Mjue Jini Mahaba: Fahamu mengi kuhusu jini mahaba

Si uWeka wewe hizo habari za kweli unazozijua wewe kuliko kuja kubwabwaja hapa? Punguone wahead ww


Wenzako kwanza hutoa challenge na mtu anaposhindwa ndipo hutoa hayo matusi yako unayayatoa kutoka kwenye domo lako kubwa kama tundu la choo cha stendi ya mabasi, kila abiria akisikia haja huja kujisaidia humo. Swine mkubwa weee.

Nimekuambia nimeshindwa kupinga huo uongo wenu kwa hoja??, Hata bila hoja yoyote tayari zilisha jipinga zenyewe, eti jini linafanana na mtu???, umeona wapi??, unajua maana ya neno jinn??, (اجن).
 
Sisi tunapazia tumefungiwa na mwenyzi Mungu ila kwa baadhi yetu aliyetupa elimu tunaweza kufungua na kuwaona sasa kuhusu dimension ile uliyopo wewe ndio na wao wapo hiyo hiyo pia wao na binaadamu ni hali moja wapo great thinker na wapo losers pia, different between us and them are only shapes and other small things but not that much
 
Nasema tena na tena, jinsi ulivyoelezea hiyo habari juu ya majinni, umetia chumvi kibao kiasi kwamba habari yote inakuwa ni uongo.

Na hizo picha ulizoweka ndiyo kabisaa zinashadidia uongo wako.
Asante kwa kuchangia na karibu kwenye thread zingine mkuu,
 
الجن مخلوقات غير مرئية لا يمكن رؤيتها بأعين طبيعية ، لكي تراها يجب أن يكون لديك المعرفة
you don't need to panic so that we can see your point mkuu, be cool son mbona humu utaeleweka tu cha mno wewe ni kuuliza pale ambapo huelewi kwani picha ndio zimekukera sana au kuna kingine! kama hujaelewa uliza na kama unahoja toa acha fujo
 


Mkuu, huyo mwenzako aliyenitusi kabla ya mimi kumjibu hukuona matusi yake au yeye hakustahili kupewa hizo nasaha unazonipa??--- yeye kaanza kunitusi na mimi nilikuwa najibu mapigo, juu ya yote mimi niko peace tu.

Tuje katika mada, umeandika maneno katika lugha ya kiarabu nadhani ni watu wachache sana humu ndani wanaojua lugha ya kiarabu na hata kama wapo sio fasaha sana katika lugha hiyo kama waiivyokuwa fasaha katika Kiswahili na kiingereza, hivyo ni vyema unapoona "raha" kuandika kwa kiarabu basi pembeni weka tafsiri yake kwa kiswahili ili wengi wetu tusiojua vyema kiarabu tupate kufahamu.

Tarjama ya maneno yako ya kiarabu ni kama ifuatavyo (nakubali kurekebishwa nitakapo kosea);-

" Majini ni viumbe, mbali na kujibadili, haiwezekani kuonekana kwa macho ya kawaida ili kuwaona lazima uwe na maarifa".


Katika hadithi fulani za mtukufu mtume Muhammad (saw, aliwakataza masahaba zake kutumia mifupa na vinyesi vikavu vya ngamia kuchambia na akasema mifupa na vinyesi hivyo ni vyakula vya majini, na pia akatufundisha tuingiapo vyooni tusome dua ili kujikinga na majini waliomo vyooni.

Elimu ya kisayansi inatuambia kwamba katika mifupa na vinyesi vya wanyama kuna bakteria kibao ambao kama utatumia hivyo vinyesi na mifupa kuchambia utakuwa na nafasi kubwa sana ya kupata maambukizi katika njia ya haja kubwa halikadhalika chooni kulingana na mazingira yake kuna aina mbalimbali za bakteria wa maradhi mfano, Chorela, dysentery, hepatitis, kisonono nk, (hasa vyoo vya umma).

Hivyo mtukufu mtume (saw), aliposema neno "jinn" alikuwa na maana ya wadudu wadogo wasioweza kuonekana kwa macho ya kawaida na hapa nakubaliana na maneno yako ya kiarabu, na ili uweze kuwaona ni lazima utumie nyenzo maalumu kama darubini (microscope) au kwa maneno mengine uwe na maarifa (معرفة) kama ulivyosema.

Sifa kuu ya jinn ni kutokuonekana kirahisi kwa macho ya kawaida na mzizi wa neno "jinn" ni neno "janna" ambalo maana yake ni kutokuonekana, hivyo basi katika lugha ya kiarabu, kitu chochote au tukio lolote lenye sifa ya kutokuonekana kirahisi linawezwa kwa ki-SIFA likaitwa kwa jina la "jinn", na hii ipo karibu katika lugha zote hata katika kiswahili mtu shujaa anaweza kuitwa "Simba" kwa sababu tu ya ushujaa wake.

Kwa muktadha huo ki-sifa , jinn anaweza kuwa mtu mkubwa, kiongozi, tajiri, mtu mashuhuri nk--- ambao kwa hizo sifa zao kuonekana kwao mbele za watu huwa ni kwa nadra sana na inapotokea akaonekana basi lazima kuwae na jambo muhimu, na hapa ndipo Allah katika Qur'an aliposema; "Sikuwaumba majini na watu isipokuwa watuabudu"-- Majini waliotajwa hapa ni viongozi, watu mashuhuri, matajiri nk, ambao kwa umashuhuri na utajiri na uongozi wao wanaweza kujawa na kiburi kujiona kwamba wao hawastahili kufanya ibada, Watu katika aya hiyo ni watu wa kawaida wasiokuwa na utajiri, umashuhuri, uongozi nk ambao nao kulingana na hali zao za kimaisha wanaweza kusema ibada haiwahusu ila inawahusu hao waheshimiwa wakubwa (majini), ndipo Allah akakata mzuzi wa fitna akasema wote lazima tumuabudu hakuna adhuru.

Allah katika Qur'an anasema "Na majinni tumewaumba mwanzo kwa mwale wa moto," (sikumbuki aya). sayansi ambayo ni elimu kutoka kwa huyohuyo Allah inasema kwamba viumbe wa mwanzo kabisa kuumbwa walikuwa ni bakteria ainavya (Eukaryotes na prykaryotes. Check spelling) ambao waliumbwa kutokana na nuru ya radi (lightining sparks).

Qur'an katika Surah jinn, Majinn waliposikia Qur'an ikisomwa walisema, "hakika tumesikia Qur'an ya ajabu inayoongoza kwenye uongofu"(sikumbuki aya) na tena wakasema; "hakika tumesikia kitabu kilichoteremshwa baada ya Musa"(sikumbuki aya), na baadaye mtume (saw) alikuwa akifanya maombi na hao majinn "wakamzonga/ wakamzingira" (sikumbuki aya). Majinn waliotajwa katika hiyo sura ni watu wageni wasiokuwa waarabu, katika lugha ya kiarabu neno "jinn" linaruhusiwa kutumika kwa mgeni/wageni kwa sababu mgeni anaonekana kipindi tu anapokuwa na wenyeji lakini yeye sio mtu wa hapo na hivyo kuonekana kwake ni kama kuonekana kwa "jinn" na hii ni katika matumizi yale yale ya Ki- sifa ya neno jinn--, na hao wageni walikuwa ni mayahudi kutoka Nasibin, ndiyo maana wakasema; "innaa sami'i'naa kitaaba unzila min baa'd Musa" (Hakika tumesikia kitabu kilichoteremshwa baada ya Musa).


Ugonjwa unaowashika kina mama na akina dada, (Hysteria), kama nilivyosema hapo awali kuwa neno "jinn" linaweza kutumika hata kwa jambo lenye sababu isiyoonekana bali athari inayoonekana (unseen cause but seen effects). Akina mama maranyingi husumbuliwa na ugonjwa wa akili ambao watu wengi huuita mapepo, majinni na hata Maruhani, mtu anayeshikwa na ugonjwa huo kutokana na sababu mbalimbali za ndani ya mwili na nje ya mwili anashindwa kabisa kujidhibiti (uncontroll) kiakili na hivyo wakati huo akili inajiendesha yenyewe (run amok), na mgonjwa anaweza kutamka maneno au hisia alizokuwa nazo kichwani kabla ya kushikwa na huo ugonjwa (ravings) au anaweza kutamka maneno katika lugha ngeni kabisa (labda aliisikia zamani alipokuwa mdogo kwani akili ni kama memory card), na watu wakashangaa na wakaanza kuhisi kwamba; "LAZIMA KUNA KIUMBE KISICHOONEKANA KWA MACHO KUTOKA NJE KIMEMUINGIA KICHWANI NDICHO KINACHOZUNGUMZA HIYO LUGHA"😁😁---- na hapo ndipo dhana na fikra za upotishaji juu ya majinn zinapoanzia hapo, kwamba majinni ni viumbe mithili ya watu na wanaweza kumuingia mtu kichwani na wanapenda kuishi chooni, kwenye milima mirefu, magogu, baharini, katika misitu minene nk, ilmradi kila mtu anatoa fikra zake anazojenga juu ya majinni, mbaya zaidi Waalimu na Masheikh Ubwabwa biashara ya kupunga majinn kwa akina mama imekuwa ni dili kubwa na Wachungaji pia hawako nyuma katika kukemea majini mapepo. Kifupi, hayo yanayoitwa mapepo, Maruhani, jinn, Mahaba nk, yanaweza kuitwa kwa jina la "jinn" kwa sifa tu kwasababu kitu kinachosababisha mama au dada ashikwe na hali ya kuweweseka haionekani kwa macho lakini madhara yake yanaonekana kwa mgonjwa, hakuna jinn mahaba, Subiani, Affrit nk, mwenye umbo la mtu kutoka nje anayemuingia mtu, hakuna, never ever there is none.

Kutupiwa "jinn"--- unaweza kusikia watu wakisema, mfano; " Jamaa katupiwa "jinn" ndiyo maana kapata ajali, naam-- zipo elimu za "spirits", mfano, Telepathy, Hynotism (mesmerism) nk, ni elimu ambazo baadhi ya watu wanazaliwa nazo naturally au kwa kujifunza, ni elimu ambayo mtu anaweza kumuathiri mtu mwingine kwa kufanya baadhi ya mambo fulani na mtu akaathirika hata akiwa maelfu ya kilometres na mtu akaathirika huko alipo, nalo jambo hili waweza kuliita "jinn" kwasababu tu nguvu inayotenda kazi haionekani kwa macho, lakini si kwamba kuna kiumbe mfano wa mtu au watu kinaruka hewani baada ya kutumwa na "fundi" kwenda kufanya madhara kwa mlengwa.

Majini kuumbwa kwa moto, naomba nimalizie kwa kutoa ufafanuzi wa maana nyingine ya jinn kuumbwa kwa moto, mtu au kitu kuumbwa kwa moto maana yake pia yaweza kuwa ni mtu mwenye kiburi, majivuno, mwenye asili ya ukali nk, kama alivyokuwa Firauni na Ibilisi katika Qur'an.
 
Nisamehe mkuu. Nilikukosea
 
Haya! Tutajie kitabu cha mwana wa zuoni gani wa Kiislam ambaye ametafsiri Qur'ani kama wewe ulivyotafsiri na utuwekee namba ya kurasa ya hiyo Tafsiri.
 
Yupi kati bin adam na jin anakiwa powerfull zaid ya mwenzake endapo individual akifika kwenye maximum spiritual and quantum mind set?

Pia naomba maelezo kuhusu pazia linalotufanya tusiwaonee? Ila nadhan wao wanatuona sio
 
Kwa tafsiri yako ya neno Jinni, tuambie hizi baadhi za aya ina maana gani?

(وَإِذۡ قُلۡنَا لِلۡمَلَـٰۤىِٕكَةِ ٱسۡجُدُوا۟ لِـَٔادَمَ فَسَجَدُوۤا۟ إِلَّاۤ إِبۡلِیسَ كَانَ مِنَ ٱلۡجِنِّ فَفَسَقَ عَنۡ أَمۡرِ رَبِّهِۦۤۗ أَفَتَتَّخِذُونَهُۥ وَذُرِّیَّتَهُۥۤ أَوۡلِیَاۤءَ مِن دُونِی وَهُمۡ لَكُمۡ عَدُوُّۢۚ بِئۡسَ لِلظَّـٰلِمِینَ بَدَلࣰا)
[Surat Al-Kahf 50]


(بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِیمِ

قُلۡ أُوحِیَ إِلَیَّ أَنَّهُ ٱسۡتَمَعَ نَفَرࣱ مِّنَ ٱلۡجِنِّ فَقَالُوۤا۟ إِنَّا سَمِعۡنَا قُرۡءَانًا عَجَبࣰا ۝ یَهۡدِیۤ إِلَى ٱلرُّشۡدِ فَـَٔامَنَّا بِهِۦۖ وَلَن نُّشۡرِكَ بِرَبِّنَاۤ أَحَدࣰا ۝ وَأَنَّهُۥ تَعَـٰلَىٰ جَدُّ رَبِّنَا مَا ٱتَّخَذَ صَـٰحِبَةࣰ وَلَا وَلَدࣰا ۝ وَأَنَّهُۥ كَانَ یَقُولُ سَفِیهُنَا عَلَى ٱللَّهِ شَطَطࣰا ۝ وَأَنَّا ظَنَنَّاۤ أَن لَّن تَقُولَ ٱلۡإِنسُ وَٱلۡجِنُّ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبࣰا ۝ وَأَنَّهُۥ كَانَ رِجَالࣱ مِّنَ ٱلۡإِنسِ یَعُوذُونَ بِرِجَالࣲ مِّنَ ٱلۡجِنِّ فَزَادُوهُمۡ رَهَقࣰا ۝ وَأَنَّهُمۡ ظَنُّوا۟ كَمَا ظَنَنتُمۡ أَن لَّن یَبۡعَثَ ٱللَّهُ أَحَدࣰا ۝ وَأَنَّا لَمَسۡنَا ٱلسَّمَاۤءَ فَوَجَدۡنَـٰهَا مُلِئَتۡ حَرَسࣰا شَدِیدࣰا وَشُهُبࣰا ۝ وَأَنَّا كُنَّا نَقۡعُدُ مِنۡهَا مَقَـٰعِدَ لِلسَّمۡعِۖ فَمَن یَسۡتَمِعِ ٱلۡـَٔانَ یَجِدۡ لَهُۥ شِهَابࣰا رَّصَدࣰا ۝ وَأَنَّا لَا نَدۡرِیۤ أَشَرٌّ أُرِیدَ بِمَن فِی ٱلۡأَرۡضِ أَمۡ أَرَادَ بِهِمۡ رَبُّهُمۡ رَشَدࣰا ۝ وَأَنَّا مِنَّا ٱلصَّـٰلِحُونَ وَمِنَّا دُونَ ذَ ٰ⁠لِكَۖ كُنَّا طَرَاۤىِٕقَ قِدَدࣰا ۝ وَأَنَّا ظَنَنَّاۤ أَن لَّن نُّعۡجِزَ ٱللَّهَ فِی ٱلۡأَرۡضِ وَلَن نُّعۡجِزَهُۥ هَرَبࣰا ۝ وَأَنَّا لَمَّا سَمِعۡنَا ٱلۡهُدَىٰۤ ءَامَنَّا بِهِۦۖ فَمَن یُؤۡمِنۢ بِرَبِّهِۦ فَلَا یَخَافُ بَخۡسࣰا وَلَا رَهَقࣰا ۝ وَأَنَّا مِنَّا ٱلۡمُسۡلِمُونَ وَمِنَّا ٱلۡقَـٰسِطُونَۖ فَمَنۡ أَسۡلَمَ فَأُو۟لَـٰۤىِٕكَ تَحَرَّوۡا۟ رَشَدࣰا)
[Surat Al-Jinn 1 - 14]


(یَـٰمَعۡشَرَ ٱلۡجِنِّ وَٱلۡإِنسِ إِنِ ٱسۡتَطَعۡتُمۡ أَن تَنفُذُوا۟ مِنۡ أَقۡطَارِ ٱلسَّمَـٰوَ ٰ⁠تِ وَٱلۡأَرۡضِ فَٱنفُذُوا۟ۚ لَا تَنفُذُونَ إِلَّا بِسُلۡطَـٰنࣲ)
[Surat Ar-Rahman 33]
 
Hakufukuzae hakwambii toka
 
Kwahyo jinni ni kiumbe kisichoonekana kwa macho Bali kwa wenye uwezo wa kuona kwa vifaa maalumu.
Kwahyo huyu jini anaesemekana ni mahaba kwa maelezo yako hayupo je ni kitu gani kinapelekea mtu kuota umefunga ndoa na mwanamke/mume, kuota unafanya mapenzi ilihali kuwa haukuwa na mawazo hayo wala haukuuandaa ubongo kureverse kitu ulichofanya (kufikiria kufanya mapenzi)
Mana nilikuwa na kademu fulani yeye kila siku alikuwa anaota hzo ndoto za kugegedwa ilihali tulikuwa tunakutana (sex) hadi ilifika kipindi alikuwa hata akilala mchana hali ile inatokea.
Sasa je hao ndio backeria uliokuwa unasema wanaitwa majinn??
Nawasilisha....
 
Hakufukuzae hakwambii toka
Kama suala huelewi ni vyema kuuliza, hupungukiwi na kitu. Huyo jamaa kachukua ukweli kwa kuuhalalisha uongo.

Rafiki yako Mokaze amezua uongo ameandika usuli wa neno Jinni ni neno Jannah. Kisha akapandikiza uongo wake kwenye definition iliyo sahihi kwa kupandikizia uongo. Yafaa tumsahihishe.

Kila kisichoonekana kwa macho lugha ya Kiarabu hutohoa herufi mbili kwenye lugha yake na huzaliwa neno. Herufi hizi ni Jiim na Nuun. Pepo(peponi) hatujawahi kuiona kwa macho zaidi ya simulizi zake, kwa Kiarabu inaitwa Jannah. Jannah ina herufi 3. Kuna Jiim, kuna Nuun na Tee. Ukiangalia unaona Jiim na Nun ipo.

Aliyerukwa na akili kwa kiarabu anaitwa Majinuun. Neno Majinuun limeundwa kwa herufi 3. Kuna herufi Miim, herufi Jiim na herufi Nuun. Jiim na Nuun hutoholewa kwa kitu kisichoonekana, akili ama kurukwa na akili hakuonekaniki bali ni ishara ya vitendo vitakavyofanywa. Herufi Jiim na Nuun ipo hapo.

Elimu ya uzazi kwa lugha ya Kiarabu inaitwa Ilmul Ajinna. Ukiliangalia neno ajinna utaona limeundwa na Alif, kuna Jiim na Nuun. Kwa nini Jiim na Nuun ipo? Tunarudi kwenye mising asili ya lugha ya Kiarabu inayosema: Itakapotoholewa Jiim na Nuun kwenye neno ufahamu ya kwamba asili ya hicho kitu hakionekani kwa macho ya mwanadamu.

Halikadhalika na Al ilmul Ajinna(elimu ya uzazi) kwa sababu kilichopo tumboni mwa mwanamke(mimba/kiumbe) hakionekani kwa macho bali kwa vipimo. Na Jinni kwa Kiarabu ameitwa hivyo kwa sababu haonekani kwa macho ya binadamu. Neno Jinni lina herufi ya Jiim na Nuun.

Hiyo ya juu ni baadhi ya mifano.

Kanuni inayokuja hapa ni kwamba: Jicho la mwanadamu kisichokiona kwa dhati yake kwa Lugha ya Kiarabu ni lazima hizo herufi 2 zitakuwepo, nazo ni Jiim na Nuun. Na wala si kwa sifa yake, kwa maana: Si kile kilichokuwa nadra mwachoni mwa binadamu kinakuwa na sifa ya Jini. Na ni nini maana ya nadra? Nadra ni kisichoonekana au kutopatikana mara kwa mara au kwa urahisi. Na hali ya kutoonekana mara kwa mara ama kutokupatikana kwa urahisi kwa lugha ya Kiarabu kunaitwa NUQSU au IHTIYAAJU.

Mokaze anasema tukio lolote au jambo lisiloonekana kirahisi linaweza kwa ki-sifa kwa kuitwa Jinni. Kwa vile neno Jinni amelifafanua kwa kutoa maana kwenye lugha ya Kiarabu yafaa atupatie uthibitisho kwenye lugha ya Kiarabu kwamba mtu asipoonekana machoni mwa watu kwa maana kuonekana kwake si rahisi( na muktadha uliyotumika hapa si kwamba mtu haonekani. Bali imetumika balagha kwamba ni nadra kuonekana machoni mwa watu ijapokuwa ni mwenye kuonekana machoni mwa watu) kisifa naye neno Jinni linamfaa. Atuthibitishie hicho alichokiandika kwa kutumia kutumia misingi ya lugha ya Kiarabu.

Mashaallah akanukuu hadithi ya Mtume akiwaambia maswahaba wake wasitumie mifupa kujiondolea najisi kwani ni vyakula vya Majinni. Kisha akafafanua kwa tanbihi kuwa Mtume aliposema neno Jinni alikuwa na maana ya wadudu. Akanukuu na aya inayosema "Sikuumba majinni na watu isipokuwa waniabudu." Kisha akanukuu na aya inayosema na "Majinni tumewaumba mwanzo kwa mwale wa moto."

Kwa vile Mokaze anasema aya (ya kwanza niliyomkoti) neno Jinni Mungu anamaanisha ni watu wasiyoonekana sana machoni mwa jamii. Aya ya pili akasema neno Jinni ni
bakteria aina ya Eukaryotes na prykaryotes.
Tusiandikie mate wakati wino ungalipo! Wanawazuoni wa Kiislam wanafahamika na vitabu vinafahamika na mabeberu wa tafsiri ya Quran wanafahamika.

Sasa atupatie ushahidi wa hicho alichoandika yeye kwamba majinni kwenye Quran ina maana kama aliyotoa yeye. Asiweke link ya mitandao ya kijamii. Atupatie jina la kitabu cha tafsiri ya hiyo Quran na imeandikwa na nani na mujallad wangapi. Tunasubiri maarifa yako Bw. Mokaze
 
Nakumbuka mahala ulipo jamaa,ikitokea ukaja Mwanza hapa maana upo karibu najua,ukija hapa mjini ktk mizunguko yako nichek tuonane mkuu
 
ndio mkuu hana tofauti na kuzini na mwanamke mwenye nuksi au mwanaume malaya! ni laana

Sasa na mie ambae nimekula sana malaya.. inakuwaje ? Maana toka nimeanza kula malaya wanafika 500.... sio nimeisha kabisa 🙈🙈🙈
 

La marashi jepesi kwa tusio na harufu. Sharti gumu akiniambia, niue, au nisisaidie jamii, nisile bata, au nisitee mademu hayo siyawezi kuyatimiza tutashinďwana dakika hiyo hiyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…