Sendoro Mbazi,
Mkuu Sendoro Mbazi, hongera kwa kuingia kwenye Kilimo cha mpunga mchango wangu ni huu hapa, utanijulisha iwapo utakuwa ni msaada kukidhi haja yako.
Aina za mbegu
Tumia mbegu iliyothibitishwa na wataalamu iitwayo SARO (TXD 306), inazaa sana gunia 32 kwa ekari moja.
Mbegu hii inaradha nzuri na inakubalika kibiashara. Ekari moja hutumia kilo 10 kwa mpunga wa kupandikiza.
Andaa sh 2500 x 2.5 jumla sh 6250 kama itabidi uzifuate mbali ongeza nauli na gharama za safari zote.
Pump
Tumia pump ya inchi 3 sawa na horse power 5 hadi 6. Ninauzoefu na pump ya JD ni ya petrol. Ekari moja petrol ni lita 5 lakini kwa mpunga itabidi uloweshe shamba mara mbili kwa wiki!
Pump 450,000/= mipira inategemea na umbali toka source ya maji, Pipe ya kunyonyea maji kwenye source 1m sh 8000, utahitaji at least mita 4, (32,000/=), pipe ya kupelekea shambani roll moja urefu wa mita 100 kama litatosha mita 1 sh 2000 ( 200,000/=) dumu la lita 20 kuhifadhia mafuta 3,000 dumu dogo la kupelekea mafuta shamba 1500/=, Petrol lita 4 kwa ekari moja x eka 2.5 x 2 kwa wiki x wiki 6 (assume 6 weeks rain, 6 weeks no rain) x bei ya petrol lita moja 2300/=, service ya pump lita moja ya oil inatosha hadi unavuna, tenga pembeni shs 10,000/= kwa service. Usafiri wa kupeleka na kurudisha pump kama huna baiskeli tenga 2000 kila siku ya kumwagilia kwa umbali ndani ya kilometer 5.
Hapa andaa jumla ya shillingi 974,500/=.
Kama ni shamba jipya
Kutengeneza majaruba idadi yake inategemea mtelemko wa shamba - andaa 50,000/= kwa ekari
kusawazisha ndani ya majaruba (hii ni kazi ngumu na kubwa sana kutegemea na slope ya shamba) andaa angalau laki 3 kwa kila ekari moja. Shamba la mpunga sharti liwe level ili kumwagilia kwa urahisi, hii ni very expensive operation, kutengeneza shamba la mpunga ni kama ujenzi wanyumba, ukishatengeneza unabaki ukarabati tu.
Andaa 350,000/= x 2.5 jumla 875,000
Bei ya shamba 50,000 x 2.5
jumla 125,000/=
Gharama zingine za shambani zote kwa ujumla hadi unarudisha mzigo tenga pembeni sh 700,000/= kwa ekari moja kwa hiyo j
umla gharama 1,750,000/=
Jumla ghafi 3,730,750/= ongezea 10% tahadhari (373,075/=)
Jumla kuu 4,103,825/=
Ukifuata utaalamu utavuna gunia 32 kwa ekari lakini kwa kuwa na uhakika assume mavuno gunia 25 kwa ekari. Uza bei ikifikia 80,000/= kwa gunia la kilo 100/=
Mapato itakuwa 5,000,000/=
Faida 5,000,000/= kutoa 4,103,825/= inabaki 896,175/=
Mahesabu yanaonesha kuwa utarudisha pesa uliyowekeza na kupata faida
Faida kubwa zaidi ni shamba ambalo utakuwa umeshali-level tayari itakusaidia kuwa na gharama kidogo za umwagiliaji na level inafaida nyingi sana, hutaingia garama hii ya levo miaka ijayo bali ni kufanya usawazishaji mdogo tu.
Nakushauri ukitaka kufanikisha kilimo cha mpunga hakikisha unaweka shamba lako level, yaani ukiweka maji kwa kina cha sm 1 au 2 yasambae jaruba lote kwa kina cha sm1 au 2. Level kweye shamba la mpunga haina mbadala, kutengeneza jaruba na kuweka level ni mambo ya LAZIMA kwenye shamba la mpunga!
Nimewasilisha !!!