Mkandarasi wa wizi wa nyeti kasababisha madhara makubwa

Mkandarasi wa wizi wa nyeti kasababisha madhara makubwa

Ni jana tu kuna kaka, mtumishi wa TRA rafiki yangu maskini wamempiga na kumuumiza vibaya. Jamaa zake zipo, mana asingewahiwa kusaidiwa na msamaria mwema wangemuua. Jamaa kaingia kwa wakala kutoa hela, kumbe kuna watu wanasoma mchezo, si ndio kutokea mtu kusema kamshika bega, watu hawajahoji wameanza kumpiga, mwisho wa siku aliesema kaibiwa nyeti haonekani, na watu washasepa na backpack ya jamaa ambayo ilikuwa ameweka hela zake. So jamaa kaibiwa na kupigwa kapigwa kwa tuhuma za huo upumbavu. Yaani like serious, watu hata hamuuliza wala kupata ushahidi mnaanza tu kumpiga mtu. Tatizo la afya ya akili kwa sasa tunaambiwa ndio gonjwa linotisha kuliko cancer
Tatizo la afya ya akili kwa sasa tunaambiwa ndio gonjwa linotisha kuliko cancer📌🔨
 
Sio kwamba wenye vipisi wamepata kichaka cha kujificha 😎
Mtu atasema mi sikua hivi niikua na mzigo sema 2026 nikashikwa bega😂😂
😂😂😂
2111cc6cefbb37e23ea48b1663c90227.jpg
 
Vipi wapuuzi waliohusika wamekamatwa ?

Ningekuwa kiongozi hao wapuuzi ningewaingiza katika chumba cha mateso na kupiga shoti mbupu zao
Hata watu wanatanabahi kama mtuhumiwa kasingiziwa tu, wezi washasepa na bagpack yake. Na kwenye wengi tena hata hujui yupi ndio yupi
 
Kuna baadhi wanadai ni kile chama cha majambazi lakini kiuhalisia hakina akili kubwa namna hiyo.. Maana chenyewe kiko hoi bin taaban chali kabisa

Haya ni matukio yakuja na kupita
Yapo
Yalikuwepo
Na yatazidi kuwepo
Baadhi ambayo yaliwahi kuvuma sana ni
Mtu joka wa buguruni
TV za kumuona nwizi
Popobawa
Mumiani mnyonya damu
Mchuna ngozi
Nknk
Sass hili la wizi wa nyeti za wanaume limekuja na madhara mengi hasa ya kijamii
Hofu ya kuibiwa nyeti
Watu kusingiziwa uongo
Watu kupigwa, kujeruhiwa na kuumizwa sana
Uharibifu wa mali
Upotevu wa pesa na mali
Watu kukamatwa kwa kusema uongo
Taharuki kwenye jamii

Kwa bahati mbaya sana matukio ya namna hii huenea haraka kama moto wa nyasi kavu mbugani

Kwa kifupi kuna watu wanafaidika na haya mambo la sivyo mamlaka husika zingetoa elimu kwa haraka kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari
Katika hali ya kawaida kabisa ni nani alishawahi kushuhudia mtu aliyeibiwa nyeti zake?
Kama huo uwezo ungekuwepo mbona wanawake wangeringa sana? Maana wangekuwa na uwezo wa kuondoka nazo asubuhi na kuzirudisha jioni (LTE edition)
Sanasana wachache walioweza kwa uchache ni wanamazingaombwe kwenye viini macho tena kwa muda mfupi sana

Hakuna mganga mwenye uwezo wa kuchukua nyeti za mtu.. Achilia mbali huu uvumi kwamba wachukuaji wakikushika tu bega mzigo wote unaondoka

Sasa watu hawajiulizi
Huyo mchukuaji ana nguvu gani ya kuhamisha nyeti za mtu
Kishapo anazihifadhi wapi
Soko lake like wali
Zinauzwaje
Zinahifadhiwaje
Zinasafirishwaje
Zinaenda kutumikaje

Kama mtu ana uwezo wa kukushika tu bega na mzigo ukahama wote! Si basi akusubiri usiku umelala kama hadithi za popobawa?

Mostly wengi walidanganywa zinapelekwa Kongo kutengeneza madawa ya kinga, mvuto na utajiri.. Kongo kuna vita hivyo kuhitaji kupata nyeti za watu hakuhitaji mtu asafiri mpaka bongo
Hata hivyo kwenye uganga pia kuna vigezo na masharti.. Ndio maana mganga hutaka kuletewa vifaa vyenye mambo fulani.. Mano jasho la jogoo wa kijani na njano aliyetoka kula mdondo saa sita mchana!
Sasa vigezo vya hizo nyeti ni vipi?
Vibamia?
Nene?
Fupi?
Iliyopinda?
Mkono wa sweta?
Yenye busha?
Yenye kovu?
Iliyopita kwa ngariba bila ganzi?
Au iliyotutumka kama mashavu ya mtu mwenye safura?
Huu upuuzi umesababisha kadhia kubwa kwenye jamiiView attachment 3570788
Screenshot_20260411_135848.jpg
 
Hata ingekua kweli, unaweza jiuliza hawa jamaa ni akina nani na wanawezaje kuendelea na zoezi licha ya hali ya hewa kuchafuka
 
Back
Top Bottom