Mjadala: Nini chanzo na tiba ya tatizo la upele kuota kwenye uume?

Mjadala: Nini chanzo na tiba ya tatizo la upele kuota kwenye uume?

Ndo raha ya JF mkuu kuna utani na usiriaz so I hope utakuwa umepata majibu kwa watu makini wenye uelewa na huo ugonjwa so ni jukumu lako kwenda kwa seehhemu husika na kwa watu makini zaidi....

Mm nakumbuka mwaka 2016 nilimgegeda demu wa kitaa kumbe yule demu alikuwa na kisonono na mm nilikuwa sijui vizuri huu ugonjwa dalili zake zilikuwaje na mzee baba nilizama kavu kavu, halafu nilikuwa na safar ya kutoka Dar kwenda Moshi the next day, basi kesho yake nikasafiri kwenda moshi nilipofika moshi maumivu makali nilianza kusikia wakati wa kukojoa na kutokwa na usaha wa njano...Isee niliogopa balaa ikabidi nizame Jf nikaweka Uzi, nashukuru Mungu kuna waliotoa maneno ya kashifu Ila kuna wengine walitoa maneno ya kutia moyo na kunipa mwanga nn cha kufanya..

Basi nilichofanya nikawasiliana na bro maana nilienda kumtembelea yeye moshi wakati huo alikuwa anafundisha Kilimanjaro school of pharmacy na uzuri alikuwa anafahamiana na doctors wa KCMC, moja wa madaktari aliowaamini akaniandikia dozi hiyo Kali sikuchelewa nikaipiga ilikuwa ya siku moja tu, baada ya siku 2 nikawa nipo normal hapo nikajifunza kutumia kinga Mara kwa Mara.

Kingine nilichojifunza nikuwa wadada wanaweza wakawa na huu ugonjwa wa kisonono lakini huwachukua siku nyingi kugundua kuliko wanaume na yule demu nilitemana naye mwisho wa siku
 
Pole boss, kwa muonekano wa hivo vijipele naona ni kama vile vya Herpes simplex virus Genital sores na mara nyingi huambatana na vipele vya mdomoni na kama vimetokea sehemu ya ubavu yaweza kuwa relapse ya previous HSV infection.

Maambukizi.Ugonjwa huo huenezwa kutoka kwa mgonjwa kwenda kwa mtu mwingine kukutana kwa majimaji ya mwili kama mate, maji ya ukeni au shahawa.

Vihatarishi/Risk factors : ni kuwa na ngono zembe mara kwa mara, kuwahi kuumwa magonjwa ya zinaa au maambukizi ya VVU.
Matibabu: Unaweza ukaandikiwa dawa kama acyclovir (Zovirax), famciclovir (Famvir) au AntiVirals nyingine.

Ushauri: Ni vema ukamwona daktari kwa uchunguzi zaidi, na ufikirie kupima maambukizi ya HIV/AIDS ili ufahamu afya yako na ujijengee mikakati kama Other STIs umeshapima.
 
Back
Top Bottom