Juzi nilitupia kijiuzi, kuhusu wanaume kugongewa wake zetu,na mwisho kabisa nikatoa maoni yangu ya nini kifanyike ili mradi tuepukane na kadhia hii inayowatafuna wanaume wengi,kwamba ni kukataa ndoa kwa hisia na uchungu sana.
Japo kuna watu walinisimanga kwa namna moja au nyingine,ila msimamo wangu ni ule ule.
Sasa leo nitaeleza kwa nini hasa niliona kuwa hilo ni suluhisho sahihi kabisa.
Miaka kama 6 hivi nilikuwa na demu mmoja ambaye kiukweli tulipendana sana tuu,alitambulika kwetu,nikajulikana kwao.
Mi kiasili ni mkimya sana na huwa sina mambo mengi,hata mtaani sikuwahi kuonekana na mademu,kwa kifupi sijawahi kuwa skendo za mademu mtaani.
Ila kwa nguvu ya mapenzi,yule demu alijulikana vizuri tu mtaani kuwa ni bebe yangu,japo hakuwa anatokea pale mtaani,yeye alikuwa anaishi zenji,mi nilikuwa mkoani.
Kuonana kwetu kulikuwa ni mpaka nipate likizo ya chuo,au yeye apate likizo ya kazi.
Kufupisha story, mahusiano yalidumu kwa muda wa miaka 5,tuliachana kwa amani kabisa kwa sababu ya tofauti za kidini, yeye hakuwa radhi kuhamia kwangu,mimi pia vile vile.
Sikuwahi kuwa karibu naye tena, baada ya kuachana kwetu, sababu naamini x ni x tu hupaswi kumuweka karibu hata dk 1, hata kama mliachana kwa amani.
Nilikuja kupata taarifa mwaka juzi kwa ndugu yake mmoja ambaye ni mshkaji wangu kuwa anaolewa,na ana mtoto tayari,muda huo nmeshamsahau kabisa.
Mwaka jana mwezi julai, nikiwa Dar, alienda home kwa mama,akiwa na mtoto wake kuniulizia,akaambiwa nimehamia dar muda mrefu, akapewa namba zangu ndo akaanza kunitafuta.
Mwaka jana huo huo,hatimaye aliolewa na kabla ya ndoa yake,nakumbuka siku moja nimetoka TRA,kulipia madeni ya kiusafiri changu kilidakwa, nikiwa njiani nakuta namba ngeni,kupokea naskia ananiita jina ambalo alikuwa anapenda kuniita tangu enzi hizo"SIR CHIEF"niliwahi kuhoji kwanini ananiita hivyo akanambia ananifananisha na jamaa moja mkorea sjui kwenye drama zao watoto wa kike.
Jina hilo alikuwa ananiita yeye peke ake dunia nzima,so endapo mtu akiniita hilo jina tu bila hata ya kumuona, akili yangu ingejua tu alikuwa ni yeye.
Hakutakiwa hata kujitambulisha,tukasalimiana pale akaniuliza mwezi december utakuepo home,nikamjibu hapana ntakuwa nimerudi dar,(december nilirudi home mkoani).
Akanambia naomba uwepo cos natarajia kuja huko kwa ajili ya kitchen party,nikamuahidi ntajitahidi,ila sikuweza kuendelea kubaki mkoani mpaka mwezi uishe so nkarudi zangu kwenye majukumu mengine dar.
Mwezi wa pili,ndipo alipoolewa ila hakuwahi kunitafuta baada ya kitchen party na sikuwahi kutaka kujieleza why skuhudhuria cos nazingatia mipaka kati yangu na x.
Juzi kati nipo nyumbani,tena chumbani nimekaa natazama mechi,demu angu amelala naskia simu yangu inaita,kupokea naskia tena "sir chief" nikamsalimia pale kama kawaida akawa anahoji vitu vya kawaida tu kama unaendeleaje,unafanya kazi gani,japo hilo sikumjibu.
akaniuliza "umeoa"?,nikamjibu "hapana ningeoa mbona ungejua tu,cos tupo wote kwenye group la form four leavers?"akasema kule alijitoa tangu kitambo,skumuhoji sababu za kujitoa.
akanambia utakuja lini zenji kumpa hi,uncle wako??nikasema sina biashara ya kunileta huko,(nilimdanganya,cos siku kuu ya idd nimepanga na mwanangu mmoja twende zetu zenji na bebe zetu).
Nikatoka nje,baada ya kuona nampigia kelele bibie aliyelala kwa raha zake,nikaenda choo cha public,huku bado naongea naye, nikamskia anaongea na mtoto wake,nikamwambia awasalimu wote kwao tukaishia hapo.
Nikarudi chumbani demu anawaka huyo aliyepiga simu ni nani,na kwanini ukaongelee nje,na kwanini kauliza kama umeoa,? Nikahoji umejuaje kama kauliza nimeoa,akasema nilikuwa naskia kila kitu,.(wakuu nilidata,kuweni makini na wanawake unaweza sema amelala kumbe anaskia kila kitu unachoongea hawa watu kwa kuigiza aseeee [emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]).
Nikajitetea pale na kumwambia ukweli ila hakuonekana kuniamini,yeye alisimamia kauli yake kiwa aliyepiga simu ni x wangu mmoja kwa jina la neema,ambaye yeye ndo anafahamu na aliwahi kuleta noma sana mpaka mtaani ikawa soo. (neema popote ulipo ujikwake ulimi panya wee [emoji38]).
Wakuu jana ananitafuta anasema,kanimiss nanukuu,"sir chief unakumbuka kipindi kile ukiwa zenji,nimemiss sana zile moments unaweza kuja hata one wikiend?".
Nikamjibu,siwezi kuja zanzibar bila sababu ya muhimu,nikipata nitakuja .
Nahitimisha kwa kuhoji je,mkeo ulimkuta bikira,?je hana x?vipi kama mimi ningekuwa mtu wa kutake advantage kwenye hili suala,si ningeleta ufisi kwa mke wa mtu nikaenda kumrukia rukia,Niliwaambia wake zenu wakishapata mtoto tu nini huwa kinatokea???haya endeleeni kuwagusa gusa tu wake zenu wakutane na mafisi huko nje.
#KATAA NDOA,NDOA NI........