HOJA MJADALA: Nini kifanyike kuwadhibiti madalali wa nyumba, vyumba, mashamba, gari n.k?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Daaah wanazngua kinoma yaaan wqnaish kijanja janja mjini na vitamb wanatoka kwa pesa za bure. Mm huaga nawakomesha na huaga sipend ujinga kabsa kwenye pesa
 
Jiulize, ni sahihi kuwaondoa madalali wanaojiita mawakala wa 'Tigo pesa' na wengine?
 
SIKU ya kulipa mzunguke DALALI, Nende peke yko...ukifika mbane mwenye eneo au nyumba utapata ukweli wa bei halisi....na km Ataonyesha UGUMU WA KUSHUKA,,,TISHIA KUVUNJA BIASHARA..,hakuna mwenye mali atakaye kataa pesa. .lazima atakubali tu kushusha bei... DAWA NI KUMZUNGUKA TU DALALI. ndy maana madalali wakijuwa mteja anakuja kulipa ksho AISEE HAWACHEZI MBALI NA ENEO LA TUKIO...
 
Uza, Nunua, Panga, Pangisha :
Nyumba, Ofisi, Yard, Maghala, Mashamba, Viwanja- Dar.

Pia, Dhahabu ghafi, Vito ghafi, Machimbo na Migodi pamoja na Mazao ya Shambani.

-Kwa Dar na kwa baadhi ya Mikoa.

Pia, Napangisha Ofisi (tu) katika karibia Miji yote mikubwa Duniani.
Tupo katika Nchi 100 na katika Miji mikuu zaidi ya 200 Duniani-

ANGALIZO:
MALIPO YA DALALI NI KODI YA MWEZI MMOJA (Kwa Nyumba/Vyumba vya kupanga.
MALIPO YA DALALI NI 10 % (Kwa Nyumba/Mashamba ya kununua)

USISITE KUWASILIANA NAMI:+255-714-591548
Nawasilisha.
 
Namchukia sana mtu anae itwa dalali katika maisha yangu najaribu sana kuepuka kufanya biashara na mtu anae itwa dalali kwa sababu kwa lugha rahisi twaweza muita kua ni mwizi ambae hakufuzu vizuri ila alikonea form two C
 
Madalali ni watu muhimu sana, ivi mtu unatafuta nyumba au chumba.
Utauliziaje hadi upate ?

Yaani upite mtaa kwa mtaa unaulizia nyumba au shamba au chumba hapa mjini..!
ina maana uache shughuri zako zoote uingie mtaani nyumba hadi nyumba kuulizia chumba..!
Hakika nashindwa kutabiri matokeo yake.
Madalali wapo dunia nzima na ndio kazi yao kutafuta vitu ambavyo wateja wake hawajui watavipata wapi, na pia husaidia kutafuta soko la bidhaa inayouzwa kwa haraka sana.
Madalali inabidi wasajiriwe ili kazi zao zihalalishwe na wasiwadhulumu wateja wao, na walipe kodi.
mfano, madalali wanaouza mazao ya wakulima sokoni wanamrahisishia mkulima kuendelea na kazi zake na kuja kuchukua pesa yake mazao yakishauzwa.
Madalali makanjanja nao wapo na wanasaidia sana kwa maswala madogo kama ya kutafuta chumba.
Fikiri umetoka mkoani na unaanza kazi mjini Daresalam utaulizia wapi chumba na wewe ni mgeni..!
Dawa ya madalali wewe wambie wakutafutie kitu unachotaka wakisha kuonesha waambie unaenda kujipanga halafu rudi kwa mda wako au mwalekeze mtu mwingine kwa mwenye mali ili uzungumze naye ana kwa ana kuhusu hicho chumba au bidhaa ili upate maoni ya mwenye mali kuhusu hiyo bidhaa.
Utapata ukweli kuhusu bei halisi ya bidhaa hiyo.

Madalali ni watu muhimu sana na wana mchango wao katika maisha ya kila siku.
 
Madalali sio watu wa kufukuzwa ama kutoheshimiwa.Mimi naona ni vyema kama hata wakipewa mwongozo wao na kuwa na ofisi zao hata vilinge lakini wakipokea kazi basi kuwe na kiasi cha kuchukua kutokana na kazi yenyewe na kiasi cha serikali kama watawatambua na kuwaheshimu katika kazi zao.Kuna watu hawajui kuongea na mteja, mfano mtu anataka kuuza kitu chake kwa sh.100 na lengo ni hilo lakini anajikuta anauza kwa sh.30 sababu hana msaidizi katika kujua wapi na nini kifanyike.Serikali nayo pia ina udalali katika DINI ndio maana inapigania vitu vya DINI viweze kuingia bila kodi toka nje ya nchi huo pia ni udalali ambao ni hatari zaidi kuliko huo mnaosema.
 
Hawa madalali sitaki kuwasikia kabisa 5000 zangu nyingi wamezila kwenda kunionesha nyumba mbovu balaa
 
Uhuru wa kutaka kitu ka
Huwa nawaelezea kabisa ila ukifika kule longolongo zinaanza
uhuru wa kutaka kitu kamili upendacho uko katika maamuzi yako.Heri yule uliyempa riziki yake akale kama wewe, huyo atakuita boss lakini vipi yule atakaye kufanya ununue kitu kimoja mara mbili?
 
Uhuru wa kutaka kitu ka

uhuru wa kutaka kitu kamili upendacho uko katika maamuzi yako.Heri yule uliyempa riziki yake akale kama wewe, huyo atakuita boss lakini vipi yule atakaye kufanya ununue kitu kimoja mara mbili?
Mmh ni shida
 
Wanalipa kodi kiasi gani kulingana na vipato vyao? Tatizo huangalii upande mwingine, hao hao madalali ndo wanaongezea wenzao mzigo wa maisha, mtu mmoja alipe kodi ya miezi 6 + udalali kodi ya mwezi mmoja, isitoshe huyo dalali hakuna mahali anakatwa income tax, huoni kuwa hiyo ni hasara kwa taifa?
 
Huko tuendako wenye nyumba pia wajipange kutumia tu mitandao, maake hawa madalali wao uchwara wanaongeza tu gharama za maisha. Mi kuna mfanyakazi mwenzangu katapeliwa 3.6m hivi hivi na hao madalali.
 
Duh! yani unatoa 500k usawa huu bila hata kupewa risiti? kweli we ni wa kipekee. Unampaje dalali pesa yote hiyo? Nyie ndo mnawapa viburi hawa wahuni mjini
 
Baba yako angekua dalali usingepost ushuzi kama huu.

Big head thinner brain

Sent from my Halotel H8401 using JamiiForums mobile app
Madalali hasa wa nyumba na magari wengi na watu walio wavivu kufikiri, hawapendi kujishughulisha, watu wanaopenda mteremko....huo ndo ukweli mchungu
 
Hatuwezi kuwa kwnye nchi ya watu wanaojielewa halafu swala nyeti kama makazi likawa holela holela tu. Lazima tuwe na sheria za kudhibiti hili. Nyumba ni moja ya mahitaji ya muhimu kwa binadamu, hatuwezi kuacha soko liwe huru 100% kama bidhaa nyingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…