HOJA MJADALA: Nini kifanyike kuwadhibiti madalali wa nyumba, vyumba, mashamba, gari n.k?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika

Binafsi nakubali wana msaada kiasi fulani,lakini wanamuumiza mno..
 
Dawa kuanzisha umoja wa wamiliki wa nyumba na kutoa tamko la kutowatambua madalali maana wamekuwa kama parasite kwenye nyumba na viwanja vyetu

Sent from my SM-J200H using JamiiForums mobile app
 
Baba yako angekua dalali usingepost ushuzi kama huu.

Big head thinner brain

Sent from my Halotel H8401 using JamiiForums mobile app
 
sallam humu..bila kusahau kwa wale wataohitaji au wanaohitaji nyumba ..viwanja..frame..nk Dodoma msisite kuntafuta tusaidiane kupata hitaji lako..ahsanteni

Sent from my SM-G313H using JamiiForums mobile app
 
Binafsi nakubali wana msaada kiasi fulani,lakini wanamuumiza mno..
Team iko ulaya inataka mchezaji africa. Mfano samatta. Hapo ni lazima dalali ahusike maana issue sio tu kucheza mpira ni lazima pia wajue na tabia ya mchezaji nje ya uwanja na mambo yake binafsi. Sasa hapo ndio kazi ya dalali. Au wewe unatafuta nyumba. Hujui tabia ya kwenye ile nyumba au ya mwenye nyumba sasa hapo mwenye kukupa ukweli au kukuangusha ni dalali. Unaweza panga nyumba kumbe kwenye nyumba kuna mtoto wa mwenye nyumba mwizi au nyumba ina mgogoro wa kifamilia au ina mgogoro na bank au nyumba imeuzwa. Wewe umetoka zako huko mkoa utajuaje
 
Kazi yao sawa lakini wao hawalipii kodi...biashara yao sio rasmi so wanambana mlaji
 
Huku kwetu hawalipi kodi
 
Hebu acha kutetea uovu kwa mambo yasiyo na uhusiano na uovu......bilashaka wewe ndio ile sampuli ambayo unatetea ati wacha mafisadi waendelee kuiba serikalini maana nao wanafamilia wanazilea.....wanawatoto wanasomesha......hebu kuwa serious kidogo basi
 
...Anayefanya kisheria analipa kodi but hawa wakwetu hata akipiga ndefu zote anatia mfukoni
 
Sijaelewa unaniattack mimi personally au unataka tujadili hoja iliyopo mezani. Hili jukwaa huru mkuu kila mtu kuna angle yake ya kuliona jambo. Kosoa hoja yangu kwa hoja ya kunishawishi
 
Ingawa mtiririko wa hoja yako hauna maaana kimantiki kuhusiana na hoja iliyopo mezani ngoja nijibu hoja yako.

Sioni kwamba wakifanyacho madarali ni 'uovu' pengine utupe tafsiri ya neno uovu kwa muktadha uliopo. Lakini pia ukishasema naweza kutetea mafisadi kwa kuiba pesa za umma. Unafananisha wizi na udalali unafanya makosa makubwa sana, wizi ni jinai na udalali ni huduma. Sifa ya huduma inaweza kuwa nzuri kwa mtu mmoja na ikawa kero kwa mtu mwingine. Kitu cha msingi ni kujaribu kuishauri Serikali kupitia Serikali za mitaa kuratibu shughuli za hawa madalali ili iwe chanzo cha mapato kwa serikali kutokana na kulipa kodi kwa huduma zao lakini pia kuwe viwango sawa kwa huduma zao.

Hakuna sehemu duniani kusipokuwa na madalali. Jiulize leo, Serikali ingekuwa inakusanya kodi za maegesho yenyewe bila kutumia madalali ingekuwaje?, fikiria mimi nipo busy na majukumu nataka chumba, nyumba, shamba n.k sehemu ambayo sina uzoefu nayo bila msaada wa hawa madalali inakuwaje?
 
Sijaelewa unaniattack mimi personally au unataka tujadili hoja iliyopo mezani. Hili jukwaa huru mkuu kila mtu kuna angle yake ya kuliona jambo. Kosoa hoja yangu kwa hoja ya kunishawishi
Hapo nakujenga maana unaonekana hata haujawahi kukutana na hao madalali wakakupa hasara. Sisi ambao tumeshakutana nao ndio tunawaelewa utapeli wao upo wapi....sasa wewe out of no where unakuja unaanza tetea uhaini wao kwenye biashara ya makazi......cheeeeh wataka tukueleweje?!
 
Sasa wewe hujakutana na madalali umekutana na matapeli. Si kila dalali ni tapeli ila kuna matapeli wanajifanya madalali
 
Ingawa mtiririko wa hoja yako hauna maaana kimantiki kuhusiana na hoja iliyopo mezani ngoja nijibu hoja yako.

Sioni kwamba wakifanyacho madarali ni 'uovu' pengine utupe tafsiri ya neno uovu kwa muktadha uliopo. Lakini pia ukishasema naweza kutetea mafisadi kwa kuiba pesa za umma. Unafananisha wizi na udalali unafanya makosa makubwa sana, wizi ni jinai na udalali ni huduma. Sifa ya huduma inaweza kuwa nzuri kwa mtu mmoja na ikawa kero kwa mtu mwingine. Kitu cha msingi ni kujaribu kuishauri Serikali kupitia Serikali za mitaa kuratibu shughuli za hawa madalali ili iwe chanzo cha mapato kwa serikali kutokana na kulipa kodi kwa huduma zao lakini pia kuwe viwango sawa kwa huduma zao.

Hakuna sehemu duniani kusipokuwa na madalali. Jiulize leo, Serikali ingekuwa inakusanya kodi za maegesho yenyewe bila kutumia madalali ingekuwaje?, fikiria mimi nipo busy na majukumu nataka chumba, nyumba, shamba n.k sehemu ambayo sina uzoefu nayo bila msaada wa hawa madalali inakuwaje?

Na ndipo hapo sasa sisi tunahoji mbinu wanazotumia katika kufanya hiyo biashara ya udalali. Sasa wewe kwa mfano nyumba inapangishwa kwa bei ya laki 2 kwa mwezi, ila dalali atamdanganya mteja kuwa hiyo nyumba inapangishwa kwa shilingi laki tatu na nusu ili tu ampige.....na kumbuka katika bei hiyo bado mteja atawajibika kulipa hiyo laki tatu na nusu mara miezi sita au kumi na mbili plus atatakiwa kumtoa dalali na laki tatu ya mwezi m'moja lakini hapo hapo huyu dalali atataka kupewa tena malipo toka kwa mwenye nyumba kwa kazi ya udalali huu wa kitapeli.

Kwa nifahamu mimi kazi yoyote ya udalali (brokerage) huwa inalipwa ujira na yule anaye tafutiwa wateja yaani m'miliki wa mali tena kwa fixed percentage (usually 10%) maana 20% hutumika sana na mawakala (agents). Na kwa upande wa mteja yaani client, atatakiwa lipa fee ndogo sana kama service charge! Sasa huu upuuuzi unaoendelea bongo hata haukustahili kuutetea mr.
Sasa wewe hujakutana na madalali umekutana na matapeli. Si kila dalali ni tapeli ila kuna matapeli wanajifanya madalali
 
Nyie ndio mnao waendekeza,kuna nyumba aliipenda brother wangu ilikua tshs 800,000/month,dalali akamwambia atachukua kodi ya mwezi,bro akasema nipeleke nikaione kwanza,dalali kapewa 20,000 tukaenda kuicheki nyumba,kisha tukamwambia mpigie mwenye nyumba aje asbh,kesho yake bro baada ya kuonana na mwenye nyumba akamwambia atalipa hiyo 800,000x18months=14,400,000..kisha akamwambia dalali kwamba atampa laki tu bcoz pesa aliyonayo ni 14,500,000 pekee,kama hataki basi ataachana na hiyo nyumba,mwenye nyumba kusikia hiyo mihela akasema nyumba ni yangu na dalali hajui ata nikitumia tofali ngapi so twende sehemu husika nikupe mkataba unipe pesa,dalali hakua na namna zaidi ya kukubali hiyo 100,000!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…