Mjue Jini Mahaba: Fahamu mengi kuhusu jini mahaba

Mjue Jini Mahaba: Fahamu mengi kuhusu jini mahaba

mche mungu tuu vya wanadamu wenye maarifa nao ni majini mahaba wengine au watafuta mali
 
Wewe ndugu unayo matatizo; si bure.

Mimi nimenukuu maelezo ya Kamusi maarufu ya maneno ya Kiarabu kwa kiingereza, (Arabic -english lexcon kilichotungwa na Edward William Lane na Aqrab), huyo W E lane alikuwa Muingereza mtaalamu wa mambo ya mashariki (orientalist) na huyo Aqrab alikuwa Muarabu. Ukitaka kumjua huyo vyema google.

Yeye akitoa maana ya neno "jinn" anasema :- جن (jinn) is derived from جن (janna) which means, it veiled, concealed,covered,or protected him or it. جن (jinn) means, such beings remain aloof from the people concealing themselves , STRANGERS, the main or chief part of body of mankind; etc.

Nimeliandika neno STRANGERS kwa herufi kubwa kwasababu inaeezekana macho yako ni mabovu au kama hujui maana ya hilo neno fungua kamusi.


Hayo maneno yametoka katika hiyo kamusi siyo maneno ysngu, kama unataka mkosoe hiyo anayesema جن ni "strangers".
Kaka ila mungu mwenyewe anasema kuwa Quran ni kitabu ambacho hakina shaka wala hakiitaji kukifanyia marekebisho ndio mana kwenye Quran wageni aliwaita kwa jina lao na jinn aliwaita kwa jina lao hvyo tusikosoe Quran au kutafsiri vibaya tutafute wana wa zuoni tuulize kupata majibu yaliyo sahihi
 
Kaka ila mungu mwenyewe anasema kuwa Quran ni kitabu ambacho hakina shaka wala hakiitaji kukifanyia marekebisho ndio mana kwenye Quran wageni aliwaita kwa jina lao na jinn aliwaita kwa jina lao hvyo tusikosoe Quran au kutafsiri vibaya tutafute wana wa zuoni tuulize kupata majibu yaliyo sahihi


Pia Qur'ani sio kitabu cha majini--- Subiani, Makata, nk--- wala siyo kitabu cha kupungia majinni bali ni kitabu kilicho muongozo kwa watu.
 
Huwezi kutoa hoja kwa mstari mmoja wa maneno, hapo haupo tofauti na wale wanao nukuu kipande cha aya ya Qur'an bila kumalizia, aya ile inayoanzia na maneno; "Ole wao wanaoswali--------" sasa hapo ndipo wewe umeiga.

Mimi sipingi uwepo wa majini, kwani si Qur'an ndiyo imewataja pale iliposema; "Sikuwaumba majini na watu ila waniabudu."- sasa ninapinga upotoshaji mnaofanya kuhusu hao majini waliotajwa hapo, kwa akili yenu mnataka kusema majini hao ni Subiani, makata, nk. Majini mliojitungia wenyewe.Huo ni uongo, majinni waliotajwa hapo ni watu maalum.
wewe unapingana na kitabu hicho hicho ambacho kinasema miongoni mwetu kuna vitu wachache tu ndio wamepewa sasa kama wewe hujapewa kitu endelea kuwa looser

Rakims
 
Ndoto zangu nyingi huwa nipuliza pumzia naonaga wanao taka kunishambulia huwa wananguka na wengine hata kufa... au wanakimbia.. so sijui hata ila huwa ndio ndoto zake nyingi. Sasa ivi nimeacha haya mambo
Basi kuna swala huitwa swala ya ISTIKHARA kumtaka mwenyezi Mungu ushauri na maelekezo ukisali hiyo majibu mengine unayokosa utayapata hapo!

Rakims
 
Kaka ila mungu mwenyewe anasema kuwa Quran ni kitabu ambacho hakina shaka wala hakiitaji kukifanyia marekebisho ndio mana kwenye Quran wageni aliwaita kwa jina lao na jinn aliwaita kwa jina lao hvyo tusikosoe Quran au kutafsiri vibaya tutafute wana wa zuoni tuulize kupata majibu yaliyo sahihi
Sahihi,
 
Mkuu, kwanza nilikosea (misspell) maandishi, ilitakiwa liwe "Psyche" katika muktadha nilikuwa na maana ya mawazo au jambo linalohusiana na akili na fikra za mtu.

Ghaibu ni kitu kisichoonekana au kisichojulikana, kitu ambacho kipo katika siri. Unaposema elimu ya ghaibu maana yake ni elimu ya mambo yaliyojificha, yaliyofichikana., mambo ya siri nk, (the unseen).
Too Shallow
 
Pia Qur'ani sio kitabu cha majini--- Subiani, Makata, nk--- wala siyo kitabu cha kupungia majinni bali ni kitabu kilicho muongozo kwa watu.
Wapi nimeandika Quran ni kitabu cha majini--- Subiani, Makata, nk? au cha kupungia majini? anaepunga majini hiyo ni yeye na nafsi yake na pia anaesema ni kitabu cha majini ni yeye na nafsi yake! ama kwa hapa umesema wewe basi ni wewe na nafsi yako!

Rakims
 
mche mungu tuu vya wanadamu wenye maarifa nao ni majini mahaba wengine au watafuta mali
Hii ni jamii Intelligence usisahau hilo unapoweka kitu weka kama kwamba kitaonyesha how intelligence you are!

Rakims
 
Kuhusu bazia ambalao hufanya watu wasuwaone majin. Pia yup kati ya bin adam na jin ana nguvu kuliko mwenzake endapo wote wakifikia maximun based in spirituality and quantum mind set
Fanya mark unikumbushe mkuu!
 
Kuhusu bazia ambalao hufanya watu wasuwaone majin. Pia yup kati ya bin adam na jin ana nguvu kuliko mwenzake endapo wote wakifikia maximun based in spirituality and quantum mind set
Ok kuhusu pazia lililowekwa kutokuonekana kwa macho ya mtu ya kawaida ni kwa sababu ya maumbile yao na kutokuwa na umbo moja thabiti ambalo wamepewa wengi hubadirika badirika hivyo kwa maumbile yao ya kutisha na kuogopesha ndio wakawa wamehifadhiwa wasionekane kwa macho tu ya dhahiri kwa maana dunia ingekuwa ni vurugu tu, lakini kwa wenye kutaka kuona ndio ikawepo elimu jinsi ya kuweza kuwaona, na kuhusu nguvu baina ya jini na binadamu ni sawa na kutaka kujua nguvu kuhusu binadamu na mnyama sasa hapo nguvu binadamu anazidiwa na jini isipokuwa yeye ndio mtawala wa ulimwengu huu na alijaliwa akili zaidi kuliko jini na kuna baadhi ya majini wanawazidi watu akili wasioweza kuzitumia!

Rakims
 
Habari wakuu!
Wengi miongoni mwenu huona kila ninapotoa thread huona kama vile hufundisha uchawi lakini kwa mwenye akili timamu hupata mafundisho kwa asilimia kubwa sana!
kumekuwa na tungo nyingi sana kuhusu jini mahaba na maelezo mengi sana kuhusu jini huyu lakini pia watu wengi sana wanaropoka tu bila kumjua lau kama wangemfahamu basi wangezidi kumuomba Mwenyezi Mungu awaepushe na mtihani wa kiumbe hiki

MJUE JINI MAHABA:
View attachment 1183758
Jini mahaba ni moja kati ya majini waliokuwa na nguvu sana na waliopo karibu sana na ufalme wa Dajjal/Shetani/Ibilisi/Lucifer/ ambaye pia wengine humuita mpinga christo.

Elewa ya kuwa ndugu yangu unaesoma makala hii kwamba kuna daraja tano tu za majini katika ulimwengu huu tunaoishi miongoni mwa ukubwa wa tabaka la majini ambayo yanasadikika kuwa milioni 72 elfu hii ni idadi iliyopigwa na baadhi tu ya mashetani wenyewe lakini tukizungumzia kiasiri ya majini hawa wapo katika makundi matano peke yake,
watu wamekuwa wakidanganywa sana kwa hadithi na baadhi ya tungo za viumbe hawa lakini unachotakiwa kuelewa ni kwamba idadi ya viumbe hawa kwa wingi wao anayejua ni mwenyezi Mungu peke yake na hakuna mwingine,
elewa pia ya kwamba majini hawa mtu akikwambia masubiani,masharifu,mashetani,mizimu,vibushuti,vinyamkela,mapepo,makudam,muwakili,ruhani,jini mahaba,makata,shetani,subisubi na yote yalew majina mengine unayoyajua hayo yote yapo kwenye kundi moja tu MAJINI hayana tofauti isipokuwa tu kwa mageuzi ya maumbile yao au uhasama wao yanayofanya au misaada yanayotoa ndio hupewa majina tofauti tofauti kulingana na kile yalichomfanyia au yanavyoonekana,
Sasa nikija kujaaliwa basi nitawaelezea majini ili kila atakaye kuwa anatamka jini aelewe anachosema na sio kutamka tu.

Turejee kwenye kumjua huyu tuliyemkusudia,

Maana ya Jini mahaba:
View attachment 1183766
asili ya jina hili ni jina lililotungwa tu na sisi wenyewe watanzania ili kuweza kutambulisha ni kiumbe cha namna gani tunachokuwa tumekusudia lakini kwa maelezo unatakiwa ufahamu kuwa jini huyu kazi yake na katika mambo ambayo anayafanya zaidi ni kuhakikisha zinaa inatawala na kazi zote zinazohusiana na ngono,

Baadhi ya kazi zake:
View attachment 1183767
Jini huyu hutumika kutumia watu ndoto za ngono,hutumika kuwalawiti wanaume kwa wanawake kama popo bawa hutumika pia kuwafanya au kuwashawishi wale alionao kuingilia au kuingiliwa kinyume na maumbile, kuwaingilia watu na kuwafanyia michezo ya kinyume na maumbile hutumika pia kuuwa kwa kubaka pia shetani huyu,hutumika vile vile katika kuleta ufukara, hutumika pia katika kuwafanya wazee na watu wazima kuzini na watoto wadogo na huwafanya watu wawe na ashiki kupindukia lakini pia kubwa katika mambo anayoyafanya ni kuwaondolea wahanga hisia za kimapenzi na kumfanya mwanaume asiweze kusimamia uume barabara unakuwa umelegea na pia kuwaondoshea wanawake radha ya mapenzi na wengine huwafanya kukosa kabisa hamu ya mapenzi na kuwapa mvuto kwenye jinsia inayofanana nao,

Baadhi ya watu humuita popobawa kulingana na yale aliyoyafanya na wengine humuita jini mahaba kulingana na alichofanya wengine humuita majina wanayoyajua wao lakini wazungu hawa huwaita Succubi au Succubus yaani hiyo mmoja anakuwa ni dume na mwingine ni jike.

Yote kwa yote elewa ewe ndugu yangu kuwa viumbe hawa hawana wema kwa mtu zaidi ya kuweka nae mikataba ya uhakika kwamba atashindwa na kuweza kukosea masharti kisha lile analohitaji yeye kuanza kulifanya kwa muhusika,

WALIOATHIRIWA:
View attachment 1183764
Mara nyingi walioathiriwa na kiumbe huyu huwa wanakuwa wasiri sana kwa kuhofia fedheha kwenye jamii na pia wengi kati ya wao fedheha ikizidi huanza kutumbukia katika ulevi uliopindukia au kuvuta bangi na vinginevyo ili tu kuweza kuficha aibu aliyo nayo.


UTAJIJUA VIPI KAMA KAKUKUMBA:
watu wengi mara ya kwanza anapowakumba huwafanya au kuwaingilia au kushiriki nao kinyume na maumbile na pia huwafanya wahanga kuwa ni wenye kujificha sana na aibu hii hata kutafuta msaada kwa maana humtia aibu katika sura yake kuzungumzia jambo hili na kumjaza upepo wa mawazo kuwa yeye akisema au akitaka msaada ataonekana vipi hivyo anakuwa anacheza na akili ya muhusika,

Wengi huota wakifanya mapenzi na Mama zao au baba zao hata kaka au dada au mtu yeyote unaemuheshimu kama shangazi na wengineo.

Muhanga mwingine hujikuta akipitiwa tu na usingizi basi huota mwanamke anakuja na kuanza kumlazimisha au mwanaume wafanye nae mapenzi kinyume baada ya hapo muhusika huishiwa nguvu na kukubali kufanya au kufanyiwa, wengine huona kabisa kama kivuli live kikilazimisha kumuingilia sasa pale ambapo hata sema na kuhangaika kutafuta msaada wa hili basi kiumbe yule huanza kumfanyia hayo na kumshurutisha mambo mengine yaliyokuwa machafu na kumuadhiri mbele za watu na kumfanya ajihisi kuzalaulika na kuchukiwa bila sababu na humfanya kuwa ni mtu mwenye hasira za hovyo au mtu wa kulipuka hovyo, jazba zinakuwa karibu nae kwa muda mwingi.

Muhanga mwingine huyu humkumba na kumuotesha ndoto kuwa anawekewa vidole na watu sehemu hizo za siri na kumkusanyia kundi la watu ndotoni wakionyesha kumcheka na kumdhalau,

Muhanga mwingine huyu humkumba na kumfanya live hata watu wakawa wanaona kinachoendelea bila kumuona anayefanya na kuanza kuingiwa na hofu kubwa hapa wengine hufungiwa ndani kwa kuficha fedheha nje kwa watu na asijulikane kinachofanyika ndani.

zipo aina nyingi sana za huyu shetani zilizo mbaya na za aibu kabisa wengine pia huzijua waliokwisha kukutana na wahanga au wahanga wenyewe. hizi nimeweka chache tu, zingine ni kama kutekenywa sehemu za siri na kuzikwa sehemu za maziwa bila kumuona anaefanya hivyo na wengine kuingiziwa vidole bila kuona anayefanya hivyo live.

Haya ikiwa hayajakukuta au hujaona basi usidhalau na kupuuza kwa maana siku kinakutokea usione kitu kipya au usikutwe ukiwa hujui,

TIBA YAKE:
Katika maradhi ambayo huwashinda matabibu wengi ni haya ya mashetani hawa wa mahaba kwa maana hutakiwa tabia yule kufanya mawili kati ya haya:
1: Kufunga yule jini na kwenda kumtupa mbali(au kama kafanya mtu kumpa mwenyewe mzigo wake)
2: Kumuua yule shetani kwa maana si rahisi kumtoa kwa makubaliano aondoke/ukitaka kukubaliana nae ili aondoke utakiwa kufanya atakayo amuru anaweza kukwambia ushiriki jambo lolote la kishetani ili amuondokee(hadi kuweza kuzungumza nae imeshapita kazi kubwa.

Kundi la pili la kumsadia muhanga huyu:
Utatakiwa kumpeleka katika Misikiti au Makanisani na upate mtu ambaye anahofu ya mwenyezi Mungu au mwenye imani thabiti ya kiroho ndio anaweza kumsaidia huyo mtu kwa maombi, vinginevyo sehemu zingine basi huwa ni anatoka na kurudi au kumvaa yule anayemtibu na kuanza kumshughulikia yeye na inatakiwa busara kubwa sana katika kumuuguza mtu wa hivi vinginevyo yanatoka kwake yanakukuta wewe.

SABABU ZA KUMKUMBA MTU:
Zipo sababu nyingi za haya madudu kumkumba mtu hapa nitataja chache tu kwanza:
1: Kukaa na Shahawa muda mrefu
2: Kuchezea baharini nyakati za magharibi
3: Kuingia mkataba kwa ajili ya kupata mali
4: Kujichua au kujisaga maeneo ya chooni au maliwato Maarufu kama PUNYETO, (sio BAFUNI)
5: Kulala Uchi Huku mwili ukiwa na mafuta peke yako.
6: Kulala peke yako ukiwa nusu uchi huku umeweka marashi au air freshener bila kusali
7: Kulala huku kioo kikikuangalia upo uchi
8: Kufanya ngono kinyume
9: Kuchungulia watu wakifanya mapenzi
10: Kukojoa au kumwaga shahawa Baharini/kisimani/mtoni/ndani ya mbuyu
11: Kutupiwa jini huyu anakuwa katika mfumo wa popo bawa
View attachment 1183770

MAELEZO:

Hapo katika sababu nilizoainisha za kutolea maelezo ni mbili tu zingine zinaeleweka na makala za watu wengine zilishazieleza

1: Kukaa na Shahawa muda mrefu
Elewa ya kuwa viumbe hawa hupenda sana harufu ya shahawa na wanapoiskia wao huona raha ni kana kwamba ni kilevi hivi chenye kuwapa tulizo la akili zao.
Vile vile kwa watu ambao hukutwa na ndoto nyevu kisha aiamke basi wao hukimbilia kufyonza hizo mbegu mapema pindi zinapokuwa zimetoka kuwahi uhai ule wa mbegu ndio maana baadhi ya watu wengi huota wameshusha mbegu nyingi lakini akitizama kwenye shuka vinakuwa kama matone tu,

2: Kuingia mkataba kwa ajili ya kupata mali
Hapa mara nyingi mtu huyu huenda kutafuta jini ambaye atakuwa nae kimapenzi na ampe mali:
Sasa huko anakuwa kapewa masharti matatu: asinywe pombe, asivute sigara na asiwe na mwanamke tofauti na yeye huyo jini, au mwanaume tofauti na yeye, kwa muda atakuo kuwa kautaka yeye:
Hapo utaaambiwa usubiri usiku wa jumamosi saa sita usiku ikifika hiyo saa utatakiwa mazingira ya ndani kwako yawe safi na pia uchome udi saba kikiwa chumba kipo tupu kisha zikiisha udi hizo aingize kitanda ambacho atakuwa kakiandaa kiwe cha chuma kipakaliwe rangi nyeupe na nyeusi na kwa siri sana anachora picha ya nyoka aliyetoa ulimi nje, kisha baada ya hapo aweke shuka godoro atandike shuka nyeupe na pazia ziwe nyeupe na awe anagamba la nyoka kisha alichome moto abaki alivyozaliwa na mwili wake aupake mafuta yang'ae kisha ashikilie udi baada ya kuchoma gamba la nyoka kisha aseme maneno haya mara 7 (*******************************************)baada ya hapo utasema jinsia kwa sauti ya hisssssssssssss kama vile nyoka anasema akiwa kainama atakapoinua tu kichwa chake kuangalia kwenye mlango wa chumba hicho anachofanyia ujinga wake huu. atakutanisha macho yake na binti mrembo ambaye urembo wake kwa yeye muhanga ataona duniani hajawahi kutokea na vigezo vyote anavyotaka kuviona kwa binti mrembo au kijana mrembo ataviona kwa kiumbe huyo, atazungumza nae kisha atamwambia kila anachotaka na hata chelewa kwa muda anaotaka atakuwa kampatia, baada ya makubaliano atafanya nae ngono na kisha atamuachia kama ni pete au cheni ambayo atakaa nayo na atakuwa kakubali kuolewa na kiumbe huyo basi akimtaka popote saa yoyote atatakiwa asugue pete hiyo kwenye meno au kubusu na shetani huyo atatokea hapo hapo hata kama yeye atakuwa magharibi na jini huyo awe mashariki.
Na ukimuona mtu anafanya haya muonyeshe thread hii ajue anathubutu kudiriki na kitu gani.
baada ya hapo watu wengi hawaoni starehe zaidi ya hizi 3 sasa mwanzo wengi hujaribu na kuona ni rahisi vile kiumbe hicho hata ukiambie kikae umbile la nani kitajibadili na hata ukiambie kiigize sauti yake hakita kosea na kitakupenda sana ila sasa ukosee kikutie adabu. (Utamaliza waganga na waganguzi/maadamu ni maagano ulifanya mwenyewe hiyo ni zima yako) na ukitaka kukiondoa kinaondoka na vyote kilichokupa. wengine vikiwazoea huanza kuwaambia toka tu nje ya mapenzi hamna shida sasa mtu anavurugika taratibu anahisi anaishi na binadamu akiona anafoka hakajibu kanalia akifanya visa kana vumilia siku umefanya jambo nje ya makubaliano utaona cha mtema kuni

View attachment 1183769
Nikijaaliwa taongezea nyama kwenye thread hii kwa maana kuna mengi ya kufahamu.

KUMBUKA:
kila unapokaa muombe Mwenyezi Mungu akukinge na viumbe hivi maana vikikukumba kutoka huwa ni vigumu sana hadi upate mwenye maarifa navyo

kwa haya na mengineyo zaidi kwa undani tembelea!


Ikiwa una swali na upo nje ya forums:

tumia email hii rakimsspiritual@gmail.com
au namba ya mtu aliye karibu nami:

0626085437
Rakims
wewe unavijuaje, unaundugu navyo?
 
wewe unapingana na kitabu hicho hicho ambacho kinasema miongoni mwetu kuna vitu wachache tu ndio wamepewa sasa kama wewe hujapewa kitu endelea kuwa looser

Rakims


Niendelee kuwa looser wa kitu gani??, hivi mimi na wewe nani looser??.

Wewe ndiye looser kwa kuifanya Qur'an ionekane ni kitabu cha ngano za majini badala ya kuwa kitabu cha kuongoza mwanadamu kiroho na kimwili.

Leo watu wengine wanaogopa hata kuigusa Qur'an kwa khofu kwamba watapatwa na majini yenu mnayoyaamini katika mila zenu.

Leo waganga wa kienyeji wanaandika aya za Qur'an katika sahani kwa kutumia zafarani na kuuosha kwa maji na kuwanywesha watu (kombe)!!!, Quran imekuwa kitu cha mchezo kiasi hicho!!;;, inasikitisha sana..
 
Wapi nimeandika Quran ni kitabu cha majini--- Subiani, Makata, nk? au cha kupungia majini? anaepunga majini hiyo ni yeye na nafsi yake na pia anaesema ni kitabu cha majini ni yeye na nafsi yake! ama kwa hapa umesema wewe basi ni wewe na nafsi yako!

Rakims



Mimi nilifafanua juu ya aina za majini waliotajwa katika Qur'an, wewe unapinga, sasa ni juu yako na wewe utoe ufafanuzi kutetea jinsi unavyoelewa kuhusu hayo majini.

Toa maelezo ili mtu asiyejua hayo majini aelewe ni kitu gani, siyo kubisha tu ilimradi ionekane Rakim yupo.!!😝😝
 


Eti, sahihi !!, sahihi kitu gani??!!.

Wageni wanaozungumzwa katika Qur'an ni wale wageni wa Nabii Ibrahimu (as), na imeandikwa hivi;

------ ضيف إبراهيم المكرمين--- (dhwaifi Ibrahiim almukramiin), yaani; Wageni waheshimiwa wa Ibrahimu.

Neno lililotumika kwa maana ya wageni hapo ni "dhwaifi" (ضيف).

Neno lililotumika katika kamusi (Lane &Aqrab) kwa maana ya neno "jinn" (جن), ni neno "Stranger" ambalo kwa kiarabu ni "gharib" (غريب).

Neno "stranger" limetokana na neno la kilatini "strange" (adjective), na lina maana pana sana na maana zote hizo kimsingi zinaashiria hali/ sifa ya "ugeni" katika vitu na watu (unfamiliarity), hivyo neno "strange" likazaa "stranger" na maana yake hasa kwa kiingereza linapohusu mtu/watu ni ""FOREIGNER(S) ", hivyo niliposema wale majini waliotajwa kwenye Surah Jinn ni wageni nilikuwa na maana ya "strangers" au "Foreigners" kwa sababu maana za hayo maneno ni sawa japo katika kamusi limeandikwa hilo moja tu yaani "strangers".

Neno "Foreigners" kwa kiarabu ni (اجنبي) angalia hapo, kama wewe ni mjuzi wa Lugha ya kiarabu japo kidogo tu, utaona mzizi wa neno "janna" (جن) hapo ndani ukiwepo katika hilo neno licha ya hiyo "conjugation" iliyoongeza herufi ya ب na ي mwishoni na ا mwanzoni lakini hapo kati bado utaona huo mzizi wa ج na ن.

Hivyo sasa wale wageni wa Nabii Ibrahim (as) walikuwa "guests" wake na wale majini waliotajwa katika surah Jinn ni Foreigners (strangers).

Katika lugha ya kiswahili huwezi kutofautisha kati ya guests, foreigners / strangers. Wote tunawaita wageni.

Qur'an inasema yenyewe ni muongozo kwa watu, na ukisoma katika mwanzoni mwa hiyo sura jinn utaona hao majinn wakiisifia Quran wakisema hakika tumeisikia Quran ya ajabu inayoongoza kwenye uongofu" --- na baadaye wakaikubali, sasa Quran ni muongozo kwa watu na kwakuwa wale majinn waliipokea iwe kiongozi chao basi wale majinn lazima walikuwa ni watu (binadamu).

Kinyume na ufafanuzi huu aje ulamaa yeyote na alete hoja kupinga.

Quran ni kitabu cha watu wenye akili na fikra wala sio kitabu cha kupungia mapepo na majini mahaba, makata, na subiani na hayo yote ni uongo mkubwa hakuna vitu kama hivyo.
 
Back
Top Bottom