Mkandarasi aliepewa kazi ya ujenzi wa BRT phase 4 kutoka Mwenge hadi Tegeta, anyang'anywe haraka sana kabla hajatupotezea muda

Mkandarasi aliepewa kazi ya ujenzi wa BRT phase 4 kutoka Mwenge hadi Tegeta, anyang'anywe haraka sana kabla hajatupotezea muda

Kwakweli sikuifuatilia sana maana mimi nakaa kigamboni ila hadi Leo sidhani kama imeanza kufanya kazi
Mradi wa miaka miwili, wao waliufanya takriban miaka sita.

Ndomaana natoa tahadhari na hawa wasije ufanya huu nao kwa miaka 6 au zaidi na wakati makubaliano ni miezi 18 serikali ikawaongezea miezi mingine 6 ili iwe miaka miwili kamili.
 
Brt yote ni miradi ya kipigaji angalia kimara inavyofeli mabasi machafu, usalama wake mdogo watu wanajazana.
 
Huo mwendokasi ungeenda hadi Bagamoyo
Nafikiri kwa baadaye BUNJU Kisha bagamoyo, kama ilivyokuwa njia ya morogoro road ilianza mwendokasi kimara Kisha mbezi Sasa mwendokasi imefika kibaha
 
Kama tutakuwa tunaogopa kuongelea madudu mpaka kwanza tumjue aliefanya madudu, basi tutakuwa tunakosea sana.

Mtu akiharibu muwahi kabla hajaharibu zaidi. Ndio inavyotakiwa.
Simaanishi tunaogopa kuongea sababu ya mmiliki wa kampuni ila nataka ujue anapata wapi jeuri ya kufanya kazi atakavyo.

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Hiii barabara ya Mwenge- Victoria inebomolewa tena wakati imejengwa kwa mambilioni wakati wa Magufuu hata miaka mtano bado?
Hio haijabomolewa? Inaongezewa BRT katikati...lakin njia ya bunju tegeta wangefikiria kuleta trams mjini Dar...sio kila mahali mabasi
 
Huenda pesa zishatolewa na zishaliwa. Sasa pesa ya kuwapa wafanyakazi waendelee na ujenzi tena zitatoka wapi?

That's my thoughts
 
Nimesikikitika kwa mleta mada kutaka ninyang'anywe tenda ya kazi yangu ninayoifanya kwa kujituma na kwa weledi
You sounding like Mr Mwigulu Nchemba 😂😂😂
 
Simaanishi tunaogopa kuongea sababu ya mmiliki wa kampuni ila nataka ujue anapata wapi jeuri ya kufanya kazi atakavyo.

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
Hilo linashangaza sana. Ndomaana nimeshauri jamaa wanyang'anywe tenda haraka sana, kabla hawajafika mbali na kuja kusumbua mbeleni.
 
Kumbe barabara za Dar karibu zote zimetifuliwa, hakuna jam za kutisha?
 
Hiii barabara ya Mwenge- Victoria inebomolewa tena wakati imejengwa kwa mambilioni wakati wa Magufuu hata miaka mtano bado?
Hapo jamhuri ya wadanganyika ujenzi wowote wa jana usishangae ukapita kesho umevunjwa. hatuna dira tunaendaenda bila mpango.
 
Kama imeshindikana kujengwa barabara za njia 6 tu kutoka Dar hadi Bagamoyo, unafikiri hilo la mwendokasi ndo litawezekana!!
ukitaka kuona sisi ni nchi ya kijuha nasikia barabara ya keko wamelazimisha kuweka mwendokasi licha ya ufinyu wa ile barabara. matokeo yake njia moja kwa kila upande wa magari ya kawaida. ikitokea gari imeharibika ni ntiti.
 
Hio haijabomolewa? Inaongezewa BRT katikati...lakin njia ya bunju tegeta wangefikiria kuleta trams mjini Dar...sio kila mahali mabasi
Hili la kuleta train kutoka Tegeta hadi Mwenge nililisikia kwa kigogo mmoja akiliongelea.

Yeye alisema serikali ipo katika hatua ya kumtafuta mjenzi wa reli hiyo ili waingie nae mkataba.
 
ukitaka kuona sisi ni nchi ya kijuha nasikia barabara ya keko wamelazimisha kuweka mwendokasi licha ya ufinyu wa ile barabara. matokeo yake njia moja kwa kila upande wa magari ya kawaida. ikitokea gari imeharibika ni ntiti.
Viongozi tulionao hawana ujuzi wala taalum ya nafasi walizo nazo. Ndomaana hakuna cha maana wanachofanya katika nafasi zao.
 
Niaje waugwana,

Huyu mkandarasi haijulikani alipewa tenda hii ya ujenzi BRT phase 4 kutoka Mwenge hadi Tegeta kwa sifa zipi. Toka tarehe ya ujenzi wa barabara hiyo ilipotangazwa kuanza, hadi leo ni miezi sasa, lakini jamaa utafikiri ndio kwanza wana siku 3 tu. Hakuna hatua yoyote ya maana ya ujenzi iliyopigwa.

Wenzao waliokabidhiwa kile kipande kingine kutoka Ubungo mataa, Mwenge hadi Posta wameshafika mbali na wanaonesha hari ya kumaliza kazi yao mapema kabla hata ya muda waliopewa, lakini hawa wa Mwenge to Tegeta bado wanasua sua tu hata Tangibovu hawajaivuka na miezi inazidi kukatika.

Nina hakika hawa watakuja kukifanya hiki kipande kikawie, kama vilivyokawia vile vya phase 2 na phase 3 ambavyo mpaka leo wakandarasi bado wanasua sua tu kumaliza wanashindwa.

Kama wakiendelea kujenga kwa mwendo huu wa konokono, basi nashauri wanyang'anywe ujenzi huu mapema na kukabidhiwa wale wengine wanaoendelea na ujenzi kwa kasi inayotakiwa.

Asanteni.
Mkuu naona maumivu ya kifo cha Haney Tehran Iran kinakuchanganya hadi unamalizia hasira zako kwa wakandarasi wa huo mradi.

Jikaze tu mkuu
 
Back
Top Bottom