Mkaka mzuri, ana magari na kazi nzuri ila amenikosa kwa utongozaji wake wa kitoto

Naomba hivyo vitabu please!!
 

Uko sahihi kwa ulichokifanya. Nakupongeza. Binafsi nakereka sana ninapokutana na mtu unayekutana naye mara ya kwanza alafu anaanza kutaja mafanikio yake kimaisha wakati hujamwuliza. Si katika mahusiano tuu hata katika urafiki wa kawaida hata ikiwa ni mwanaume mwenzako. Picha ya kwanza inayoonekana hapo ni ulimbukeni, na anaona hilo gari au kufanya kwake kazi bank au taasisi flani kubwa kubwa ndo silaha pekee ya kuwachapia wanawake. Wanasahau kuwa kuna bad boys wanakula pisi kali huwezi amini.

Back in 2007 niliwahi kukutana na class mate wangu wa advance pale UDSM karibu na hill park. huyu dogo alisoma economics na mimi nikasoma education. Sasa mbwembwe zake kwa sababu hatukuonana muda mrefu cha kwanza akaanza kuniambia anafanya kazi wizara ya viwanda, hapo hapo akanionyesha gari yake, hapo hapo kanionyesha picha ya nyumba yake anayojenga changanyikeni. Hapo hata sijamwuliza wala hajaniuliza kuhusu issues zangu. Upuuzi wake alidhani mimi nitakuwa nimeenda kufundisha sekondari kama ilivyozoeleka kumbe niko kwenye taasisi nyingine kubwa tena mshahara hatupishani sana. Hata hivyo nikaona ujinga kujitambulisha kihivyoo, tukaachana bila kumwambia nafanya kazi wapi. Na sasa hivi kama ni elimu nimeshamzidi ngazi moja. Dharau mbaya
 
Wadada wa kibongo ndo mnapokosea, huyo jamaa bado humfaham kabisa, na hiyo ni tabia ya wanaume wote.. Kama uko single, kwani ungekufa kumpigia na kumfaham zaidi?
First acquaintances huwezi kuropoka mambo ya mali, kazi, magari na ufahari wako. Binafsi tu mwanaume akija na swagger za namna hiyo namkataa. Mtu hata humjui unaanzaje kutaja unavyomiliki, kwani kauliza unamiliki nini?

Sio tabia ya wanaume, ni tabia ya baadhi ya watu tu!
 
Naomba icho cha kiswahili maana kingereza ni tatizo kwangu
 
Ungeviweka hivo vitabu hapa ingekua vizur
 
Umeandika Kama Mwanaume.

Wewe ni mwanaume
Au umempa mwanaume akuandikie.
Chagua kimoja.

Flow ya uandishi na muanganiko wa neno Kwa neno, sentensk Kwa sentensi na Aya Kwa Aya ni wakiume zaidi
Taikon wa fasihi[emoji1787][emoji1787]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…