Mjane wa Mrema atoswa, familia yapinga wosia uliachwa na Mrema. Mjane apokonywa nyumba ya Salasala

Mjane wa Mrema atoswa, familia yapinga wosia uliachwa na Mrema. Mjane apokonywa nyumba ya Salasala

Kuoa uzeeni ni kuleta migogoro kwenye familia
Tunaoa uzeeni sababu ya kutafuta matunzo, kuna baadhi ya mambo watoto hata kama wanakupenda vipi hawawezi kuyafanya...kwa mfano mwanao wa kike kukuogesha, kukuvalisha nguo nk

Lakini pic kali inakusaidia vyote na unakufa huku ukitabasamu... cha muhimu tu uwe na cha kumwachia ukishasepa.
 
Ndio kazi ya Kubenea siku zote. Ni binhwa Sana kwenye kudraft UDAKU hasa kwenye SIASA
Cheki picha za Moshi Kilimanjaro weweee
DSC_4910-640x430.jpg
DSC_4916-640x430.jpg
 
Raia Mwema limekuwa Gazeti la Udaku? Mbona Kuna Mambo Mengi Muhimu sana ya Kuandika, na Sio Udaku wa Mke wa Mrema???
Unaoita udaku wa mke wa mrema unaakisi jamii,Kuna kesi nyingi za nanna hiyo,Kama jamii tunaliepukaje kwa kuweka Sheria ya haki na rahisi
 
tunaoa uzeeni sababu ya kutafuta matunzo, kuna baadhi ya mambo watoto hata kama wanakupenda vipi hawawezi kuyafanya...kwa mfano mwanao wa kike kukuogesha, kukuvalisha nguo nk

Lakini pic kali inakusaidia vyote na unakufa huku ukitabasamu... cha muhimu tu uwe na cha kumwachia ukishasepa.
Sasa muwe mnasolve ishu za wosia mapema kabla ya kufa
 
Haya mambo sasa yamekuwa kama maigizo
Wahusika wa pande zote haya mambo ya mirathi tokea mwanzo ina maana hawashirikishan kila mtu ajue nafasi yake kuepuka aibu hizi za kila siku
 
Kina Dada mchukue somo kwa haya yanayotokea, Kwa Marehemu Mengi na Mrema na wengine.

Kabla hamjaingia makubaliano na Mzee aweke wazi unapata nini na afanye huo mpango mapema na uhakikishe ya kuwa hakuna Mgogoro kabla ya kusaini cheti cha ndoa...kwa mfano kama ni kiwanja mkanunue cha kwenu kisajiliwe kwa jina lako kabisa.

Ila nanyi kina Dada muwe Waungwana kwa mali ambazo zina mkono wa Mke aliyetangulia, usikubali kumdhulumu Mwanamke mwenzako.
 
Upo sahihi lakini inategemea na aina ya ndoa iliyofungwa. Kama ni customary marriage hawezi kurithi.

Pia sheria ya mirathi inaangalia wanandoa waliishi maisha gani kipindi cha uhai wake/wao. Mfano kama waliishi kimila mali itagawanywa kulingana na sheria za mila.

Vivyo hivyo kama waliishi katika imani za dini mfano kiislamu basi itatumika Islamic law kwenye suala la mirathi.
Mahakama hata kama mlioana bila ndoa na mkaishi angalau miaka 3 inamtambua mke kuwa ni mke halali, na linapotokea suala lolote iwe mirathi au Talaka anakuwa na haki ya mgao wa mali!

Hivyo nina hakika suala hili la mjane wa Mrema na familia likifika mahakamani mwanadada huyo hatatoka mikono mitupu!
 
Imekuwa trend sasa ya hawa mabinti watafutaji kuolewa na watu wenye ushawishi kijamii hasa kiuchumi na kimadaraka ama mamlaka kwa lengo la kuchuma mali za hawa watu walizozihangaikia kwa miaka mingi, mfano ni kama huyu ama klyinn mengi acha yawakute yanayowakuta.

Huwezi kunukia kwa urahisi hivyo kisa tu umekaa karibu na uwaridi. Ajifunze toka kwa mwenzake jackline mengi yaliyomkuta
 
Ukifika miaka 70, kisheria kuna baadhi ya maamuzi yako yanaweza kupingwa mahakamani either ukiwa bado hai ama mfu sababu kuu ni kwamba afya ya akili inakuwa ishaanza kuzorota katika umri huo.
Yes, maamuzi yako yanaweza kupingwa iwapo yanakiuka haki na sheria! Lakini haki ya mtu kufanya maamuzi yoyote haiangalii umri ispokuwa maamuzi yasikiuke haki na mfano.

Mfano Ukaandika wosia ambao unabagua watoto wa kurithi mali zako ilihali ni wanao wa kuwazaa mwenyewe! Lakini kwa suala la kuamua kuo baba ana haki ya kufanya uamuzi nalo bila kuingiliwa na mtu yeyote hasa ukizingatia hakuwa na mke!
 
Mimi nadhani sheria zibadilike ili kuangalia ''hali halisi''. Nakwazika kukubali mwanbiamke anayeolewa na mtu mgonjwa na mzee kama alivyokuwa Mrema, na wakaishi kwa muda mfupi kabisa na hana mtoto yeyote eti anastahili kurithi mali ya marehemu.
bi mkubwa anataka nyumba na Prodo la Mzee !! yaho mengine ya kwenu.
 
Back
Top Bottom