Mjue Peter Mollel Gumbo aka Pierre Konki Mzee wa Liquid ambaye wengi hawafahamu vizuri

Mjue Peter Mollel Gumbo aka Pierre Konki Mzee wa Liquid ambaye wengi hawafahamu vizuri

Konki Liquid. Pierre. Mama nakufa. Chii. Ni utambulisho wa mwanamume aliyeishika mitandao ya kijamii wakati huu.

Huyu ni Peter Mollel aliyejizolea umaarufu baada ya video iliyomuonyesha akisema “mama nakufa” kuzagaa mitandaoni mwishoni mwa mwaka jana.
Leo Machi 13, 2019 ametembelea ofisi za kampuni ya Mwananchi na kufunguka mengi kuhusu maisha, umaarufu na mipango yake ya baadaye.

Pamoja na wengi kumfahamu kwa video hizo zinazomuonyesha akiwa kwenye vilabu vya usiku na baa, Pierre anasema yeye si mlevi kama wengi wanavyomtambua.

“Kuna mtu aliandika katika mitandao ya kijamii akisema mimi ni mlevi wa taifa, hilo halina ukweli wowote kwa kuwa nina shughuli zangu na huwa nakunywa baada ya mambo mengine, angeniita mnywaji angepatia,” amesema Pierre huku akitabasamu.

“Mimi kama hamjui nina ofisi ya kuuza samani pale Keko na sofa moja nauza kuanzia Sh3 milioni, meza Sh1.2 milioni . Umaarufu pia umeniongezea chanzo kingine cha mapato. Katika shoo moja nalipwa hadi Sh3 milioni kwa usiku mmoja,” amesema Pierre.

Alipoulizwa kuhusu familia, Pierre mwenye umri wa miaka 42 amesema hajaoa na hana mtoto na kueleza kwamba katika suala la ndoa hataki kukurupuka na kuja kujutia baadaye.

Wakati kwa upande wa ratiba yake ya kila siku, amesema huwa mara nyingi analala saa tisa usiku na kuamka saa nne asubuhi na jambo la kwanza analofanya ni kusali kwani anaamini Mungu ndio kila kitu pamoja na kwamba kwake starehe ni kila siku.View attachment 1044853

Sent using Jamii Forums mobile app
Nchi imekuwa ya watu wapumbavu watupu, huyu naye atapandikiza mawazo ya kipumbavu kwa watoto wetu na watamuona wa maana. Alianza Shika, sasa tunaye huyu.
 
Eti huyo naye 'celebrity'. Tanzania tunapenda kutoa coverage kwa vitu vya kupuuzi kweli.
Hapana nadhani wewe ni mshamba, hakuna watu wanaongoza kutoa coverage kwa vitu vya kipuuzi kama wazungu, nadhani haufuatilii media za nje huko ndiyo maana umendika pumba ukidhani ni kitu cha maana, pia acha wivu kwa konki liquid..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapana nadhani wewe ni mshamba, hakuna watu wanaongoza kutoa coverage kwa vitu vya kipuuzi kama wazungu, nadhani haufuatilii media za nje huko ndiyo maana umendika pumba ukidhani ni kitu cha maana, pia acha wivu kwa konki liquid..

Sent using Jamii Forums mobile app
Leta upumbavu wako tukupe coverage na wewe.
 
Lofa anaamuka saa nne wakati bilionea Dangote analala masaa 4 tu,halafu baadae ataomba tumchangie kwani kafanye mengi kuitangaza Tanzania.
 
Peter Mollel maarufu kama pierre gumbo au liquid alishawai kusema yeye sio mlevi ni mnywaji na huwa ana biashara zake anazifanya na jioni huwa anaenda kunywa pombe.

Kwenye clip zinazosambaa sijawai kuona akifanya mambo ya ajabu wanayofanya walevi kama kutukana ama kuleta vurugu au kugombana na mtu

Baada ya kupata umaarufu clip video zinazomuonesha akinywa pombe zimekuwa hazipo na huwa anahojiwa au akifanya matangazo yake bila kunywa pombe

Kutoka kwenye video za kunywa pombe mpaka kwenye video za matangazo interview na media kubwa kukutana na watu maarufu ni hatua kubwa
 
Ni Kweli kabisa.
Mimi namfahamu vizuri Piere, hajawahi kuwa Mlevi.
Ni mtu amayejiheshimu na kuheshimu watu.
Ndio maana nayeye anaheshimiwa na watu.
Madikteta hawataki watu wengine waheshimiwe.
WAKUHESHIMIWA NI WAO TU NA NI LAZIMA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom