Hatuwezi kulaumu serikali kwa kila kosa linalofanywa na watu huku chini!,sio kwamba hawakuweza kumuwahisha hospital huyo mama mambo mengine sie wananchi wenyewe hatuna uwajibikaji huyo dereva alishindwa nini kuwasaidia mafuta ya 180000! hata nauli mwanza dar haifiki hiyo hii ni rushwa sasa!..
huo si uzembe wa rais ni uwajibikaji wa dereva ama hiyo sehemu anayofanyia kazi,mwananchi hawezi kulipia pesa yote hiyo et mafuta huo ni uzandiki!.
watanzania tubadilike kwanini tutumie shida za mwengine kama sehemu yakupatia fedha,kwani kila mtu akifanya wajibu wake nini kitaharibika!!.
uchunguzi ufanyike na wanaotakiwa kuwajibishwa wawajibishwe hatuwezi kulea huu upuuzi kiasi hichi,hizi ni tamaa za watu binafsi!.