MJADALA: Maswali, majibu na ushauri kuhusu Kilimo cha Mpunga cha kitaalam pamoja na masoko yake

MJADALA: Maswali, majibu na ushauri kuhusu Kilimo cha Mpunga cha kitaalam pamoja na masoko yake

Inaonekana Chodoo hata huko kijijini hajafika na yuko tu mjini maana hata jina la kijiji hatwambii wadau kote huko tunapajua! Je yuko Ndumbuli,Lipangalala, Kikwawila au wapi?????
 
Inaonekana Chodoo hata huko kijijini hajafika na yuko tu mjini maana hata jina la kijiji hatwambii wadau kote huko tunapajua! Je yuko Ndumbuli,Lipangalala, Kikwawila au wapi?????

Mmh jamani hata kusoma umeshindwa, au ulitaka kuandika tu, mbona nilishajibu kwamba ni kikwawila
 
mkuu tupo sambamba katika hiii project, mpaka mwisho tunaomba uendelee kuwa muwazi hivihivi tupate hali halisi. shukrani sana.
 
Naomba ushauri jinsi ya kuanzisha shamba dogo la kilimo cha mpunga; maelezo yangu ya awali ni kama ifuatavyo

  1. lengo ni kujiongezea kipato
  2. eneo ni eka 2.5
  3. aina ya mbegu : za muda mfupi zinazonukia , kwa ajili ya kuvutia wateja
  4. aina ya kilimo : ningependa kununua pampu ya kutumia petrol/diesel ili niongezee maji wakati pakiwa na upungufu wa mvua; niwe namwagilia ndani ya vijaruba vidogo; naomba pia ushauri kuhusu aina ya pampu
  5. nitaajiri kibarua 1; atafanya kazi za ulinzi na palizi
  6. Ardhi ni ya kununua ( Tshs 50000 kwa eka), maji yapo ndani ya mita 50 na ni ya kudumu
  7. Mtaji nitategemea mkopo kutoka benki nitakaorejesha ndani ya miaka 4
Naomba ushauri wa hali halisi ya kilimo hiki, je bajeti yangu inatakiwa iewje(kiasi gani), je eneo linatosha au halitaweza kulipa gharama za uendeshaji?, nitaweza kubreak even baada ya muda gani

nawasilisha
 
Ngoja waje wakuu Kubota , ureni etal ,naamini na mimi ntafaidika na mawazo watayoleta wadau hapa
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Sendoro Mbazi

eka 2.5 ni sawa na hekta 1, hapo unapata vijaruba 25 vya 20 x 20
kulima kila kijaruba sh 3000(makadirio kibarua), jumla 75000
kwa trekta 50,000 x 2.5 = 125,000
kusawazisha/ harrowing 30 x 2.5 = 75000.

Mbegu tafuta kwa wakulima ndio za uhakika zaidi japo madukani ni kati ya 2500 mpaka 3500
ukisambaza mbegu/broadcasting utahitaji kg 20 x 2.5 = 50 x 3000 = 150,000
ukipanda kitaluni kg 3 x 2.5 = 7.5 x 3000 = 22500 (kuna gharama za kuotesha miche)

Palizi 2, (25 x 3000)2 = 150,000.

niishie hapo kwanza..
sijataja gharama za kuvuna kupiga na kuhifadhi na vingine kama nimesahau

NB: kijana mmoja hawezi palilia peke yake kama hujapanda kwa mistari itamgharimu muda mwingi sana
 
Last edited by a moderator:
Sendoro Mbazi,

Mkuu Sendoro Mbazi, hongera kwa kuingia kwenye Kilimo cha mpunga mchango wangu ni huu hapa, utanijulisha iwapo utakuwa ni msaada kukidhi haja yako.

Aina za mbegu
Tumia mbegu iliyothibitishwa na wataalamu iitwayo SARO (TXD 306), inazaa sana gunia 32 kwa ekari moja.
Mbegu hii inaradha nzuri na inakubalika kibiashara. Ekari moja hutumia kilo 10 kwa mpunga wa kupandikiza.
Andaa sh 2500 x 2.5 jumla sh 6250 kama itabidi uzifuate mbali ongeza nauli na gharama za safari zote.

Pump
Tumia pump ya inchi 3 sawa na horse power 5 hadi 6. Ninauzoefu na pump ya JD ni ya petrol. Ekari moja petrol ni lita 5 lakini kwa mpunga itabidi uloweshe shamba mara mbili kwa wiki!

Pump 450,000/= mipira inategemea na umbali toka source ya maji, Pipe ya kunyonyea maji kwenye source 1m sh 8000, utahitaji at least mita 4, (32,000/=), pipe ya kupelekea shambani roll moja urefu wa mita 100 kama litatosha mita 1 sh 2000 ( 200,000/=) dumu la lita 20 kuhifadhia mafuta 3,000 dumu dogo la kupelekea mafuta shamba 1500/=, Petrol lita 4 kwa ekari moja x eka 2.5 x 2 kwa wiki x wiki 6 (assume 6 weeks rain, 6 weeks no rain) x bei ya petrol lita moja 2300/=, service ya pump lita moja ya oil inatosha hadi unavuna, tenga pembeni shs 10,000/= kwa service. Usafiri wa kupeleka na kurudisha pump kama huna baiskeli tenga 2000 kila siku ya kumwagilia kwa umbali ndani ya kilometer 5.
Hapa andaa jumla ya shillingi 974,500/=.

Kama ni shamba jipya
Kutengeneza majaruba idadi yake inategemea mtelemko wa shamba - andaa 50,000/= kwa ekari
kusawazisha ndani ya majaruba (hii ni kazi ngumu na kubwa sana kutegemea na slope ya shamba) andaa angalau laki 3 kwa kila ekari moja. Shamba la mpunga sharti liwe level ili kumwagilia kwa urahisi, hii ni very expensive operation, kutengeneza shamba la mpunga ni kama ujenzi wanyumba, ukishatengeneza unabaki ukarabati tu.
Andaa 350,000/= x 2.5 jumla 875,000

Bei ya shamba 50,000 x 2.5 jumla 125,000/=

Gharama zingine za shambani zote kwa ujumla hadi unarudisha mzigo tenga pembeni sh 700,000/= kwa ekari moja kwa hiyo jumla gharama 1,750,000/=

Jumla ghafi 3,730,750/= ongezea 10% tahadhari (373,075/=)

Jumla kuu 4,103,825/=


Ukifuata utaalamu utavuna gunia 32 kwa ekari lakini kwa kuwa na uhakika assume mavuno gunia 25 kwa ekari. Uza bei ikifikia 80,000/= kwa gunia la kilo 100/=
Mapato itakuwa 5,000,000/=
Faida 5,000,000/= kutoa 4,103,825/= inabaki 896,175/=

Mahesabu yanaonesha kuwa utarudisha pesa uliyowekeza na kupata faida
Faida kubwa zaidi ni shamba ambalo utakuwa umeshali-level tayari itakusaidia kuwa na gharama kidogo za umwagiliaji na level inafaida nyingi sana, hutaingia garama hii ya levo miaka ijayo bali ni kufanya usawazishaji mdogo tu.

Nakushauri ukitaka kufanikisha kilimo cha mpunga hakikisha unaweka shamba lako level, yaani ukiweka maji kwa kina cha sm 1 au 2 yasambae jaruba lote kwa kina cha sm1 au 2. Level kweye shamba la mpunga haina mbadala, kutengeneza jaruba na kuweka level ni mambo ya LAZIMA kwenye shamba la mpunga!
Nimewasilisha !!!
 
Thanx KXY, notes nzuri sana, nimeshapata eneo hilo hivyo nitawapa feedback
Kwa kuongezea kuhusu pampu:

mkuu Kubota kaelezea vizuri na mchanganuo wake umegusia mambo mengi ya msingi, kwa uzoefu nilionao eneo la hekta 1 pampu ya inch 2 inatosha japo pia inategemea chanzo chako cha maji. kadri upana unapoongezeka ndio pampu inavuta maji mengi kwa mda mfupi sasa kama ni visima vyetu vifupi itakuwa usumbufu sana.

kwa kupunguza gharama pia bila kuathiri sana ufanisi,
pampu inch 2 sh 210,000 - 230,000 (Honda)
Mpira wa kumwagilia roll 100M sh 130,000 (japo kama miuondombinu ya mifereji iko vizuri 50m inatosha kwa sh 70,000)

NB:Kazi ya kukunja na kukunjua mpira wakati wa kumwagilia si ndogo kwasababu mpira hautakiwi kujikunja, unapojikunja unaongeza mzigo wa kusukuma maji kwahiyo mafuta yanaenda zaidi na mpira unaharibika mapema. lizingatie hili pia wakati wa kuamua urefu wa mpira unaohitaji
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom