Kaka Mambo ya dini sio Magumu ni watu kuwa wagumu wa kuelewa na wengi hawampi Roho Mtakatifu muda wa kuwafunulia maandiko na Wachungaji na Wainjilisti ndio wanakuwa kila kitu
Kuhusu Bikira Maria, hiyo ni Habari kubwa na sio ya mchezo mchezo,
Kiimani ya Kikatoliki Yesu ni Neno la Mungu nae pia ni Mungu, na Kimaandiko sisi wote ni wakosefu kwa maana tuna dhambi ile ya kurithi, ile laana waliopewa Adam na Hawa mpaka leo tunayo, Mungu akalifanya Neno lake lije Duniani kuwakomboa wanadamu kwenye ile laana iliyotoka kwenye Mti wa katikati kupitia mti wa Msalaba
Yesu kama Mungu alikuwa hawezi kuja kupitia binadamu mwenye dhambi, Hivyo Bikira Maria alikingwa na ile dhambi ya ya Urithi, alikuwa PURE AND FRESH
Malaika Gabriel anatumwa kwa Mungu na anampa Maria ujumbe huu, kwamba MARIA AMEJAA NEEMA, BWANA YUKO NA WEWE NA UMEBARIKIWA KULIKO WANAWAKE WOTE, Pia hiyo Mimba itakuwa ni kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, So Maria ndio Binadamu wa kwanza Duniani kuzipokea nafsi zote tatu za Mungu, BABA, MWANA NA ROHO MTAKATIFU
Baada ya Malaika Gabriel kumwacha Maria, Bikira Maria hakuwa wa Dunia hii tena, alikuwa anatembea na Nafsi zote tatu za Mungu, na alikuwa kwenye Dunia ya Kiroho, Dunia ya watakatifu kwani alikuwa na Mwana wa Mungu ndani yake kwa Uwezo wa Roho mtakatifu
Alipofika kwa Elizabeth na kumsalimia, Yohana aliruka ndani ya tumbo la Elizabeth na Elizabeth alijazwa roho mtakatifu hapohapo Maria hakuwa mtu wa kawaida, na Eliza akijazwa na Roho mtakatifu akajikuta ananena kuwa MARIA WEWE UMEBARIKIWA KULIKO WANAWAKE WOTE
Nae Maria akiwa kwenye utakatifu wake Akasema Luka 1:48- vizizi vyote vitaniita MBARIKIWA
Na kwenye kitabu cha ufunuo kinaonyesha ni kwa jinsi gani Shetani akupenda mpango wa Mungu wa mkombozi kuzaliwa,
Na ishara kubwa ikaonekana Mbinguni, mwanamke mwenye mImba , mwanamke ALIYEVIKWA JUA NA MWEZI UKIWA MIGUUNI MWAKE, anataka kujifungua, na Shetani (Joka) anajitahidi kwa nguvu zote azuie mwokozi asizaliwe
Kasome Ufunuo 11:19 na 12:1-6 kwa habari kamili
Lakini pamoja na hayo yote, kwa Wakatoliki, BIKIRA MARIA SIO MUNGU, BIKIRA MARIA HAWEZI KUSAMEHE DHAMBI, BIKIRA MARIA HAWEZI KUOKOA MTU
KIKATOLIKI BIKIRA MARIA NI KAMA DARAJA LA KUTUUNGANISHA NA MWANAE (Yesu Kristo)
Nitaelezea baadae kivipi?