Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Nimeikuta hii habari kule kwenye habari na hoja mchanganyiko.............

nakumbuka huko nyuma mch. rwakatale wa mikocheni B assemblies of God aliwahi kutumia mtindo wa kununua vitambaa (leso) vyeupe na kuviombea kisha anawapa watu ati wakivitumia kama kuviwekwa kwenye viipaji vya nyuso zao au za wagonjwa wao nyumbani, wanapona maradhi yanayowasumbua. shuhuda nyingi sana zilitolewa na ilifikia mahali kama mtu yumo ndani ya basi akielekea kanisani na akagundua kuwa kasahau kitambaa nyumbani huteremka na kurudi kukifuata, yaani kikawa sacred kupita kitambaa cha kawaida.

binafsi sikuwahi kuunga mkono tabia ya huyu mama kuombea vitambaa na kuvifanya kama hirizi, na kwa kweli sikuona msingi wa jambo hilo kitheolojia.


sasa tena ameibuka Mch. Mwasapile akidai kupata ndoto juu ya mti ambao unapochemshwa, kikombe kimoja tu cha maji yake kinatosha kutibu magonjwa sugu kama ukimwi, kisukari, kansa, pumu nk. hapa pia sioni msingi wa kitheolojia.

kwa mujibu wa BBC, mch. mwasapile alisema si maji yale yanayoponyesha bali ni maombi. sasa mi najiuliza iweje neema ya Mungu ya uponyaji ijifungamanishe na maji kiasi kile? tena kiasi cha kwamba bila hayo maji neema hiyo haifanyi kazi? mbaya zaidi wanasema kuna masharti kama: lazima akupe kwa mkono wake, huruhusiwi kunywa zaidi ya mara moja nk. hapa neema ya Mungu inaletwa kwa masharti!

binafsi nashindwa kuiita karama, uwezo wa Mungu hauna mipaka ya mahali wala wakati. hainiingii akilini kwamba mti huo ukichemshwa mahali pengine nje ya kiiji cha samunge, hauponyi na babu akikuombea bila kukupa kikombe chake kwa mkono wake huponi!

siwezi kutoa hukumu juu ya babu lakini naamini Mungu ni mkuu na muweza kuliko anavyoonekana kupitia hali ya huko loliondo. biblia inatuasa, tusimzimishe Roho, tusitweze unabii, tujaribu mambo yote tushike lililojema na tujitenge na ubaya wa kila namna (1 thesalonike 5:19-22)

naomba mnielewe kuwa sikejeli ndugu zetu wanaogua magonjwa mbalimbali sugu wanaopata faraja ya pekee huko samunge kwa babu, la hasha. haya ni mawazo yangu tu yaliyojikita kutazama jambo zima kitheolojia zaidi na sijatumwa na mtu yoyote. pia tusiwabeze wale wanaoonyesha kuhoji mantiki ya kanisa la KKKT kujipambanua pamoja na huduma hii ya babu.

HUKUMU NI ZAKE BWANA

mbarikiwe sana wapendwa

Glory to God
 
Ingefaa akina Muhogomchungu na Zubeda waendelee kukosa imani ili wenye imani wakapone,wasikute foleni kwanza,najua baadae watakuja kufumbuka na kukimbilia huko. Ubaya wa dawa kama hii ,hauponi kama hauna imani. Heko mchungaji,ushuhuda wa Mzee Ali
 
Je walijaribu kumpima huyu mgonjwa wa zamani kwa PCR (Polymerase Chain Reaction) kuona kama kweli hana virusi vya UKIMWI? Na je, alishawahi pimwa kabla kuona idadi ya virusi ili kudhihirisha kweli kwamba mwanzoni alikuwa na virusi kadhaa na sasa hana, maana kupanda kwa CD4+ cells sio issue ya kusema umepona, kwani hata wanaotumia hizi dawa za VVU pia CD4+ cells hupanda japo kwa rate tofauti kati ya mtu na mtu.

Na pia tunategemea mtu anayepata dawa za VVU ambaye vijidudu vyake havijatengeza usugu awe na undetectable viral load, ikiwa na maana ya kuwa japo virus wapo hasahasa katika cells zilizojificha ndani ya mwili katika maeneo kama vile ya ubongo n.k. lakini vifaa tulivyonazo kwa sasa vina limit ya kuona virusi, yaani wakiwa kidogo sana vifaa havitaona na hivyo vinasema huna kirusi.

Sipingi dawa hii, tatizo nina wasiwasi kama mchakacho wa kujua mtu huyu kama kweli amepona umefanyika vizuri. Na zaidi, je, ni kweli alikuwa na HIV? Isije ikawa hakupimwa sawa mwanzoni na akaanzishiwa dawa kimakosa.

Pia mashine huwa zina False Positives. Mungu atusaidie dawa ya mzee iwe inafanya kazi, maana naamini watu wengi wataacha kunywa dawa za hospitali na hivyo kutengeneza virusi sugu ambao kama mtu akimwambukiza mwingine tutakosa option za dawa.

kaka hii dawa si ya kisayansi, ushaambiwa na daktari mwenzako kwamba amepona sasa kipi ndugu yangu huelewi? kuna madaktari wenzako wa maabala waliipima hii dawa wakakuta ni sumu haifai kwa matumizi ya kiumbe chochote sasa hapo napo utasemaje?
hii dawa ni ya ki maajabu - madaktari wenzako sasa hivi wako fileni loliondo kama huna taarifa.
 
Tanzania sasa itajulikana ulimwengu mzima na Mungu lazima ana malengo yake kuifunua hiyo dawa hapa tanzania nchi masikini. Ni bahati iliyoje mtanzania kufunuliwa dawa inayotibu maradhi sugu pamoja na ukimwi!! Tumwache Mungu aitwe Mungu.

jamaa anapendekeza tuongeze gharama za VISA kwa wale wanaokuja kutibiwa toka nje, Mapato yanaweza kusaidia ujenzi wa miundobimbu huko loliondo.
 
Ubarikiwe kwa mtazamo huo. Hakuna upuuzi mkubwa na wa kihistoria tuliofanya watanzania kama kumrejesha kwenye madaraka makubwa ya nchi yetu mtu anayesema hajui kwa nini watu wake ni maskini na wakati huo huo anawaahidi maisha bora kwa kila mtu!!!!!

Kwa kweli ni upuuzi wa kihistoria, ukizingatia kwamba alikiri mwenyewe eti miaka miwili ya mwanzo ya utawala wake alikuwa akijifunza!!! Halafu bado akarudishwa madarakani!! Huwa ninajipa moyo kwa kusema at least mimi sio miongoni mwa waliompa kura yangu!
 
Kwa nini Mungu asiamuru kirusi cha Ukimwi kife duniani kote katika jina la Yesu?

Kwa nini Mungu anapenda kubembelezwa, na hela za dawa na sadaka analipwa?

Halafu Mr. Mungu ameshatawala miaka mingi mpaka anamkaribia Gaddafi, na matatizo ya health care system yake hayaishi, tumuondoe madarakani.

Pole sana; wewe na Jenerali Ulimwengu mna mawazo kama ya mwanambuzi ya kuamini kuwa mtu kazaliwa hapa Duniani na mwisho wake ni hapa hapa Duniani.Vitabu vya Hadithi vinawapoteza sana. Jenerali maisha si kuuza gazeti tu.
 
Kwa wanaoamini sioni sababu ya kutokwenda! kwa wanaosubiri agundue mzungu wasubiri as well!
 
Maswala ya kutumia chombo kimoja kwa kundi la watu ndiyo maisha ya watanzania karibu 75% waishio vijijini, 75% ya watanzania wanalala mahali ambapo hapatamaniki kwa karne ya sasa, maji yao si safi na salama, wengine bado wanajisaidia maporini kama loliondo. Barabara zetu nchini zinazounganisha mikoa yetu watu tunachimba dawa maporini tuwapo safarini kama loliondo tu. Hatuna umeme wa uhakika, tiba bado duni. Tatizo la BABU ni nini? Come out with utafiti wa kutosha. Mbona tunabwabwaja bila kuangalia hatari katika changamoto aliyoleta Mch.Ambilikile? Kubwa zaidi katoka KIIMANI, maana yake ni ibada tayari. Bila imani imekula kwako.
Simaanishi babu yuko sahihi lakini hatukujipanga tulipokuwa tunawasikia akina kakobe, lwakatare, lusekelo, she yahya, ndodi na sasa babu katu-challenge. Something must done to protect our nation.
 
I have read the General's Story from the beggining to the end. What i have discovered is that most Tanzanians write things by assumptions. THE WORD RESEARCH to us Tanzanians is quite ambiguous word. This is what is also facing mr Ulimwengu. ''What testimony is he looking for if thousands and thousands of people are scrambleling for KIKOMBE every day!!! I guese he need to conduct research in order to satisfy himselves. I believe in one way or another Mr Ulimwengu has a relative or neighbour saffering from one of the deseases mentioned by people and MEDIAs that they can be cured at BABUs place. I advice him there fore to take somebody to BABus home to get the MEDICs and there after wait to see the results.
NO RESEARCH NO RIGHT TO SPEAK OUT???
 
Kwa nini Mungu asiamuru kirusi cha Ukimwi kife duniani kote katika jina la Yesu?

Kwa nini Mungu anapenda kubembelezwa, na hela za dawa na sadaka analipwa?

Halafu Mr. Mungu ameshatawala miaka mingi mpaka anamkaribia Gaddafi, na matatizo ya health care system yake hayaishi, tumuondoe madarakani.

.
Isaya 14:13-16 and Ezekiel 28:13-19.
.
 
Jenerali shukuru kwa kupata habari iliyokuwezesha kuuza gazeti.

Kama dawa inaponyesha au haiponyeshi hilo wewe halikuhusu.

Wangapi waliokuwa mahospitalini miaka nenda rudi na hawajapona? kuna ubaya gani wakienda Loliondo?

Angegundua mzungu Jeneráli asingeongea haya ila kwa vile ni Babu Mwasapile basi imekuwa nongwa.

Direct attack with weak reasons and evidence.
 
Kwa nini Mungu asiamuru kirusi cha Ukimwi kife duniani kote katika jina la Yesu?

Kwa nini Mungu anapenda kubembelezwa, na hela za dawa na sadaka analipwa?

Halafu Mr. Mungu ameshatawala miaka mingi mpaka anamkaribia Gaddafi, na matatizo ya health care system yake hayaishi, tumuondoe madarakani.

God of where? wa Yelusalem au Loliondo or Africa? God has no chase a power! Ulimwengu anaweza kuwa sahihi. Tusubili tuone.
 
Kama vile baadhi yenu hamtaki kuamini lakini pia tusibishe kama hatukuwa wagonjwa tukaenda kutibiwa halafu hatukupona. Usiseme ni uongo kama hujajaribu ikashindikana.
Ikiwa unataka kuthibitisha basi nenda kaone mwenyewe ndipo uwe na haki ya kupinga. Ni kichekesho kulinganisha hii na DECI, ni vitu viwili tofauti, usiseme eti tufanye uchunguzi wa maabara maana yeye mwenyewe anakiri kwamba hajui nini kilichomo humo, hii ni mchanganyiko wa mti na imani, sasa sijui content ya imani katika dawa hiyo itapimwaje.
Inachekesha pia, kwamba tunataka watu wasiende lakini waliokwenda wanasema wamepona, nadhani kila anaeugua atataka kwenda kutibiwa, ikishindikana angalau hatakuwa amekosa nafasi. Kama watu walikuwa hospitalini kwa miezi kadha, wakatoroka wakaenda huko wakarudi wamepona, halafu wewe unamwambia mwongo, atakucheka tu kwa vile yeye anajua alivyokuwa na alivo baada ya kwenda huko.
TUNAOTAKA KUBISHA NA KUSHAMBULIA TUKACHUNGUZE KARIBU PALE, kama ni uwongo tutauona, kama ni kweli tutaona, na kama ada ni sh 500 tu, tena mwenyewe wala haishiki yeye!!!!
Waliosema wajengewe vyoo sio yeye ni watu wanaoangalia kwa nje, kama amekataza hata wenye usafiri wasichaji nauli kubwa, iweje kama anataka pesa, ISIWE TUNATAKA KUBISHA TU KILA KITU HATA BILA KUJARIBU



namuunga mkono Jenerari,huo upuuzi wa mganga wa loliondo ni sawa na DECI,watu tuliwaambia hapo nyuma DECI ni utapeli watu hawakusikia,inashangaza sana tena sana katika hizi zama za maendeleo watu wazima na akili zao wanadanganyika eti na miujiza ya dawa ya Loliondo,na kwa ujinga huo hata serikali nayo imeingia mkenge wa kumruhusu huyo mzee tapeli eti aendeleze tiba,jamani si hapo nyuma serikali ilipiga marufuku hayo mambo ya waganga wa kienyeji.Jamani msiwe wajinga hakuna dawa inyotibu ukimwi au kisukari hivi sasa ,dawa ni kufuata masharti.
 
Prove ni utapeli, usiseme tu juu juu. Kama vile kusema anaponyesha inataka proof, hata kubisha haponyeshi inataka proof pia.

Namuunga Mkono Ulimwengu 100% .. Kisukari na magonjwa mengine yanatibika na herbs za kawaida pia.. hapo babu si mpingi lakini linapokuja swala zima la HI5 "HIV" .. ni utapeli "nukta"
 
Babu mwenyewe hajasema chochote kuhusu kuijaribu dawa yake maabara, ni watu wa wizara ya afya ndio walisema SIO BABU, tunazusha mengi mno, kwani mtu akienda kuichukua akaondoka nayo akaipime ana nini??


Pamoja na heshima zote nilizonazo kwa Ulimwengu, nachelea kusema haya ni maswali mepesi kuulizwa naye.Majibu ni kama ifuatavyo

1.Amekataa isiwe tested katika lab sababu hiyo siyo scientific medicine...nadhani unajua huwezi kuprove that God ana-exist in the lab
2.Hata kama dawa yake inatibu Ukimwi au Diabates ambayo ni magonjwa makubwa, siyo sahihi kusema basi watu wasichukue tahadhari ya kupata magonjwa mengine kama kipindupindu.....ni sawa sawa kama wewe uwe na dawa ya Malaria ndani basi ulale tu bila chandarua au bila kuchukua tahadhari yeyote ya kuumwa Malaria sababu dawa ipo

In general, kwa sababu ulizotumia nashindwa kuungana nawe katika doubts zako...
 
God of where? wa Yelusalem au Loliondo or Africa? God has no chase a power! Ulimwengu anaweza kuwa sahihi. Tusubili tuone.

.
Hivi yule wa Yerusalemu sii ndie huyu wa Africa eeeh?
Ukitaka kuwasiliana na huyu wa Yerusalemu inakulazimu kwenda hija huko huko au;
.
 
Kwa mara ya kwanza Jenerali kaanguka.

Anawakebehi watu walokata tamaa na maisha kwa matatizo mbalimbali yaliyosababishwa na mfumo ambao yeye pia alishiriki kuujenga. Kwa nini asiuchambue mfumo uliopo? Poor jenereali, kashindwa kabisa kuanalyze chanzo cha tatizo na uhusiano na mfumo wa kitawala uliopo. Wanamchambua Babu wa watu badala ya mfumo. Jenerali that is too low of you!

Besides sijui kama amewahi kuugua na/au kuuguza mtu aliyelala kitandani miaka 7 au 8, aliyezunguka na kula makemikali ya maabara (ambayo Ulimwengu anayaita ya kisayansi) bila matumaini ya kupona. Sometimes Ulimwengu usiandike tu for the sake of it.
 
Back
Top Bottom