Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

watu waendelee kupata kikombe, UDSM,NIMRI na wizara ya afya wamethibitsha uhalisia wa dawa kwa wale wanaotamani ilete madhara kama mediaman na wengieo sijui watasemaje tena?????? Tuwaache wenye imani wakanywe dawa.
 
Naangalia Tbc1 serikali imethibitisha kuwa Dawa ya Babu Loliondo haina madhara lakn wanachokifanya ni kuja kuthibitisha kama kwel inaponya au la magonjwa yalitajwa kuwa inaponya.

Source: Tbc1 habari saa 7 mchana
 
habari njema. ni hatua moja muhimu ya kwanza. kuwa walioitumia hawaqna madhara ya kibinadamu.
 
Sawa haina madhara je inatibu kweli au inatibu kwa imani?

Mkuu kulithibitisha hilo bado. Tungepata m2 humu jamvini ambae ametumia na kuthibitisha kupona ingekuwa vizuri zaidi. Tatizo suala hili tumekuwa tunalizungumzia sana na uthibitisho hatujapata. Mimi pia ninashauku kubwa ya kupata huo uthibitisho wa kuponyesha au la.
 
Hivi kweli serikali haioni madhara ya kumuendekeza huyu babu wa KKKT(Kunywa Kikombe Kimoja Tu). Tunaambiwa wanakufa watu sio chini ya watano kwa siku.
 
Angalau sasa serikali inaanza kufanya wajibu wake. Hili lilikuwa la muhimu sana kufanywa na serikali.
 
Swali lilikua ni kutibu au kutokutibu hizi nyingine ni porojo tu!kwa hiyo nikinywa ndoo nzima ya dawa ya babu sitakufa.where in the world dawa ikawa haina side effects?huu ni upupu!
 
Hivi kweli serikali haioni madhara ya kumuendekeza huyu babu wa KKKT(Kunywa Kikombe Kimoja Tu). Tunaambiwa wanakufa watu sio chini ya watano kwa siku.

umeambiwa wanakufa baada ya kunywa dawa? na kama wanakufa baada ya kunywa dawa,unajuaje siku zao zilikuwa zimefika au walikiuka masharti?manake babu anasema watu wasikatize matibabu hadi wathibitike mtu anakunywa anaacha kunywa dawa alizokuwa anatumia kabla!!!! kwa taarifa zinazotangazwa na vyombo vya habari wengi wanakufa hawajamfikia babu!!! bora wamethibitisha manake kuna watu walipata la kusema na kuhoji imani za wenzao.:juggle:
 
WC yaelekea una chuki binafsi na Mchungaji, vifo ya watu huko Loliondo hayatokani na madhara ya kikombe anachotoa Babu huyo bali ni kukosa huduma hiyo ya matibabu kwa muda muafak kutokana na wagonjwa hao kuzidiwa
 
watu waendelee kupata kikombe, UDSM,NIMRI na wizara ya afya wamethibitsha uhalisia wa dawa kwa wale wanaotamani ilete madhara kama mediaman na wengieo sijui watasemaje tena?????? Tuwaache wenye imani wakanywe dawa.

Tumsubiri Kakobe tusikie atasema nini tena maana inaonekana anamuombea mabaya babu wa watu na alikuwa anasubiri ripoti hii kwa hamu akitegemea itakuwa na mapungufu afurahie.
 
Hivi kweli serikali haioni madhara ya kumuendekeza huyu babu wa KKKT(Kunywa Kikombe Kimoja Tu). Tunaambiwa wanakufa watu sio chini ya watano kwa siku.

Hivi babu alisema dawa inazuia mpaka kifo!
Mbona hata hsptl wanakufa. Kumlaumu babu sioni kuwa na tija coz kifo kikikufika hakina kizuizi.
 
umeambiwa wanakufa baada ya kunywa dawa? na kama wanakufa baada ya kunywa dawa,unajuaje siku zao zilikuwa zimefika au walikiuka masharti?manake babu anasema watu wasikatize matibabu hadi wathibitike mtu anakunywa anaacha kunywa dawa alizokuwa anatumia kabla!!!! kwa taarifa zinazotangazwa na vyombo vya habari wengi wanakufa hawajamfikia babu!!! bora wamethibitisha manake kuna watu walipata la kusema na kuhoji imani za wenzao.:juggle:

hawajathibitisha kama ni dawa!
 
Nasikia halmashauri imepata mradi mpya, kila gari inayopita inachajiwa,
mie nilidhani ni kwa ajili ya ujenzi wamiundombinu, lakini kumbe hapana,
watu bado wanapata shida sana kufika, matokeo yake ambao hawajui kiwango cha ugonjwa wao wanajikuta wanazidiwa, wanafariki kabla ya kufika, hili ni jambo baya sana.
Ambulance iliowekwa pale inatumika kwa kazi gani??
nasikia ambulance inabeba 'wateule' wachache wasiopenda kupanga foleni, baada ya kuongea na wakuu wa pale, wanafika mara moja kwa babu na kupata kikombe, wakati waliozidiwa wanapitwa nayo kama upepo na wanafariki, na kuhesabiwa tu kama namba ya maiti.
Utata nipale unapokuwa umesafiri peke yako bila ndugu, unapofariki, inabidi gari ulio nayo, watu wasiokujua, wakuweke pembeni kwanza, wakapate kikombe, au basi ligeuze na wote wakose kikombe?
 
Hivi kweli serikali haioni madhara ya kumuendekeza huyu babu wa KKKT(Kunywa Kikombe Kimoja Tu). Tunaambiwa wanakufa watu sio chini ya watano kwa siku.

serikali dhalimu inateketeza watu wake.kuna miradi ya watu pale fikiria-hoteli za arusha,cruzer,ushuru wa halmashauri,perdiem za watafiti,diversion ya dowans na hali mbaya ya uchumi.
 
Mkuu kulithibitisha hilo bado. Tungepata m2 humu jamvini ambae ametumia na kuthibitisha kupona ingekuwa vizuri zaidi. Tatizo suala hili tumekuwa tunalizungumzia sana na uthibitisho hatujapata. Mimi pia ninashauku kubwa ya kupata huo uthibitisho wa kuponyesha au la.
hii dawa nami naiamini kwa kiasi fulani lakini hili suala la ushahidi linaleta utata. Ofisini kwetu kuna mtu ana sukari/hiv lakini tangia arejee kutoka Loliondo ni zaidi ya majuma mawili lakini hatwambii lolote!
 
Swali lilikua ni kutibu au kutokutibu hizi nyingine ni porojo tu!kwa hiyo nikinywa ndoo nzima ya dawa ya babu sitakufa.where in the world dawa ikawa haina side effects?huu ni upupu!

Kwa kuanzia hili la mdhara ndio la muhimu zaidi na kwa kweli wamechelewa kuifanyia kazi na kutoa matokeo. I just cant imagine kama wangesema ina madhara....ukizingatia maelfu waliokwisha kunywa pamoja na viongozi kadhaa! Ni kweli kila dawa ina side effects lakini ni kwa kiwango gani cha madhara ukilinganisha na faida yake kwa mtumiaji.
 
umeambiwa wanakufa baada ya kunywa dawa? na kama wanakufa baada ya kunywa dawa,unajuaje siku zao zilikuwa zimefika au walikiuka masharti?manake babu anasema watu wasikatize matibabu hadi wathibitike mtu anakunywa anaacha kunywa dawa alizokuwa anatumia kabla!!!! kwa taarifa zinazotangazwa na vyombo vya habari wengi wanakufa hawajamfikia babu!!! bora wamethibitisha manake kuna watu walipata la kusema na kuhoji imani za wenzao.:juggle:
Serikali yetu ingebaki bila DINI wala IMANI yoyote hata kwa suala kama hili. Badala yake VIONGOZI wetu kwa kuwa wao wanaweza kumfikia kigagula huyu wanamtangaza kwelikweli. Wanasababisha msongamano wa ajabu wa watu wetu.
 
Back
Top Bottom