Mkaka mzuri, ana magari na kazi nzuri ila amenikosa kwa utongozaji wake wa kitoto

Mkaka mzuri, ana magari na kazi nzuri ila amenikosa kwa utongozaji wake wa kitoto

Umeandika Kama Mwanaume.

Wewe ni mwanaume
Au umempa mwanaume akuandikie.
Chagua kimoja.

Flow ya uandishi na muanganiko wa neno Kwa neno, sentensk Kwa sentensi na Aya Kwa Aya ni wakiume zaidi
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Behaviourist hili sio parody lako kwelii?
Mkuu mimi na mashine yangu hii mambo ya warembo wapi na wapi.Sinaga hizo mambo za warembo mimi.
dfile876.jpg
 
Una maoni mazuri. Lakini sifa kubwa ya wanaume wanaowavutia sana wadada ni "Kutojali". Ni kutojali ikiwa mwanamke unayemtaka, kumuomba namba, kuomba kutoka nae out au chochote atakubali au la. Ni Kutojali namna mwanamke anavyokuchukulia. Avoid seeking validation.

Kosa la James ni kuonesha uhitaji kupita kiasi. Alitakiwa asijali ikiwa ningemuona mtu wa maana au la. Kuanza kujivuna kwa mwanamke mgeni inaleta picha kuwa ndio tabia yako na mbinu ya kuwavutia wanawake. Hii inaweza kufanya kazi kwa wauzaji, wanawake wasiojiamini au washamba.

Kwa wanawake wengine kadri ulivyo mhitaji ndivyo unavyoshusha thamani yako. Kwa mfano unamuomba namba mdada akasema 'Hapana' using'ang'anie wala kusisitiza. Ukifanya hivyo unaonekana mhitaji sana na akili ya mwanamke inazidi kukukataa.

Wanaume wahitaji sana na ving'ang'nizi huwa hawana thamani. Ni ishara kuwa hawana kazi za kuwaweka busy, hawana wanawake wazuri wanaowapenda, hawana chochote cha maana na ndio maana wanatumia nguvu kulazimisha ukaribu. Akili ya mwanamke haivutiwi na watu wanaoonesha uhitaji kupita kiasi.

Unakuta mtu amekubaliana kutoka out na mdada halafu mdada akabadili mawazo dakika ya mwisho kabisa. Mtu anaanza kubembeleza, kupiga simu zisizopokelewa, kuahidi zawadi na mengine. Thamani yako inashuka, utu wako unashuka na mwanamke unazidi kumpoteza.

Kwa hadhi ya James ni ajabu sana kuonesha kujali kiasi kile. Alitakiwa asalimie na kupiga stori nyingine kwa kujiamini. Kwa kweli pengine saa hizi tungekuwa tunazungumzia mengine.
nimekuelewa,lakini naomba nikuulize,unakutana na mwanamke wa ndoto yako sehemu,na hakuna namna mnaweza kuonana tena siku ya usoni,yaani mkiachana hapo ndio huna ramani ya kumuona tena,mtu kama huyu kumbuka ndio wa ndoto yako na ni nadra kuwaona,unaachaje kuwa desperate?..
Point ya nyongeza,kuna uwezekano mkubwa huyo James wako asiwe James kweli,asiwe meneja wa bank yeyote wala hana gari lolote..Tywin lannister kwenye game of thrones aliwah kusema "anyone who says i am the king,is not a true king".Pengine alitaka kukuvua akazidisha mbinu,ila kila mwanaume na aina ya wanawake anaowataka,yeye anataka wanawake wa kubabaika na hivyo vitu,akikutana nae wataenda sawa.
Inaonekana wewe ni aina ya mwanamke ambae ili kumpata inabidi utumie mbinu,sio hisia.
 
Hata Wanawake wa hivyo wapo sana! Tena mwingine anaweza kua Yuko kwenye Mikutano wa kazi anaongea Kama Mkuu wa kitengo eti lazima akupigie simu ukipokea unamsikia yeye anamwaga ma points zake kwa meeting, utaita hallo hallo lakini hajibu anaendelea kufokea Wafanyakazi wake upande wa pili!!
Khaaaa[emoji1787][emoji1787][emoji1787]...ni ushamba aisee
 
Wewe unajikosha tu hapa.. nini kitabadilika akianza au ukigundua mwenyewe? Wewe unapenda pesa mwenyewe umejidhihirisha hapa tayar… uyo jamaa angekuja kwako na hizo swaga usingechomoa[emoji38]
[emoji28][emoji1787][emoji1787][emoji1787]sawa...hakuna asopenda hela..ht mimi napenda kweli tena haswaa....ila kuna namna wanakosea approach....kujimwambafy kwa maneno inakeraaaaaaaa[emoji1787]
 
Back
Top Bottom