hakuna ubishi anatibu na watu wanapona. Mahita alipata dawa na alipopona akarudi na familia nzima. Mtoto wa Ndesamburu alitua kwa helicopter akiwa na mkuu wa mkoa wa Musoma. Magufuli alipata dawa huku akizuga amekwenda kukagua barabara. Kikwete alifika na mkewe akafuatia. Mufti mkuu ameshapata dawa na kama huamini hebu kajionee waislamu walivyo wengi kuliko wakristo. Wanaotoka huko wote wanakiri kupona bila kuzingatia imani zao. Babu hapokei zaidi ya sh.500 na hataki zawadi kama shukurani baada ya kupona. Amekataa gari na nyumba toka kwa muhindi na pia amekataa kuhamishiwa Dodoma na kudai Loliondo ni katikati ya dunia na kazi yake si kwa Tanzania tu bali dunia nzima. Kikubwa ni kwa serikali kusaidia kujenga vyoo kwani kuna hatari ya kilichopo kujaa. Pia chakula ni tabu kwani kuna hatari ya njaa kwani kuna uwezekano wa kusubiri dawa hadi siku nne na zaidi. Nina ndugu yangu amepona vidonda vya tumbo kabisa na kwa kumjaribu tumetia pilipili kibao ila sisi ndio tumeshindwa kula chakula.

NABII HAKUBALIKI KWAO.
 
Kuna taarifa kuwa mgonjwa mmoja mwenye asili ya ki-asia amepoteza maisha baada ya kuzidiwa kwenye foleni ya kusubiri tiba ya mchungaji wa loliondo.
Inasemekana viongozi wa kiserikali na matajiri wakubwa wanatumia nyadhifa zao 'kuchakachua' na kuwaacha walalahoi wakisubiri foleni.
USHAURI:Chonde chonde wagonjwa mnaoenda huko chukueni dawa zenu za kawaida kwani huduma inachelewa sana.
 
Kuhonga au kutafuna pombe ya laki 5 rahisiii, sasa hii 80 elfu ina ugumu gani km kweli unahitaji maisha. Hata nauli ingekuwa ya km ya ndege watu wangefurika tu.

Huyu babu angekuwa marekani na una shida ungeenda tu
 
Back
Top Bottom