TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Bukoba Mjini

Obakesye mshaija mkuru
 
Ungepata kamda ukasogea site tukapata tupicha ingekaa vizuri sana. Kuna na mradi wa barabara chini ya pesa ya w.bank sijui nao umefikia wapi tokea yule mkandarasi aliyegoma kusaini kukamatwa
 
Ndugu zangu baada ya kuwa nimepiga moyo konde na kuchukua uamuzi wa kurejea nyumbani, mimi mwenyewe na binafsi nimeamua kwa kuanza niingie katika ngazi za kuomba uongozi ili niweze kuwatumikia wanamkoa wetu kwa urahisi.

Na ili kufikia hazma yangu hiyo, nimeamua pia kupitia katika siasa. Kwa maana natizamia nafasi moja kati ya ama udiwani ama ubunge ili kuelekea huko. Ama katika udiwani ili niingie katika baraza la madiwani manispaa na kuleta mitizamo mipya ama kupambana kuelekea bungeni ili kuingia katika chombo kikubwa kwa taifa letu

Najiamini na naamini huo uwezo ninao, changamoto iliyopo ni kwamba bado sijaamua hasa ni nafasi gani nianze nayo. Katika hili ndio maana kupitia kwenu naomba nipate mawazo na ushauri wenu juu ya ni ngazi gani inafaa nianze nayo na niwahakikishie, nitayaheshimu na kuyazingatia sana mawazo yenu mtakayoyatoa

Asante sana na karibuni kwa mawazo na ushauri

Rweyemamu.
 
juzi mkuu wa mkoa alisema hakuna mradi kama huo Bukoba
Kweli hata mie niliona anaongea na mie nilishasema mara nyingi, yule hafai kuwa pale hata ukimuona anaongea unajikuta unatamani hata kwenda kulala. Hizi kazi za kuongoza raia ni tofauti kabisa na jeshi na kwa vile alishakuwa mstaafu jamaa angemwacha tu akastaafu. Ukiona anavyoongea unaelewa ni kwanini stand hii pamoja na hatua ilikofikia inashindwa kuendelea.

Unajifikilia ingekuwa kwa mkuu wa mkoa wa Simiyu/Shinyanga hii stand ingekwama kweli, jibu ni hapana. Uwezo wa kuchambua na kushawishi huyu mzee hana, spirit ya kuona mambo yanakimbia kwa spidi hana ..mwisho wa siku, tuna mtizamaji tu.

Aliongea eti tumepewa soko, soko lenyewe liko wapi ..hata sielewi liko wapi labda mlioko hapo mtwambie kuna hatua gani kuhusu soko. Kila kitu kipo kwenye 0. Meli tumeambiwa iko kwenye 0, stand inarudi kwenye 0 yaani every project iko kwenye 0 not even nearing the commencement. Serikali ya mkoa iko hoi kuliko ajuza wa miaka 200
 
Sio wew unayeshangaa tu pia hata watu tuliiopo bukoba kama tunawatch movi yaani huyu anasema hiki huyu kile hatuona kinachotendeka soko halijengwi,stendi kama imekwama,barabara haziishi,ihungo haishi,meli haiji yaana ni shida tupu na mji unapanuka ovyo bila mpangilio yaani sijui tufanyeje wanabukoba.ila nadhani kuna upinzani mkubwa wa kisiasa kati ya chadema na ccm unaendelea yaani wanagombania jimbo kiasi kwamba manispaa ikitaka kufanya kitu ccm wanapinga ili wapate upenyo 2020 na serikali haitoi support kubwa kisa mji wa chadema wakati hawajui wanaumiza wengi na walaaniwe sana watu hao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na kinachoumiza ni ujinga wa raia, yaani wapo wapo tu kama wadudu na wasijua kesho. Obufela ndwala
 
alisema hakuna mradi gani?
Kuhusu stand ya mabasi alisema serikali imekubali kutoa pesa kwa ajiri ya soko tu kwahiyo stand haiko kwenye mipango ya serikali hii tukufu.

Sasa hilo soko lenyewe lishaanza ama ndo yale yale ya wachenge huku wakigeuka watie kanzu wakija kushangaa mpira umeisha! Wanacheza mchezo wa maneno tu na bila aibu usishangae kesho wakakwambia hata hilo soko serikali haijawahi kupanga kutoa pesa ...yaani ni ikwamishe Kagera hadi basi.
 
Stand inajengwa kwa mapato ya ndani ya Halmashauri na ujenzi wake unaendelea ingawa kuna changamoto zinazosababisha mradi kusita sita. Soko bado halijaanza kujengwa
 
Yaani sijui nini kinakwamisha pesa IPO lakini soko halijengwi na hakuna utaratibu wowote uliopo
 
Umaskini katika mkoa wetu Kagera na baadhi ya mikoa mingine, ulisababishwa na mambo yafuatayo:-
1.Kuanguka au kudorora kwa vyama vya ushirikika kama vile BCU,BBU,UNGA,KNPA, N.K.

2.Kushushwa bei kwa zao la buni/kahawa.

3.Kudhoofika kwa baadhi ya viwanda kama vile kiwanda cha Pepsi,kiwanda cha kahawa, n.k Sababu zote hizo zilichangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya mkoa wetu kurudi nyuma maana vijana wengi walikosa ajira sambamba na kukosekana mapato ya kutosha,kodi na ushuru wa kuiendesha Manispaa ya Mji wa Bukoba,hivyo ikabaki kuwa tegemezi ya ruzuku toka serikali kuu ili iweze kujiendesha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…