Mkaka mzuri, ana magari na kazi nzuri ila amenikosa kwa utongozaji wake wa kitoto

Mkaka mzuri, ana magari na kazi nzuri ila amenikosa kwa utongozaji wake wa kitoto

Kosa lake ni kuvitaja hadharan hvyo vtu ila ukwel usiopingika ni kwamba hvyo vtu ndo wanavyopenda wanawake

Yaan unapo mu aproach tu anawaza huyu ana kazi.. au nyumba.. au ana gar?

So mwamba akarahisisha kwa kuvinadi mapema.. binti hukupenda.. bas sawa.. huyo mwamba hakukupenda kiivyo alitaka kula tunda asepe... Mwanamke unaempenda kikwel kwanza utakua unatetemeka hata hayo magar huwez kumbuka..

Kuna ukweli pia, alitaka kupiga na kusepa.. ni sawa tu nae kuna wanawake anakutana nao hawana wowo, wanamshobokea anawatosa ndio maisha...
 
Bro uko vizuri kwenye utunzi Hivyo vitabu unauza bei gani? Hiyo story yako ipo humo?
 
Mkuu mwnywe nazungusha matunda majumbani unaonaje kama tukiunganisha biashara😂😂😂
Tuje kua na BMW maana Harrier sio nzuri kama mtoa mada alivyotuambia
Dah 😁😁😁inatosha sasa.
 
Nilikuwa nimekaa zangu kwenye mgahawa fulani. Akaja mkaka mzuri tu na alikuwa amependeza. Akakaa kiti cha mbele yangu.

"Mambo? Nimependa nikae na wewe hapa." Akaniongelesha.

"Haina shida." Nikajibu.

"Mbona huna kinywaji au chochote? Agiza chochote. Usikae kinyonge hivyo" Aliuliza.

Nikamjibu "Nimeagiza chakula. Ndio nakisubiri."

"Oh sawa. Vizuri tufahamiane. Me naitwa James, naishi (******). Nafanya kazi hapo (****) Bank kama branch manager. Nikufahamu na wewe please!"

"Naitwa Ederra. Naishi (******).". Nikajitambulisha.

Akaendelea na stori nyingine kwa dakika chache kisha akainuka na kusema angerudi pale punde. Baada ya dakika tatu akarudi.

"Nimerudi Ederra. Nilienda kuangalia gari yangu. Nilikuwa na wasiwasi kama nilikuwa nimepandisha vioo." Akasema huku akikaa tena kwenye kiti.

"Sawa. Karibu tena."

"Asante. Nilikuwa naogopa isije kunyesha mvua au watu wakaniibia KiBMW changu. Unajua gari yenyewe ni mpya nisije kupata hasara. Nilichoka kutembelea Harrier nikaona ninunue na hii"

"Yeah wasiwasi ndio akili." Nikamuunga mkono.

Chakula kikafika. Na yeye akaagiza. Nikawa naendelea kula huku nikisikiliza stori za magari yake, kazi yake nzuri, anapoishi na nyingine kama hizo mpaka nikamaliza kula.

Mhudumu alipokuja kuleta chakula cha jamaa nikamuomba bill.

"Acha tu nitalipa Ederra. Unalipaje wakati mimi niko hapa?" James akaingilia kati.

"Oh sawa. Nashukuru sana."

Nikamuaga kuwa naondoka. Akaniomba namba ya simu. Nikamwambia anipe yake ningemtafuta. Akanipa business card yake na kung'ang'ania nimpigie pale pale lakini nikamwambia asijali ningemtafuta tu. Nikaondoka.

Ile business card niliitupa kwenye dustbin baada ya kupotea kwenye upeo wa macho yake. Nisamehe James. Sio kwa ubaya.

Mwanaume unapotumia nguvu kutaka kuonesha magari unayoendesha, kazi yako unayoiona nzuri, unapoishi na mafanikio yako mengine kwa mwanamke ambaye ndiye kwanza unakutana naye unadhani ndiyo utamvutia?

Hii tabia haivutii. Meseji ya nje unayoileta kwa kufanya hivyo ni kuwa wewe ni mtu wa maana sana na mwenye mafanikio. Meseji hii ya nje sio inayoathiri mvuto wako kwenye akili ya mwanamke.

Meseji iliyojificha (ya ndani kabisa) ndio inayoathiri mvuto wako. Hiyo ni kwamba hujiamni na unadhani huna thamani wewe kama mwanaume na hivyo unalazimika kutumia vitu kama magari, kazi, mafinikio ili uonekane una thamani. Hakuna mwanamke anayejielewa anavutiwa na mwanaume wa hivi.

James asante kwa kunilipia chakula. Lakini wewe na wanaume wengine wenye akili kama zako badilikeni. Itawasaidia.

Jifunzeni kuwa na tabia zinazowavutia wadada. Mnaweza kusoma vitabu hivi viwili mtanishukuru baad3ae.

1) "UNLOCK HER LEGS: How to Effortlessly Attract Women..." By Dominic Mann

2) "MWANAUME WA DHAHABU : Jifunze Namna ya Kuwatawala Wanawake na Kutawala Mahusiano." By Anita Shija

Mwanaume tafuta uvisome yasije kukukuta ya James. Hasa hicho cha Kiswahili. Usipovipata njoo nikutumie bure tu. Utachangia bando lakini.
I love youu ❤❤❤
 
Very correct
..as for me napenda mtu awe so private...yani siku nikija gundua kwamba anamiliki mavitu na mahela ndo nafall in love mara 10
Yn nitreat vzr kimya kimya tu bila kujimwambafy....

Kifupi we nifiche kila kitu..kazi..kipato..unakoishi etc etc

Then huko mbelen nikijua(inategemea nutagyndua mwenyewe au utanieleza)
ndo nitakupenda mara 2000

Lkn ukija na style za kujimwambafy nakuignore hapo hapo maana naanza kuona hili jamaa ni lishamba[emoji3]
Wewe unajikosha tu hapa.. nini kitabadilika akianza au ukigundua mwenyewe? Wewe unapenda pesa mwenyewe umejidhihirisha hapa tayar… uyo jamaa angekuja kwako na hizo swaga usingechomoa😆
 
Back
Top Bottom