Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Kwa babu unaambiwa imani yako ndio itakayokuponya sio mambo ya utafiti kwani imani inautafiti jamani? kama ww huamini haina haja ya kwenda kwa sababu ata ukienda kunywa haikuponyi.

Imani sawa. Wenye imani waliopona wako wapi. Imani haipimwi lakini kupona kansa au ukimwi kunapimwa. Mtu anaweza kuhisi kwamba amepona kwa imani lakini vipimo vikaonyesha kwamba kweli amepona ama la. Watupe ushahidi jamani siyo mtu akiulizwa anasema imani. Imani siwe kichaka
 
ni ngumu,watajitokeza wa kisukari, BP na kansa usitegemee kumsikia wa ngoma hapa!mpaka sasa hayo matatu yashatibika ndo maana halmashauri nyingi e.g misungwi,umwagiliaji kanda tabora,bunda,na........... angalau wameshapeleka watumishi wao huko kupata kikombe kwa magari yenye namba zinazoanza na SM....
 
Na sielewi hao waliokuwa wanatumia ARV kama Babu anawaruhusu kuja kuendelea na dozi zao au anawazuia? Hii mbona itakuwa hatari jamani!!!!

kuloloma na kulalama sio ufumbuzi! Taasisi zinazoshughurikia mambo ya afya zipo na wafanyakazi wake ni kati ya wale waliopata kikombe cha babu, kama dawa hiyo isingekuwa inaponya nafikiri "SIRI-KALI" ingalipiga stop. Halafu swala la kupona wote si kweli, maana hata huko kuhospitalo wengine hufia huko na hakuna kesi, iweje kwa Dr Babu anayekutibia kwa kutumia imani yako?
 
Hakuna ushahidi wowote tangible unapatikana sijui kwa nn! Kila m2 anasema, nimesikia lile na lile, hakuna anayejitokeza km muhusika kusema alikuwa na shida gani na kikombe kimemsaidiaje! Ushahidi ni muhimu sana!
 

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Tanzania Kadinali Pengo

Kiongozi mmoja wa kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam jana alielezea msimamo wa kanisa Katoliki kuhusu tiba ya Loliondo inayotolewa na Mchungaji Ambikile Mwaisapile kuwa kabla mtu yeyote hajapata tiba hiyo lazima ajiulize maswali manne kwanza kabla ya kuamua kuitumia.

Akihutubia katika Ibada ya Jumapili katika Kigango cha Mt. Yohane wa Msalaba Parokoa ya Mbezi Luis, Paroko wa parikoa hiyo Padre Vivian alisema, "Sina chuki wala tatizo lolote na tiba ya Loliondo, lakini kama unataka kwenda lazima ujiulize maswali manne yafuatayo.

"Kwanza, tiba inayotokana na miujiza ya Mungu lazima iwe endelevu isiwepo kwa kipindi kifupi tu," alisema.

Swali la pili alilotaka watu wajiulize ni kuwa tiba inayokuja kama muujiza kutoka kwa Mungu huwa na masharti? Swali la tatu alilolitaja Paroko huyo ambaye ni Padre wa Shirika la Wakalmeli ni kuwa, Kama tiba hiyo inafanya kazi ndani ya Loliondo, kwanini isifanyekazi Dar es Salaam na kwingineko?

Na swali lake la mwisho alilotaka watu wajiulize kuhusu tiba hiyo ya magonjwa sugu ukiwemo UKIMWI ni je, Mungu aliwaumba wanadamu na kisha kuamua kuwaangamiza? Au wanadamu wanaangamia kutokana na vitendo vyao vya ujanja ujanja?

"Ukiisha jiuliza maswali hayo na kujiridhisha kwa majibu utakayopata unawea kufanya maamuzi ya kwenda Loliondo. Hivyo ukiliona basi limeegeshwa katika stendi ya Mbezi au mahali pengine na ukasikia wapigadebe wanaita Loliondo Loliondo Loliondo, basi panda ukapate kikombe cha Babu," aliongeza kusema.

Katika siku za hivi karibuni Mchungaji Mwaisapile ameutikisa Ulimwengu baada ya kutangaza kuwa anatibu magonjwa sugu kwa kutoa dozi ya kikombe kimoja cha dawa ya kienyeji kwa gharama ya shilingi 500/ kwa Watanzania na Tsh 1,000/= kwa wageni.

Viongozi mbalimbali wa siasa na dini wakiwemo maaskofu wa madhehebu ya Kikristo wamekuwa wakitoa ushuhuda wa ukweli wa tiba hiyo na kuwashauri wananchi wenye magonjwa sugu kwenda kijijini Samonge mkoani Arusha kupata tiba.

Hata hivyo kwa upande mwingine, baadhi ya viongozi wa makanisa hayo akiwemo Askofu Zakaria Kakobe wa kanisa la FGBF na Mchungaji Christopher Mtikila wamekuwa wakiipinga vikali tiba hiyo.

Source: mbs
 
Je samwel aliitwa mara ngapi ili apewe masharti ya kwenda kueneza neno la Mungu?

Je Musa wakati anapokea amri za Mungu akupewa masharti?

Kwa nini Yesu aliambiwa akapalizwe uwinguni kupitia milima ya Oliva na si kwingneko?

Je, Yesu si alishawai kusimamia sadaka mpaka akamsifia mjane aliyetoa kidogo?

Je Yesu alisemaje kwa anayetaka kumfuata?si sharti abebe msalaba wake? Si sharti?

Hamna kitu chochote duniani kisicho na sharti! Hapa kucheka sharti uoneshe kuhusika na jambo fulani,kuendesha gari sharti uliwashe! Kula sharti umeze! Au mpaka kila kitu kitajiwe sharti ndo ufurahi? Anasema wajiulize kama Mungu anaponesha kwa msimu,je kwani baba kashaacha kutibu?

Acheni wivu, Babu kafunuliwa! Kwa ili fanyeni siasa ila hapa siambiliki japo mi na dini ya babu tofauti!
 
Ila bwana ulimwengu una kingeledha kigumu! mbona hata wadhungu wenye lugha yao wakiandika makala hawaweki mavocabulari kama yako? Lengo ni watu wote hata wenye kujua cha kuibia kama sisi tuelewe au ni nini? Anywei nimedonoa kama kuku......
hahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaahahaaaaaaaaaaaaaa
 
Hivi mpaka sasa ni watu wangapi waliopoteza maisha wakienda kurekebisha afya kwa babu? Hii ni pamoja na wale waliopoteza maisha hapo hapo nyumbani na baada ya kubwia hicho kikombe. Nani anajua atusaidie?
 
Watu wamepona mi jirani yangu amepona kabisa ehhe ushahidi gani mnautaka
 
Je samwel aliitwa mara ngapi ili apewe masharti ya kwenda kueneza neno la Mungu?

Je Musa wakati anapokea amri za Mungu akupewa masharti?

Kwa nini Yesu aliambiwa akapalizwe uwinguni kupitia milima ya Oliva na si kwingneko?

Je, Yesu si alishawai kusimamia sadaka mpaka akamsifia mjane aliyetoa kidogo?

Je Yesu alisemaje kwa anayetaka kumfuata?si sharti abebe msalaba wake? Si sharti?

Hamna kitu chochote duniani kisicho na sharti! Hapa kucheka sharti uoneshe kuhusika na jambo fulani,kuendesha gari sharti uliwashe! Kula sharti umeze! Au mpaka kila kitu kitajiwe sharti ndo ufurahi? Anasema wajiulize kama Mungu anaponesha kwa msimu,je kwani baba kashaacha kutibu?

Acheni wivu, Babu kafunuliwa! Kwa ili fanyeni siasa ila hapa siambiliki japo mi na dini ya babu tofauti!

Ama kweli watu wanaangamia kwa kukosa maarifa. This is nonsense.
 
ata Yesu alitoa mifano ya mafumbo.Fumbo mfimbie mwelevu atalifumbua lakini kwa mjini ni kitendawili .
 
Hivi kweli dawa ya Babu haina sharti? Mbona nilipata kuona akinukuliwa ya kwamba dawa yake inaponya wale tu wenye imani. Kauli kama hiyo aliitumia Yesu Kristo mara kwa mara kwa kusema kwa wale aliokuwa akiwatibu; "imani yako imekuponya"
 
Padre katoa msimamo au mahubiri yake. Huo sio msimamo wa kanisa. Bosi wake alisema yeye amebaki midomo wazi maana hawezi kuelezea kinachotokea , unless padiri huyu ni type ya Kakobe
 
Hayo maswali inatakiwa ujiulize kama hausumbuliwi na ugonjwa wowote!! lakini kama wewe ni mgonjwa, huitaju kujiuliza.. KWEA BASI nenda Loliondo kwa babu!!
 
Baba padri usiwe moga kwa kumung'unya maneno eleza wazi kwamba M Nimdhambi sio unachotufundisha kwamba acheni dhambi!
Mungu alisema; "....Nitainua hata mawe yanitumikie..."!
 
babu wa loliondo amekuwa akisema dawa anayotoa anaiombea na Mungu huweka neno lake ndani ya dawa-Sasa jiulize neno la Mungu ni nani kama sio Yesu?
 
padre ana hoja ya msingi. wakristo hawpaswi kushabikia jambo na kilikimbilia kama majuha. padre amewapa vipendele vya kuzingatia kama checklist kabla hawajakurupuka kukimbilia loliondo. najua watampuuza na wameishampuuza sana huyo padre lakini yeye katimiza wajibu wake. Mungu ambariki sana

tatizo watu wameishalewa na mrigariga hawataki tena kusikia maneno ya Mungu yanasemaje!

ooh Lord have mercy on your people. amen

Glory to God
 
Viongozi wengi wa dini ni waoga inapokuja mwenzao kuwa na nguvu fulani zaidi yao. LUSEKELO, KAKOBE ,MWINGIRA. Hii hupelekea kupingana na mungu na kunyima faida kwa waumiini wao.

Kanisa katoliki pamoja na kuwa na mitazamo yenye misimamo imara limefanya makosa mengi ikiwemo la wanamaombi wa Padre Nkwera ambae kazi zake zinatambulika hata Roma hadi leo kanisa hilo bila sababu linawapinga. Kanisa likumbuke Yesu aliwajibu wanafunzi wake 'asie kinyume chetu yu pamoja nasi'. Kwa vile hawana uhakika wanyamaze wasitoe matamko ya kibinafsi.
 
Ni mawazo yake tu,sio kauli ya kanisa,,wasiomini waache,wanaoamini wanywe kikombe as alternative medicine na dawa zao za hospital wanywe wakati wakifuatilia checkups..ni hali halisi.
Hakuna udini hapo
 
Hapa kuna tafsiri ya aya hizo kutoka kwa Robert Stapleton;
Aya ya 1
1. Mto wa maji ya uzima. (Angalia Yoh. 4:5-14, 7:37-39 katika hili, Yohana ametumia mfano huu kuongelea njia ambazo watazipita watoto wa Mungu. Nyuma katika ufunuo 7:16,17 tuliona “chemichemi ya maji ya uzima” ambayo imetumika kuelezea ulinzi wa waumini au wanamwamini Bwana. Hapa inasisitiza baraka zote ikihusisha na ulinzi.)

2. Yenye kung’aa kama bilauri.(Inaonyesha usafi.)
3. Ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu.(Inaonekana kwangu kwamba hii inaonyesha baraka za kiroho ambazo zinatoka kwa Munguambazo ziko katika kanisa - Efe. 1:3.)

4. Na cha mwana - Kondoo.(Hii inaonyesha mamlaka ambayo Yesu anayo (Mat. 28:18-20) kwa hiyo hamna nyingine hjii itakkuwa ndio siku ya mwisho, I Kor. 15:24-26.)

Aya 2
1. Katikati ya njia yake kuu.(Tuliongelea kuhusu njia katika Ufu. 21:21 Ikisisitiza uzuri wa Kanisa)


2. Upande huu na upande huu wa kanisa.(Zingatia Yohana kuona miti mingi lakini wa uzima ulikuwa katika pande zote za mto).

3. Mti wa uzima (Huu mti ni alama ya habari njema yua wokovu ambayo inaendelea kuenea)

4. Uzaao matunda kwa wakati wake (Kuenea kwa injili pamoja na baraka zilitolewa kwa wototo wa Mungu . Inasisitiza kuwa hakuna kipindi maalumu cha kutokuwepo mavuno katika kueneza injili)
.
5. Na majaniya mti huo ni wa kuponya mataifa (Ndiyo, maana nafikiri hii yanaelekezwa mbinguni. . Kumbuka tulivyosema kuhusu mataifa katika Ufu. 21:24. Kama hii ni mbinguni sasa mataifa inatoka wapi Kumbuka kwamba neno la mataifa linamaanisha watu wa ulimwengu badala ya watu wa Mungu. b. Hivyo, imekuwaje, mataifa (watu wa ulimwengu) waende kuponywa baada ya hukumu?
Labda nafasi watapata nafasi nyingine baada ya miaka elfu moja au miaka miwili. Kuna nafasi moja ambapo tunaweza kuweka mataifa, ambapo wanaponywa ni wakati wa
mfumo wa Kanisa kabla ya hukumu. Au labda kila usiku Mungu atatoa mwaliko kwa watu waliopo Jehanamu ili waweze kutubu. Lakini sasa, vipi kuhusu wayahudi 9:27 na hukumu yao. Tunachokiangalia ni uhitaji wa mataifa wa kuponywa na nguvu za Kanisa katika kueneza injili ili kuwatibu. Tunaongelea kuhusu kuponywa kiroho.
 
Back
Top Bottom