TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Kigamboni

Hii barabara ya mwasonga kibada kimbiji ni kibwa sana. Inahitaji ijengwe kwa lami ili ifungue fursa.
 
Pia ningeomba uanzishe thread maalum ya wanakigamboni ikielezea maendeleo ya kigamboni.
 
Kama unasikia maajabu ndiyo haya!

Daraja la kigamboni lililojengwa Kwa mabilioni ya Pesa! Daraja lililojengwa Kwa Nondo za kuagiza toka nje, daraja ambalo huvuki mpaka ulipie!

Maungo ya barabara yake baada ya daraja ni mabovu haijawahi tokea! Barabara ina mashimo na madimbwi kiasi kwamba hata kutembea Kwa miguu haifai!

Nimetoka kigamboni sahivi na kikirikuu changu shock-up zote hazifai;
Ni mambo ya ajabu sana sehemu ambapo ni uso Wa nchi kama daraja ni panakuwa pabovu namna hiyo kama vile nchi haina viongozi!

Inamaana wameshindwa hata kutia mafta greda likasawazisha watu wapite? Kutwa kukusanya road license za magari lakini barabara ni mbovu! Mbovu, mbovu kila mahali!

Sijui nini cha kujivunia Tanzania, kila mahali kero tupuuu!
(HATA UWANJA WA TAIFA MVUA IKINYESHA MTU ALIYEKAA V.I.P ANANYESHEWA NA MVUA)

Njia zoote kuanzia mitaa hadi njia kuu kuna mashimo tupu ! Sijui serikali iko wapi!
" haya ndiyo matokeo ya kuongozwa na watu wanaojuwa kusoma na kuandika"

Mmenitia hasara ya kununua tena shock-up ovyo kabisa nyie watu!
 
Ukiwa kwenye daladala za Kigambo - (M/Complex) Soko la Ilala ndiyo hatari hasa.
 
Hilo eneo kama una Gari LA chini wala usipite.. In aibu sana aisee, ndio maana foleni ya Magari imerudi feri! Kieneo cha km moja kimewashinda na hela wanakusanya kila siku? Nchi ina maudhi sana hii.. Kodi tunalipa ila huduma hovyo kabisa
 
Zito Kabwe kaiba hela zote kaenda kujengea Mavilla yake!
 
Daraja la Kigamboni litaleta madhara makubwa sana it's just the matter of time tutaishia kulia kwa kuwapoteza ndugu zetu. Daraja limeelemea upande mmoja . Kwa ufupi 'Lililipuliwa'
We una masiala wewe... Nimepita apo Leo ndani ya basi to and from machinga complex... icho unachokisema ni ulongo sana japo sijachunguza ila I don't think ukweli wa observation yako. Wewe ni muongo pia mulongo
 
Daraja la Kigamboni litaleta madhara makubwa sana it's just the matter of time tutaishia kulia kwa kuwapoteza ndugu zetu. Daraja limeelemea upande mmoja . Kwa ufupi 'Lililipuliwa'

Usitutie kihoro cha roho we mzushi.. Dahh.. Tena shika adabu yako. Wewe ni zaidi ya sheikh Yahaya
 
Usitutie kihoro cha roho we mzushi.. Dahh.. Tena shika adabu yako. Wewe ni zaidi ya sheikh Yahaya
Matusi ya nini Mkuu?! Nina haki ya kuchangia kile naamini au kile nimeona. Ubarikiwe kwa matusi yako!
 
Pole sana ! Ni PM nikuuzie shokapu Kwa bei poa Mdau! Kufa kufaana! Zipo Mpya na used
 
Hilo eneo kama una Gari LA chini wala usipite.. In aibu sana aisee, ndio maana foleni ya Magari imerudi feri! Kieneo cha km moja kimewashinda na hela wanakusanya kila siku? Nchi ina maudhi sana hii.. Kodi tunalipa ila huduma hovyo kabisa
Unadhani ndege zitanunuliwa na nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…