Nabisha mbona wachamungu wengi tu ndoa zao changamoto lakini wanaficha tu kwa kivuli cha dini
Ni kweli. Ndoa za sasa zimekaa kimitego sana. Kuna mzee swala 5 na mtu wa dini haswa na muungwana kupitiliza lakini mke kimeo kwelikweli narudia kimeo kwelikweli. Yule mzee anapata taabu sana na mkewe. Anavumilia basi tu.
Mpaka huwa najiuliza huyu mtu wa imani hivi anapata maswahibu kama haya inakuaje tena.
Japo na wanaume vichomi kwenye ndoa nao wapo. Nadhani lililokubwa ndoa inahitaji tafakuri nzito kama kuchagua mchele super. Wanawake kwa waume wa sasa ni wa ovyo kimaadili na kiimani hivyo kupelekea athari katika taasisi ya ndoa.
 
FACTS MAN ndoa zilikua zamani,,sa hiv kati ya ndoa 100 apo 80 zinamatatizo makubwa plus usaliti plus manyanyaso labda zingne ndo zimepona
 
kwa mara ya kwanza naona mwanamke anapinga ndoa humu jf, safi sana

KATAA NDOA

NDOA NI TOZO ZA MWIGULU
 
Wanawake mnalaumiwa huku nyie ndio chanzo Cha hii Kataa Ndoa kwa vijana . Sasa sijui mtaishije.Kwa hiyo mtu itakuwa ukishatoa mahari basi unabeba mzigo shuguli imeishia hapo hakuna cha msikitini Wala kanisani.
 
Mwisho wa siku hakuna taji kwahiyo kwa ambaye hajaweza akae kando. Ila chonde chonde,tafadhali nawaomba sana, nipo chini ya miguu yenu wafikirieni watoto.

Tatizo nchi yetu na jamii nyingi za kiafrica hazina utaratibu mzuri wa malezi ya watoto UKIACHA wale wanaolelewa katika ndoa au wale ambao wazazi wao wanaishi pamoja.

Nchi za wenzetu sheria imejitahidi kushape utaratibu mzuri wa co-parenting ikiwa wazazi hawaishi pamoja, mambo ya pesa ya malezi na kuwepo katika maisha ya mtoto kumewekewa utaratibu mzuri kiasi kwamba watoto wanakua wakielewa kuwa wazazi wetu wanatupenda japo hawakuweza kufanikiwa kuishi pamoja, hata hivyo upande wa pili wa shilingi watoto wa aina hii huwa wanakabiliwa kwa kiasi kikubwa na emotional trauma zinazowapelekea kuwa watu wa "ajabu ajabu" ukubwani. Tofauti kabisa na watoto waliolelewa na wazazi wawili.

Hiki tu ndicho kitu pekee mimi nakihofia. Wakataa ndoa wangefanya kampeni ya kukataa kuzaa mimi ningewaunga mkono 100% hakuna uchaguzi usiokuwa na consequences, siku population ikiwa ndogo akili itatukaa sawa.
 
Mkuu mie nina ndoa takatifu.. nina mke .. sipo kwenye hicho chama cha mpinga Mungu
 
Ban zinatembea kama upupu daah
 
Sio kataa ndoa wala kataa vitu gani
PESA PESA PESA
Wanaume wachache sana karne hii.
Kheee
 
Ndoa ni investment ambayo imekaa kidwanzi sana. Miaka ya nyuma mwanamke alikuwa ni jambo la heri sana kwa mwanaume sababu alikuwa loyal na msaidizi na jamii ililea wanawake kuwa wake za wanaume kama kitu cha kwanza katika maisha yao.

Ila sasa wazazi wakishasomesha binti zao wamemaliza. Hayo mengine watajua huko huko wanapokwenda. Matokeo yake vijana tunakujakupewa majukumu ya kufundisha maadili mtu mzima aliyekomaa akili na hana adabu na mwenendo wake si wa kuridhisha.

Kimsingi ni kama kwenda hotelini halafu ulipie chakula kisha uambiwe nenda jikoni ukapike mwenyewe na uoshe vyombo na kuhakikisha unapiga deki hoteli nzima. Sasa nakuwa nimefuata nini hapo hotelini na si ni bora ningetulia tu home nile cha nyumbani?

Maisha ni changamoto sana.
 
UNA MNUNULIA ZAWADI, UNA GHARAMIA MIHITAJI YAKE YOTE, UNAJARIBU KUTOA ULINZI NA KUFANAYA MWENYE FURAHA. YOTE HI UNAFANYA KWA AJILI YA KUMUONYESA UNAVYO MPENDA.
YOTE HAYA KWA MALIPO YA UNYUMBA TU! KUFANYA MATUSI TU ! BAASI!!!
All in exchange for Sex baaaasi.
 
Hata usipoolewa bado utazaa na utaendelea kufanya majukumu yale yale kwa wanaume za watu na watoto wako. Na huko utateseka mara mbili maana utatakiwa kufanya vile vitu ambavyo mume humsaidia mke kama kutafuta pesa ya chakula, kumlipa house girl (na uombe MUNGU uwe sasa na uwezo wa kukaa nao maana mahousegirl nao siku hizi changamoto),utatakiwa kwanza ulipe kodi then ujenge nyumba kwaajiri yako na watoto. Hapo bado haujaumwa ujitazame afya, uzee ukianza kuingia utatakiwa uendelee kuingiza kipato ili kusapoti maisha yako.

So twende mbele turudi nyuma ndoa ina faida kwa mwanamke kwa asilimia 90% na yeye ndie anaekuja kufaidika mwisho wa siku si mwanaume. Sasa ukisusa Ndoa it means unapoteza hii 90% advantage ya maisha so unabidi kuishi kwa kukaza buti sana.

Anyways, pole sana.
 
Kabisa, jitu linakupangia marafiki wa kuwa nao, mavazi ya kuvaa, siku za kukaa kwenu ukienda kuwatembelea ndugu zako....muda mwingine linakukataza hata kufanya Kazi.
Ndoa ni kuuza utu na kukabidhi Uhuru wako Kwa binadamu mwenzako.
Ukifika miaka 45 hakuna mtu atakuwa na time ya kuhangaika na wewe na uhuru wako[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hapo sasa ndipo umuhimu wa ndoa kwa mwanamke huwa unaanza.

Sasa igeni kuishi kisela, mtajua hamjui.
 
Nyie endeleeni na kampeni yenu ya feminist hutuwataki huku msituharibie focus
Naona wanajaribu kuiga hii movement kama kawaida yao wanadhani kila kitu ni 50/50.

Sasa ngoja sisi tufike 45 tubadili gear angani tunataka kuoa mabinti wapo kibao balaa wanalo wao. Miaka 45 unampata mwanaume gani wa kufunga nae pingu za maisha?
 
Tutabanana huku huku na Sisi hatutaki, tumechoka kufugwaa, tumekataa ndoa....mlidhani wanawake ndo tuna shida ya ndoa? Na Sisi hatutaki.....haina kubembelezana, kataaa ndoa[emoji1787]
#ndoa ni kukabidhi utu wako mikono mwa mtu mwingine
#kataa ndoa
Aaaah weee. Sijawahi ona mwanaume natafuta ndoa. Wewe unaongea uongo hapa. Hivi kijana na binti wakianza kuishi kisela ni nani ambaye ataanza kuingia baridi kuishi na mwenzake bila ndoa?

Kuna mwanamke atakaa na mwanaume miaka 10 bila ndoa wakipika na kupakua bila shida?!
 
Wanaoendaga kutoa mahari ni wanawake? Tatizo wanaume mnaona wanawake tuna shida sana ya ndoa, hata Sisi hatuzitaki, basi tu mfumo WA kijamii unalazimisha kuingia kwenye ndoa
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…