Mkakati wa mama mwenye nyumba kushinda uchaguzi mkuu wa 2025 kwa 95% huu hapa umeshawiva tayari

Mkakati wa mama mwenye nyumba kushinda uchaguzi mkuu wa 2025 kwa 95% huu hapa umeshawiva tayari

Mbowe lamba asali utakavyo jasho lako tu.elishuhudia kwamacho kamanda hawa mbwa wanao andikaandika wasio nauwezo wakutoka nje kuleta kashkash hawana maana tunakua ulitumia rasilimali zafamilia naukoo wenu pamoja naukweni kuinua chama chetu pendwa ila wafuasi wako bado niwaoga nawapumbavu kwaviwango visivyo pimika nahata siku moja usije kubali kufa ukauacha ukoo wenu ukinuka umasikini nahali mbaya kwaajili yawapuuzi wasio saidika waoga wanafiki wenye chuki pandikizwa yote kwa yote piga hela zako nakama inawexekana washauli serikali waweke tozo Kila Kona ikiwezekana hata oxygen tuanze kuilipia kwamaana hakuna chakuokota hapo akili zitaanza kutukaa sawa
Yote kwa yote nakutakia afya njema namapambano mema ktk familia yako mungu akutie nguvu
Wewe hata kuandika hujui lakini umejilazimisha kuandika ili na wewe uonekane kuwa ni mmoja wa waliopo humu kumtetea Mbowe na genge lake. Hivi ushawahi kujiuliza ni kwanini watanzania ambao walikuwa tayari kupigwa mabomu, kukamatwa, kuumizwa na hata kuuwawa wakati wa Dr Slaa leo hii hawako tayari kukutwa na kadhia hiyo baada ya Dr Slaa kuondoka CDM?
Unajua kati ya 2010 hadi 2015 ni watu wangapi walifungwa, walipigwa, waliteswa na wengine waliuwawa kwa sababu tu ya kuandamana na bado watu hawakuchoka wala kuogopa kuandamana? Je ni kwanini baada ya uchaguzi wa 2015 hadi leo watu ndo wamegoma kuandamana?

Ukweli ni kwamba kuanzia mwaka 2010 hadi 2015, watanzania wengi waliamini kwamba wapinzani haswa CDM ikiongozwa na mwana mapambano hodari katibu mkuu wa enzi hizo mh dr Slaa wapo kwa ajili ya kupigania demokrasia, kupambana dhidi ya ufisadi uliokuwa unafanywa na baadhi ya viongozi wa serikali akiwemo mzee Lowasa. Sasa ilipofika mwaka 2015 huyu mlamba asali ninaemzungumzia hapa ndo akaingiza nuksi ndani ya chama baada ya kupewa chake mfukoni ili agawane na genge lake kisha wawapitishe wale waliowaita mafisadi wagombee uraisi kupitia chama chake. Hapo ndo watanzania walipoanza kuona usaliti, uongo na unafiki walio nao wapinzani katika siasa za Tanzania.

Sasa watanzania hao wakaona hamna tena sababu y wao kuwaamini tena viongozi wa upinzani iwe kwa njia ya maandamano, maneno matupu nk.
 
Waambie hao
Hebu fikiria eti mpaka leo bado kuna mtu mwenye akili zake timamu, anaamini kwamba huyu mwamba atawapeleka katika nchi ile ya asali na maziwa 🤣🤣🤣 ama kweli akili ni nywele kila mtu ana zake.

Jamaa atakuwa ana mganga mkali sana ambae kampa huyu mwamba uwezo wa kumiliki akili zaidi ya milioni 2 za wanachama wake katika mfuko wake. Ndo maana kila analosema chamani ndio hilo hilo 🤣🤣🤣
 
Attachments

  • images (39).jpeg
    images (39).jpeg
    24 KB · Views: 1
Acha Kuandika huku ukiwa kirabuni,Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani haihitaji kumshawishi kiongozi wa upinzani asusie uchaguzi ili yeye ashinde, kwa kuwa Rais wetu anakubalika na kupendwa Sana na watanzania,Anaungwa mkono na makundi yote kutokana na kazi kubwa aliyoifanya ndani ya muda mfupi,Hii ndio sababu ya wenye kuutamani Urais kupata kigugumizi Cha kuchukua fomu kushindana naye,Maana kila mtu anatambua kuwa hakuna mwenye ubavu wa kushindana na Rais Samia iwe jukwaani au kwenye boksi la kura
 
Tatizo vyama vyao vinaongozwa na makada wa kile kitengo cha wasiofahamika. Kwahiyo inapoonekana kuwa kuna uchaguzi ambao utakuwa mgumu kwa chama tawala kushinda, basi wazee wa kitendo wanawashtua wa vitengo wenzao wanaoongoza vyama hivyo watengeneze mgomo (wasuse) utakaosababisha chama tawala kipate ushindi mnono na hivyo kuendelea kutawala nchi yetu.
Vyovyote iwavyo, kususa sioni kama ni suluhu kwa nchi kama hii.
 
mpinzani yupi anayejielewa atapigania wapumbavu wanaoambiwa kupigania haki zao zilizoporwa yamekaa tu kama mazezeta.
Hao unaowaita wapumbavu ndio waliouwawa Unguja na Pemba mwaka 2001, lakini bado hawakuchoka wala kuogopa kuandamana, hao unaowaita wapumbavu ndio waliouwawa kwenye bomu la Soweto Arusha, ndio waliopigwa, walioadhibiwa na kufungwa na polisi katika maandamano mbali mbali ya kudai haki kuanzia mwaka 2010 hadi 2015 bila kuogopa kufa, kuteswa wala kuujeruhiwa.

Iweje baada ya mwenyekiti wa chama fulani kumkaribisha yule waliomwita fisadi papa agombee ndani ya chama chao ndio kibao kilipoanza kugeuka kuanzia maandamano ya ukuta na mengineyo?

Kuna jambo limejificha na baadhi ya wanaharakati wanalijua lakini ni nani wa kuthubutu kuongea ukweli kuhusu hilo. Kila mtu anakataa kuongea ukweli ili asije kuonekana ni msaliti wa mwenyekiti wa chama na chama kwa ujumla. Kinachofanyika sasa hivi ni hii style ya kuwatupia wananchi jumba bovu kwa kuwapa lawama mbali mbali kama hizi ulizoandika hapo juu ili kumnusuru mwenyekiti na kashfa ile ya mwaka 2015 ambayo imebadili kabisa mwelekeo wa mioyo ya watanzania kuhusu upinzani, maandamano nk. Ni mtanzania gani mwenye akili timamu ambae atakuwa tayari kudanganywa kizembe hivi na mtu ambae alikuwa anamuamini kwa asilimia zote?
 
Attachments

  • images (1).jpeg
    images (1).jpeg
    27.8 KB · Views: 1
  • download.jpeg
    download.jpeg
    10.7 KB · Views: 1
Habari zenu wana JF wenzangu, bila kupoteza muda ngoja niende kwenye mada husika ili kuwarahisishia wasomaji wasiopenda kusoma maandishi mengi.

Ni hivi... baada ya mama mwenye nyumba kufanikiwa kukitia chama chake mwenyewe mfukoni, na kuwadhibiti wale wote waliokuwa na ndoto ya kutaka kupimana nae ubavu mwaka 2025, sasa amehamisha mikakati yake ya ushindi kwa viongozi wakuu wawili wa vyama vyetu vikuu vya upinzani.

Viongozi hao ambao ndio nguzo kuu ya vyama vyao, tayari wameshatengenezwa kimkakati na mmoja wao aliwahi kuitwa mara mbili katika lile jumba jeupe la taifa na kukabidhiwa bahasha yake kimya kimya kama ishara ya shukran kwa makubaliano yao waliofikia na mama huyo wa nyumba yetu pendwa.

Viongozi hao licha ya account zao kuvimbishwa ili kupata nguvu ya kukamilisha walichopanga, lakini pia walihakikishiwa ulinzi wa maisha yao, ulinzi wa familia zao, ulinzi wa mali zao na pia kufutiwa kesi zao nk.

Mkakati huo utatimiaje, sasa fuatilia vizuri kile ninachoandika hapo chini 👇

Ikumbukwe kwamba vyama vya upinzani vimekuwa vikiitaka serikali itengeneze katiba mpya ambayo wanahisi itaweza kuwasaidia wao kushinda chaguzi mbali mbali na hatimae na kushika dola. Lakini kwa upande mungine pia wanaitaka serikali iifumue tume iliyopo na kuunda tume nyingine "huru" ambayo itawashirikisha wadau wote kwa ukaribu zaidi.

Kwahiyo sasa haya mambo mawili ya "katiba" na "tume huru" ndio yatakayotumiwa na wasukaji wa mpango huo kama kichochoro cha kutimiza mikakati ya ushindi wa mama huyo mwenye nyumba.

Inasemekana kitachofanyika ni kwamba serikali itaendelea na msimamo wake wa kutokuwa tayari kutengeneza katiba mpya wala kuunda tume huru, baada ya hapo kiongozi mmoja "mlamba asali mkongwe" wa upinzani atajifanya kuchukizwa na hali hiyo, kisha atatumia uwezo wake na madaraka yake makubwa katika chama kuwashawishi wenzake ambao asilimia kubwa ameshawatia mfukoni, kwamba wasusie uchaguzi wowote utakaofanyika nchini.

Wakishakubaliana kususia inamaana ushindani wa vyama vingine vya upinzani vilivyopo utakuwa mdogo sana hivyo kumpa mama mwenye nyumba fursa ya kuendelea kutawala yeye na bunge lake kama ilivyo sasa.

Yule kiongozi mungine ambae anatokea katika mkoa uliyopo pembezoni mwa ziwa fulani, atabaki kupewa nafasi ya kubwabwaja bwabwaja pale inapobidi ili kuwafunga macho wale wasiojua kile kinachoendelea katika siasa za nyumbani kwetu.

Dalili za mipango hiyo zimeshaanza kuonekana kwa viongozi hao kutia zip midomo yao, na mmoja wao kufikia hatua ya kwenda kumfagilia mama mwenye nyumba huko katika dunia ya kwanza.

Hii mada ni kwa ajili ya wale watu ambao wako huru kifikra na ki akili, wale ambao wanaona mbali na hawana mihemko ya kisiasa.

Hakika "moyo wa mtu msitu", unachokipanga wewe, sio kile anachokipanga mwenzio. Wakati kuna chawa wanashinda mitandaoni kuwapigania, kuwasifia na kuwafagilia viongozi wao wa vyao, wao wanaopiganiwa, wanaofagiliwa na kusifiwa wako busy kulamba asali kimya kimya na kutelekeza mipango ya vyama vyao kiaina.

Jioni njema wakuu. 🙏

Wangeshughulika kwanza kulipa mdeni na mishahara 2025 bado mbali. Maana watofautishe kuwawin CHADEMA na kuwatumikia wananchi.
 
Moja ya mbinu zao ni hiyo ya kuwatumia wachumia tumbo wakubwa wa vyama vya upinzani.
Kama unafikiria kuwa kuna mpinzani au mwanasiasa ambae atakukomboa ujue unajidanganya sana.

Maneno mengi kumbe lengo lako ni kuusema upinzani. Unaona aibu kuisema ccm iliyokamata vyombo vyote vya maamuzi, inatoza tozo, inatoza kodi, inakopa njee lakini unausema upinzani kana kwamba ndio imeunda serikali. Jifanye kipofu ipo siku utaona.
 
Ikiwa wale viongozi waliotegemewa kuleta mageuzi kupitia vyama vyao ndio hao wanaolamba asali na kupigania matumbo yao.

Ni njia gani nyingine unadhani inaweza kutumika kuleta mageuzi ya kweli nchini kupitia sanduku la kura?

Upinzani sio Viongozi, upinzani ni spirit ndani ya wafuasi wa upinzani. Hata Viongozi wakinunuliwa na serikali , upinzani utaendelea. Wameondoka wangapi upinzani bado upo?
 
Hili la kususia uchaguzi halikuanza kuzungumziwa leo wala jana. Toka enzi za CUF ya Lipumba na Maalim, pia wengi tulifikiri kuwa 2020 CDM na ACT wazalendo wasingeshiriki, lakini tukaona wanashiriki.

Kwahiyo hata huu uchaguzi wa 2025 najua wangeshiriki tu, lakini kwa vile tayari walamba asali wameshalambishwa kama nilivyosema, basi safari hii huenda ikawa kweli hawatoshiriki ili kukamilisha mission niliyoiandika hapo juu.

CCM walishajimilikisha serikali. CCM kushinda uchaguzi sio hadithi, wao washughulike na uchumi wa mwananchi na taifa. Mwezi januari watu hawana mishahara.
 
Habari zenu wana JF wenzangu, bila kupoteza muda ngoja niende kwenye mada husika ili kuwarahisishia wasomaji wasiopenda kusoma maandishi mengi.

Ni hivi... baada ya mama mwenye nyumba kufanikiwa kukitia chama chake mwenyewe mfukoni, na kuwadhibiti wale wote waliokuwa na ndoto ya kutaka kupimana nae ubavu mwaka 2025, sasa amehamisha mikakati yake ya ushindi kwa viongozi wakuu wawili wa vyama vyetu vikuu vya upinzani.

Viongozi hao ambao ndio nguzo kuu ya vyama vyao, tayari wameshatengenezwa kimkakati na mmoja wao aliwahi kuitwa mara mbili katika lile jumba jeupe la taifa na kukabidhiwa bahasha yake kimya kimya kama ishara ya shukran kwa makubaliano yao waliofikia na mama huyo wa nyumba yetu pendwa.

Viongozi hao licha ya account zao kuvimbishwa ili kupata nguvu ya kukamilisha walichopanga, lakini pia walihakikishiwa ulinzi wa maisha yao, ulinzi wa familia zao, ulinzi wa mali zao na pia kufutiwa kesi zao nk.

Mkakati huo utatimiaje, sasa fuatilia vizuri kile ninachoandika hapo chini 👇

Ikumbukwe kwamba vyama vya upinzani vimekuwa vikiitaka serikali itengeneze katiba mpya ambayo wanahisi itaweza kuwasaidia wao kushinda chaguzi mbali mbali na hatimae na kushika dola. Lakini kwa upande mungine pia wanaitaka serikali iifumue tume iliyopo na kuunda tume nyingine "huru" ambayo itawashirikisha wadau wote kwa ukaribu zaidi.

Kwahiyo sasa haya mambo mawili ya "katiba" na "tume huru" ndio yatakayotumiwa na wasukaji wa mpango huo kama kichochoro cha kutimiza mikakati ya ushindi wa mama huyo mwenye nyumba.

Inasemekana kitachofanyika ni kwamba serikali itaendelea na msimamo wake wa kutokuwa tayari kutengeneza katiba mpya wala kuunda tume huru, baada ya hapo kiongozi mmoja "mlamba asali mkongwe" wa upinzani atajifanya kuchukizwa na hali hiyo, kisha atatumia uwezo wake na madaraka yake makubwa katika chama kuwashawishi wenzake ambao asilimia kubwa ameshawatia mfukoni, kwamba wasusie uchaguzi wowote utakaofanyika nchini.

Wakishakubaliana kususia inamaana ushindani wa vyama vingine vya upinzani vilivyopo utakuwa mdogo sana hivyo kumpa mama mwenye nyumba fursa ya kuendelea kutawala yeye na bunge lake kama ilivyo sasa.

Yule kiongozi mungine ambae anatokea katika mkoa uliyopo pembezoni mwa ziwa fulani, atabaki kupewa nafasi ya kubwabwaja bwabwaja pale inapobidi ili kuwafunga macho wale wasiojua kile kinachoendelea katika siasa za nyumbani kwetu.

Dalili za mipango hiyo zimeshaanza kuonekana kwa viongozi hao kutia zip midomo yao, na mmoja wao kufikia hatua ya kwenda kumfagilia mama mwenye nyumba huko katika dunia ya kwanza.

Hii mada ni kwa ajili ya wale watu ambao wako huru kifikra na ki akili, wale ambao wanaona mbali na hawana mihemko ya kisiasa.

Hakika "moyo wa mtu msitu", unachokipanga wewe, sio kile anachokipanga mwenzio. Wakati kuna chawa wanashinda mitandaoni kuwapigania, kuwasifia na kuwafagilia viongozi wao wa vyao, wao wanaopiganiwa, wanaofagiliwa na kusifiwa wako busy kulamba asali kimya kimya na kutelekeza mipango ya vyama vyao kiaina.

Jioni njema wakuu. 🙏
watz mnapenda story za umbea umbea tu ambazo mtu huwezi hata kuzithibitisha
 
Hayo uliyoandika hayana msingi wowote, ushindi kwa CCM upo wazi na njia ni nyeupe kabisa, pia kumbuka haiwezi kutokea upinzani ukaja kushinda uchaguzi sahau hilo, na kama kudhibitiana hayo yatakuwa ni ndani ya CCM wenyewe kwa wenyewe.
#SSH2025-30.

CCM Mara ya mwisho kushinda uchaguzi ilikuwa 2005 kkipindi Cha kikwete. Baada ya hapo wanatumua dola kubaki madarakani. Akili za kuongoza hawana ndio maana serikali inategemea mikopo kulipa madeni.
 
Back
Top Bottom