Diwani
JF-Expert Member
- Oct 25, 2014
- 2,680
- 2,779
Bila shaka mu wazima wa Afya, basi tumshukuru Mungu hata tukiwa si Wazima pia.
Lengo langu kuandika 'Uzi' huu ni kuwahasa na kuwasihi vijana wenzangu ambao bado hatujaoa, kuwa makini na maneno/mawazo/mashauri 'Mabaya' ya watu 'Waliotoswa' na ndoa.
Ndugu zangu; kwa kawaida maisha hayana furaha, uwe umeoa ama hujaoa, ukiwa peke yako shida, ukiwa na mwenza shida, ukiwa na watoto shida na usipokuwa nao pia.
Vile vile maisha ni furaha, ukiwa peke yako raha, ukiwa na mwenzio raha, ukiwa una watoto raha na usipokuwa nao raha; Namanisha kuwa, hakuna neno moja kuhusu jambo lolote. Hata bahati mbaya ina uzuri wake.
Hakuna dunia hii mahala pazuri kama 'Nyumbani' simaanishi lile jengo, namaanisha zile 'Hisia' ambazo kimsingi zinajengwa na Familia, haya wenye pesa na wenye nguvu Ulimwenguni wanafanya maamuzi mengi huku wakiwa wamevuta kamba zao upande wao yaani kwenye "Familia zao".
Usikatishwe tamaa na watu walioacha ama kuachika, na hata wewe ukifanya maamuzi ya kuacha ama kuachika juwa kwamba huyo ni wewe na Moyo wako, usiwakatishe tamaa na wengine. Wape Moyo, kuwa sehemu ya nguzo yao.
"Familia" ni Upendo, familia ni furaha familia ni baraka, Mungu hubariki Familia zaidi kuliko chochote, labda ndio mana Wayahudi, Wazungu na Waajemi wamebarikiwa zaidi kuliko sisi, kwa sababu, Shughuli zao nyingi wamezikabidhi kwa 'Mungu' kupitia Mikono ya Familia. Ila, taasisi inayosimamia Familia ni "Ndoa" Yes, ni Ndoa.
"Ndoa na Iheshimiwe na Watu wote" Kwa maana Mungu hubariki maamuzi ya taasisi hii, Kama Mungu ni Upendo, na Familia ni Upendo, Kwanini Mungu asikae kwenye "Familia"?
Oa, ikifika wakati unataka na unapaswa kuoa, Oa, usikatishwe tamaa na watu aidha kwa 'Kutumwa' au kwa kufanya kwa 'Kunuwia' wanapiga vita ndoa.
Kama ni Muumini, kumbuka Shetani alipiga vita Ndoa ya kwanza pale Edeni, ndio mana ilikuja kuwa chukizo kwa Mungu, lakini kwa Kuwa Mungu aliilinda "Ndoa" miaka mingi baadae, Shetani akashuhudia 'Familia' yenye nguvu zaidi Ulimwenguni, nayo ni Yusufu, Maria na Yesu, kupitia Herode Familia hii ilitafutwa lakini kwa Mapenzi ya Mungu, dunia ilikombolewa.
Ndoa ipo kwenye vita hata leo, simama, kuwa na busara, songa.