Stanboy
JF-Expert Member
- Jul 4, 2013
- 1,115
- 1,328
- Thread starter
- #61
Broker, Agent, wakala, Dalali.......wote hawa ni kitu kimoja inabadilika lugha tu na mbwembwe kibao. ni sawa na kusema mshahara, overtime, pensheni, ada.....zote ni malipo. nenda Toyota Japan waambie nataka gari jipya toyota hawatakuuzia watakwambia nenda kwa agent wetu Toyota Tanzania Ltd. Huyo ndio waliompitisha kuwa Dalali wao kuuza magari yao. Huyo ndio atakayeongea na wateja wa tanzania. Ndiye atakayewaeleza soko la tz. Nenda kampuni ya Heineken pia watakwambia sisi Tanzania tuna agent wetu yaani Dalali wao. Nenda nje ya TZ huko majuu nyumba za kupanga zipo hivi unadhani unaweza kupata nafasi ya kuongea na Tajiri mwenye nyumba . Utatoa wapi hiyo nafasi Tajiri ni Tajiri kweli ana nyumba zaidi ya 500. Atapata wapi nafasi ya kukusikiliza wewe unayetaka chumba kimoja. Tajiri ana nyumba au mali lakini hajui soko linaendaje au soko likoje kwa kipindi kile. Hapo ndio kazi ya Dalali. Dalali ndio anahangaika kufungua ofisi, kutafuta wateja, kuisifia nyumba na kuitangaza. ........mfano wewe umetoka zako kijijini umekuja kununua gari used ya mtu dar. je utajua ni gari ipi inauzwa na mwenye gari yuko wapi je unaweza kubargain naye. Je anaweza kukusikiliza? Hapo lazima utafute Dalali. Ni majina tu yanabadilika ila kazi ni ile ile. Ila bongo tu kwa vile hii kazi haina utaratibu haijapitishwa kama ni kazi rasmi ndio maana watu wanapigwa. Dalali anavuta. hela mara mbili yaani Kote Kote........kuna mtu kasema eti kutafuta nyumba sio kazi. nani kakwambia Hebu jaribu kuzunguka dar utafute nyumba uone kama hujaishia kutapeliwa
Binafsi nakubali wana msaada kiasi fulani,lakini wanamuumiza mno..