Mjue Peter Mollel Gumbo aka Pierre Konki Mzee wa Liquid ambaye wengi hawafahamu vizuri

Mjue Peter Mollel Gumbo aka Pierre Konki Mzee wa Liquid ambaye wengi hawafahamu vizuri

Peter Mollel maarufu kama pierre gumbo au liquid alishawai kusema yeye sio mlevi ni mnywaji na huwa ana biashara zake anazifanya na jioni huwa anaenda kunywa pombe.

Kwenye clip zinazosambaa sijawai kuona akifanya mambo ya ajabu wanayofanya walevi kama kutukana ama kuleta vurugu au kugombana na mtu

Baada ya kupata umaarufu clip video zinazomuonesha akinywa pombe zimekuwa hazipo na huwa anahojiwa au akifanya matangazo yake bila kunywa pombe

Kutoka kwenye video za kunywa pombe mpaka kwenye video za matangazo interview na media kubwa kukutana na watu maarufu ni hatua kubwa
Ulevi mbaya zaidi kuliko ulevi wote ni ulevi wa madaraka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Piere baada ya kulewa umaarufu, akihojiwa na mwandishi wa habari alimwita "taka taka" "we ni taka taka tu".
Leo waandishi wa habari wanapewa nasaha kuachana na Pierre ambaye RC amemtambua kama "mtu wa hovyo hovyo". Karma is Bitch
Japo watanzania bado wako upande wa Pierre, na hii ni bahati isiyo ya kawaida...kumfurahisha mtanzania!....Pierre achukue hii kama alert juu ya namna gani anapaswa kua na adabu na ukarimu pasi na kujikweza kisa tu ni maarufu na anapata deals...watanzania ni species za ajabu sana..watamshusha na kumpuuza hatoamini.
Nenda youtube kwenye channel ya wasafi tv uangalie video yote ndo uje ucomment apa sio unaangalia kile kiclip alichopost bashite
 
Pierre is trending.

Huyu jamaa ni mtu wa wapi na back ground yake ya maisha ikoje?

Mwenye cv ya huyu Bwana atupatie.

Maana kila kukicha anazidi kuwa juu. Kuwa kileleni. Nambari 1

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TWENDENI NA PIERRE
Nandy kwa mdomo wake alidai kupiga pesa nyingi baada ya video yake ya chupi na Bilnass... akapata na ubalozi wa brand kadhaa. Hayo ndo mambo ya maana?

Hamisa Mobetto baada ya kuzaa na Diamond ambaye alikuwa kwenye uhusiano na Zari. Na zaidi akaendelea kupata umaarufu kwa matukio ya ngono na uzinzi mpaka juzi tu na kapata ubalozi wa brand kadhaa... umaarufu wa uasherati ni wa maana zaidi?

Steve Yanga kwa kulialia tu baada ya Yanga kupigwa goli 5 na Simba. Manji akampa bodaboda na baadaye Azam wakampandia dau akawa shabiki wao na kupewa ajira ya kudumu. Kulialia tu kama mwehu akawa maarufu akapewa na ajira nzuri.

Pierre siyo mlevi mwenye kulala mtaroni wala kutusi watu mitaani. Ni mnywaji ambaye clip yake moja tu akichekesha watu ilisambaa mitandaoni na kumpa umaarufu. Na yeye kutumia nafasi hiyo kuendelea kupiga pesa. Anaharibu nini kama wenyewe mlitumia punguzo la bei ya pombe kuhamasisha kushangilia Taifa Stars?

Kwani Steve Nyerere ana kipi cha maana kinachopelekea awekwe mbele mbele kwenye issue za msingi hata na serikali ya mkoa?

Kuna video ngapi za kipuuzi za wasanii baadhi wa Bongo Movie zinasambaa mitandaoni na bado wanawekwa mbele kwenye masuala ya kitaifa?

Huwezi kumharibia Pierre ambaye anaingiza pesa bila kuvunja sheria za nchi. Haya mambo yapo hata kwa wenzetu. Hivi Mpoki anafanya kipi kwenye vichekesho kiasi cha kuonekana wa maana na Pierre awe mpuuzi?

Joti kuvaa na kujipodoa kikekike ndo mambo ya maana ya kumfanya awe brand ambassador wa kampuni kubwa? Kwanini Pierre tu?

NB😛ovu ruksa

NB: Mimi sijawahi kugusa pombe
 
Huyu jamaa kaharibu sana ile kiki baada ya mwenyekiti wa kamati ya ushindi kufanikiwa ,mbaya zaidi kiki yake imepozwa na huyu Pierre,ndomana jamaa anamaindi.
 
Nyota ya Pierre ipo juu na atabaki kileleni. tatizo lilianzia Ikulu baada ya mama kumponda kaka na kumsifia Pieree
 
Jina: Peter mollel gumbo
Sex:Male
Age:42
Education:form 4
Marital status: Never married
Tribe:Mmeru
Region:Arusha-Tanzania
Occupation: carpenter man
Height: Short below the mean
Interests: Comedian

Conflicts: Conflict with bashite concerning public reputation/Media promotion about his stupid issue of drinking alcohol too much.


Wengine waongezee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom