Sandali Ali, Dah acha tu kiongozi. Huyu jamaa mimi alinirequest urafiki Facebook basi nikapitia profile yake na nilipoona picha yake sikuitambua. Akaja inbox na kuanzia story za sehemu niliposoma o-level, basi kutazama baadhi ya mutual friends ni kweli wapo wale waliokua mbele ya darasa langu na hakunionesha shaka yoyote na hasa ukiweka na lafudhi yake ya kisukuma basi nikaondoa wasiwasi maana huko nilikosoma wanafunzi wa jamii hiyo walikua wengi. Basi akaniuliza nilipo nikamjibu nae akanambia yupo Arusha na anafanya kazi NMB akaniambia kuna kazi zipo anaweza kunifanyia mpango niipate mojawapo basi sikuona ubaya na nikajua ndo navuna matunda ya mahusiano mema niliyokua NATO lna wenzangu wakati anasoma.
Akaniambia nimtumie CV na soft copy za vyeti. Nikamtumia na huku akiniharakisha sana basi nikajisemea moyoni kuwa hapa kazi ipo.
Baada ya kutuma akaniambia kuna gharama za ku'certify vyeti pia kuna copy moja inabid itumwe headquarters kwa njia ya EMS so nimtumie elfu 25 kwa ajili ya shughuli hizo, nani bila kusita nikamtumia fasta japo nikajiuliza yaani huyu rafiki yupo na position NMB anashindwaje kulimaliza hill tatizo dogo hivyo!! Nikakausha nikijua nasubiri tu simu ya interview.
Baada ya hapo akaniambia atanipa feedback kesho yake asbuhi. Hiyo kesho yake nikawa busy sana hivyo sikumtafuta, akanicheki na kuniambia mambo yanaenda fresh ila kuna issue ya mwisho inabidi niikamilishe maana alikua a nahitaji apate confirmation kwanza ya hiyo kazi toka kwa huyo mkubwa, kuuliza issue gani akanambia inatakiwa nitume hela ya job insurance ambayo itakua refunded nikianza kazi, basi hapo ndo akili ikanirudia.
Nikarudi nyuma nikagundua naomba niliyotumia kumtumia hela ni tofauti na niliyoongea nae pia ikiwa na jina tofauti na lake, lakini hizi habari za insurance nazo zinatoka wapi wakati hata interview sijaitwa? Wakati huo huo alisema angenitumia job description ya hiyo nafasi ambayo hadi wakati huo nilikua sijatumiwa hivyo bado sijui hata nafasi niniyoipigania ni nini.
Akaanza kunisisitiza kila mda niitume hiyo hela, mi nikamwambia kuwa anisaidie kuilipa na mimi nitamrejeshea baada ya kwenda huko Arusha kwenye hiyo interview. Ila akaendelea kunikomalia vibaya mno hadi nikamwambia "nashkuru sana kwa moyo wako wa kutaka kunisaidia, ila siihitaji tena hiyo kazi"
Leo baada ya kusoma huu uzi ndo natamvua kuwa nilitapeliwa na huyu jamaa ilikua sh 27,000 nikimtumia kwa tigo pesa. Dah hadi leo namba yake nimeisave kwa jina la "Venance M'boyzia"