Mjamzito afariki kwa kukosa pesa ya mafuta gari la wagonjwa, wakati Mama ananunua magoli

Mjamzito afariki kwa kukosa pesa ya mafuta gari la wagonjwa, wakati Mama ananunua magoli

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2020
Posts
4,548
Reaction score
11,901
Wakati anaupiga mwingi, kwa kununua magoli ya Yanga na Simba kuna watu wana safa sana kwa huduma za afya. Kule Kilosa Mama kafariki kwa kukosa pesa za mafuta ya Gari ya kubebea wagonjwa.

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro, Shaka Hamdu Shaka ametoa siku tatu vyombo vya usalama kuchunguza tukio la mama mjamzito aliyefariki baada ya familia yake kukosa pesa za kuweka mafuta gari la wagonjwa.

Shaka alipokea tuhuma hizo kutoka kwa mume wa marehemu, Seleman Makuani wakati akisikiliza kero za wananchi katika Kata na Kijiji cha Kidodi, mkoani humo.
FB_IMG_1726141231016.jpg

Hii hakuna anaye jali kabisa.
Screenshot_20240912_144038_com.facebook.katana.jpg
 
Attachments

  • Screenshot_20240912_144038_com.facebook.katana.jpg
    Screenshot_20240912_144038_com.facebook.katana.jpg
    741.7 KB · Views: 7
Ila ujauzito ni mchakato maandalizi ya kujifungua ni muhimu sana hasa kwa wanaume tusiishie kutia mimba tu tuwajibike unakuta jitu linatia mimba tu Kila baada ya miaka miwili hospital akiambiwa achangie japo dawa na vipimo anakuambia Sina pesa inasikitisha sana.

Kuna jamaa mmoja limeoa binti wa watu akampa mimba ikalelewa hivyo hivyo kimagumashi mpaka ikatimiza miez 9 ikatakiwa 350000 ya operation na huduma nyingine bahati nzuri wale ma Dr wa Hospital ya Mwanyamala waliweka mbele ubinadamu wakamzalisha salama yule binti ila wakasema hatoki mpaka pesa ilipwe jamaa anaambiwa na baba Mkwe wake Lete pesa japo kidgo anasema Hana hata Senti yule binti alizuiliwa hospital karibu week 2 ndio baba Mkwe akaingia mfukoni kwake na kutoa 350000 kwa minajiri kwamba Mkwe atamrudushia mpaka Leo mtoto ana miez 11 na pesa jamaa hajamlipa baba Mkwe wake sasa hii sio sawa.
 
Hatuwezi kulaumu serikali kwa kila kosa linalofanywa na watu huku chini!,sio kwamba hawakuweza kumuwahisha hospital huyo mama mambo mengine sie wananchi wenyewe hatuna uwajibikaji huyo dereva alishindwa nini kuwasaidia mafuta ya 180000! hata nauli mwanza dar haifiki hiyo hii ni rushwa sasa!..
huo si uzembe wa rais ni uwajibikaji wa dereva ama hiyo sehemu anayofanyia kazi,mwananchi hawezi kulipia pesa yote hiyo et mafuta huo ni uzandiki!.

watanzania tubadilike kwanini tutumie shida za mwengine kama sehemu yakupatia fedha,kwani kila mtu akifanya wajibu wake nini kitaharibika!!.
uchunguzi ufanyike na wanaotakiwa kuwajibishwa wawajibishwe hatuwezi kulea huu upuuzi kiasi hichi,hizi ni tamaa za watu binafsi!.
 
Ila ujauzito ni mchakato maandalizi ya kujifungua ni muhimu sana hasa kwa wanaume tusiishie kutia mimba tu tuwajibike unakuta jiti linatia mimba Kila baada ya miaka miwili hospital akiambiwa achangie japo dawa na vipimo anakuambia Sina pesa inasikitisha sana.
kwenye hili nitamtetea jamaa hata kama kujipanga ndio lkn 180000 hiyo nauli hata dar mwanza ni kubwa! hapa kuna namna ambulance imepewa wapigaji kuna upuuzi umefanyika kwa maksudi hapa!.
 
Hatuwezi kulaumu serikali kwa kila kosa linalofanywa na watu huku chini!,sio kwamba hawakuweza kumuwahisha hospital huyo mama mambo mengine sie wananchi wenyewe hatuna uwajibikaji huyo dereva alishindwa nini kuwasaidia mafuta ya 180000! hata nauli mwanza dar haifiki hiyo hii ni rushwa sasa!..
huo si uzembe wa rais ni uwajibikaji wa dereva ama hiyo sehemu anayofanyia kazi,mwananchi hawezi kulipia pesa yote hiyo et mafuta huo ni uzandiki!.

watanzania tubadilike kwanini tutumie shida za mwengine kama sehemu yakupatia fedha,kwani kila mtu akifanya wajibu wake nini kitaharibika!!.
uchunguzi ufanyike na wanaotakiwa kuwajibishwa wawajibishwe hatuwezi kulea huu upuuzi kiasi hichi,hizi ni tamaa za watu binafsi!.
watu wanaokamata na kuzishikilia maiti washindwe kuzuia ambulance acha mahaba na serikali
 
Wizara ya afya iangalie uwezekano wa kupunguza gharama za Ambulance!!
Route za ndani ya mji 60000,Moro-Dar 230000
Inatakiwa ilipwe yote ndo mgonjwa aondoke! Ni watanzania wangapi wanamudu?
Au basi ingewekwa kwenye Bill ya mgonjwa,yaani asafirishwe ndugu wakiwa wanatafuta pesa!
 
Ambulance inaokoa Maisha ilitakiwa iwe BURE kwa Watanzania, kweni hizi Kodi tunalipa za nini?!
 
Back
Top Bottom