Mjue tapeli aliyewatapeli graduates wengi kwa kuwahadaa nafasi za kazi NMB

Mjue tapeli aliyewatapeli graduates wengi kwa kuwahadaa nafasi za kazi NMB

Mkuu hawa vijana wanasikitisha sana.
Kibaya zaidi wameenda shule.
Mda huu nipo sokoni hapa vijana na wazee hawalali wanapiga kazi hasa.
Wamama pia wanakoleza majiko wapike vitafunio chai na uji.

Cha ajabu sisi vijana tena wasomi hatutaki fanya kazi na kuamua kujiajiri kwenye utapeli.
Nakubaliana na wewe kabisa madam, shida ni kupenda shortcuts, dunia hii mtu ajitokeze tu akupe mchongo kama huo haushtuki?? Au kwao yeye hana ndugu au watu wa karibu wenye uhitaji wa namna hiyo, that's so ridiculous 😤
 
Shauri wakalime na siyo kuchoma maandazi na chapati. Kilimo pekee ndiyo suluhisho la umasikini kwa vijana. Ardhi tunayo kubwa na mahotaji ya chakula ktk hii Kanda bafo yapo juu

Sent from my SM-J530F using JamiiForums mobile app
Kilimo si lelemama kama hauna mtaji.
Serikali iangalie upatikanaji rahisi wa mitaji ya kilimo.
 
  • Thanks
Reactions: amu
Sandali Ali, Dah acha tu kiongozi. Huyu jamaa mimi alinirequest urafiki Facebook basi nikapitia profile yake na nilipoona picha yake sikuitambua. Akaja inbox na kuanzia story za sehemu niliposoma o-level, basi kutazama baadhi ya mutual friends ni kweli wapo wale waliokua mbele ya darasa langu na hakunionesha shaka yoyote na hasa ukiweka na lafudhi yake ya kisukuma basi nikaondoa wasiwasi maana huko nilikosoma wanafunzi wa jamii hiyo walikua wengi. Basi akaniuliza nilipo nikamjibu nae akanambia yupo Arusha na anafanya kazi NMB akaniambia kuna kazi zipo anaweza kunifanyia mpango niipate mojawapo basi sikuona ubaya na nikajua ndo navuna matunda ya mahusiano mema niliyokua NATO lna wenzangu wakati anasoma.

Akaniambia nimtumie CV na soft copy za vyeti. Nikamtumia na huku akiniharakisha sana basi nikajisemea moyoni kuwa hapa kazi ipo.
Baada ya kutuma akaniambia kuna gharama za ku'certify vyeti pia kuna copy moja inabid itumwe headquarters kwa njia ya EMS so nimtumie elfu 25 kwa ajili ya shughuli hizo, nani bila kusita nikamtumia fasta japo nikajiuliza yaani huyu rafiki yupo na position NMB anashindwaje kulimaliza hill tatizo dogo hivyo!! Nikakausha nikijua nasubiri tu simu ya interview.

Baada ya hapo akaniambia atanipa feedback kesho yake asbuhi. Hiyo kesho yake nikawa busy sana hivyo sikumtafuta, akanicheki na kuniambia mambo yanaenda fresh ila kuna issue ya mwisho inabidi niikamilishe maana alikua a nahitaji apate confirmation kwanza ya hiyo kazi toka kwa huyo mkubwa, kuuliza issue gani akanambia inatakiwa nitume hela ya job insurance ambayo itakua refunded nikianza kazi, basi hapo ndo akili ikanirudia.

Nikarudi nyuma nikagundua naomba niliyotumia kumtumia hela ni tofauti na niliyoongea nae pia ikiwa na jina tofauti na lake, lakini hizi habari za insurance nazo zinatoka wapi wakati hata interview sijaitwa? Wakati huo huo alisema angenitumia job description ya hiyo nafasi ambayo hadi wakati huo nilikua sijatumiwa hivyo bado sijui hata nafasi niniyoipigania ni nini.

Akaanza kunisisitiza kila mda niitume hiyo hela, mi nikamwambia kuwa anisaidie kuilipa na mimi nitamrejeshea baada ya kwenda huko Arusha kwenye hiyo interview. Ila akaendelea kunikomalia vibaya mno hadi nikamwambia "nashkuru sana kwa moyo wako wa kutaka kunisaidia, ila siihitaji tena hiyo kazi"

Leo baada ya kusoma huu uzi ndo natamvua kuwa nilitapeliwa na huyu jamaa ilikua sh 27,000 nikimtumia kwa tigo pesa. Dah hadi leo namba yake nimeisave kwa jina la "Venance M'boyzia"
 
Nimemcheki fb nimeona nashea na marafiki zangu 23, (mutual friends) wanne kati Yao Ni product ya Lindi Boys Kama alivyoeleza kwenye wasifu wake kuwa amesoma Lindi Boys. Ngoja nimcall mutual friend mmoja nimdadisi. Mana na mimi kwa umbea nipo vizuri.
 
Nimemcheki fb nna mutual friend mmoja na yeye kiukweli sijawahi kutapeliwa na MTU yoyote though kwenye harakati za kuomba kazi nimeshakutana na matapeli wengi sana good lucky najua kuwa kazi yoyote professional huwezi kuombwa hela yoyote ile ukishaaply unasubiri interview tu so ukitapeliwa umetaka kutapeliwa
 
Nimemcheki fb nimeona nashea na marafiki zangu 23, (mutual friends)wa4 kati Yao Ni product ya Lindi Boys Kama alivyoeleza kwenye wasifu wake kuwa amesoma Lindi Boys. Ngoja nimcall mutual friend mmoja nimdadisi. Mana na mimi kwa umbea nipo vizuri.
Acha tu, mi mwenyewe alinikamatia hapo tu na tamaa zangu za kijinga kupenda virahisi pasipo kutumia nguvu
 
Uvivu, Kupenda kitonga, kutoshughulisha akili ndio chanzo cha kutapeliwa..

Ila Mkuu una uhakika hio picha ni yake?
Matapeli wengi wa mtandao hawatumii picha zao.

Kama huyu kweli ni tapeli hivyo na katumia picha yaka na/au jina lake halisi....

Naye akili zake hazitofautiani na hao anaowatapeli.
Ni pwagu na pwaguzi....
Uwezekano mkubwa kabisa siyo picha yake na hata jina siyo la tapeli. Formula ni zile zile: 1. Ukiitiwa fursa basi wewe ndiye fursa ya kuneemesha wengine! 2. Usimpe/usimtumie mtu yoyote fedha bila kumjua kwa undani kabisa.
 
Hivi alivyovaa tu kwenye picha kama ni yeye ni ushahidi tosha wa utapeli. Anayeibiwa na huyu tumuonee huruma na mara nyingi ni vijana wadogo. Mtu kama mimi hata kama nina ndugu hana kazi siwezi kumuunganisha naye.

Tangu lini facebook ikawa sehemu sahihi ya kupata marafiki. Kama umekosa rafiki mtaani kwako na kwenye shughuli zako basi pumzika tu. Rafiki wa kweli hapatikani facebook wala twitter
 
Nimemcheki fb nna mutual friend mmoja na yeye kiukweli sijawahi kutapeliwa na MTU yoyote though kwenye harakati za kuomba kazi nimeshakutana na matapeli wengi sana good lucky najua kuwa kazi yoyote professional huwezi kuombwa hela yoyote ile ukishaaply unasubiri interview tu so ukitapeliwa umetaka kutapeliwa
Ni kweli kabisa na mimi pia naamini hivyo. Na ndio maana aliponiletea habari za eti job insurance nikajua nimeingia mtegoni. Ila elfu 27 niliyomtumia aliila kwa hoja kuwa ni lazma a certify vyeti pia atume nakala moja kwa njia ya EMS vitu ambavyo sikutilia shaka kabisaaaa maana ni kawaida
 
Back
Top Bottom