ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
Mabadiliko ya Teknolojia na pia utamaduni wa Watanzania sio watu wa Habari labda za umbea
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Uko sahihi mkuu. Mimi ni music na documentary tu. Movie ni once in a while, rarely.Angalia usihadaike ukajiunga na hizo kamari zao😅chek movies na music kwa sana
Na umbea wanazipata insta. Sijui kama shigongo na yale magazeti yake ya ijumaa, uwazi, ijumaa wekenda, sijui nini kama yapo, sijui.Mabadiliko ya Teknolojia na pia utamaduni wa Watanzania sio watu wa Habari labda za umbea
Mtandao ya kijamii ndo imeua main stream media, hata wenyewe wanatoa habari kitoka social media.
Mkuu watabalance vipi wakati wana njaa. Njaa inaharibu kabisa msimamo wako.Tatizo Siasa. Wasingeegemea Siasa wangefanya vizuri tu.
Issue za kubalance balance habari zinawaponza hawana mijadala yenye Akili kubwa
Hakuna Uhuru wa habari. ITV alikuwa wa moto sana kipindi Fulani before JPM Kwa sababu alikiwa anareport bila kupepesa macho..Mkuu watabalance vipi wakati wana njaa. Njaa inaharibu kabisa msimamo wako.
Kila media Duniani iko biased kiasi chake kwa sababu ni mali ya mtu na inafanya yale mtu yule anayotaka.
Sasa chombo cha habari kikiwa na njaa ndio ile biasness inaongezeka mara dufu.
Juzi juzi hapa kiongozi wangu aliita media, akawapiga bahasha kila mtu, yaani walimuuliza maswali ya ajabu ajabu sijawahi kuona. Ni balaa.
Nakumbuka Lowasa aliita media Dodoma, walikua wanauliza maswali ya ajabu ajabu sijawahi kuona. Hata akijibu utumbo wanapiga makofi na kucheka meno yote nje. Pesa hatari sana.
Wanasiasa wameua media ZETU.Sio kweli, sheria, sera na taratibu mbovu ndio zimeua mainstream media hapa kwetu. Huko nchi zilizoendela ambako mitandao ya kijamii ndio nyumbani kwake mainstream media bado ina nguvu kubwa sana.
Malumbano yalikua ya enzi zile za mzee mbishi Mtikila na yule mbishi wa masuala ya meli,, nasikia alifariki mwaka jana.Hakuna Uhuru wa habari. ITV alikuwa wa moto sana kipindi Fulani before JPM Kwa sababu alikiwa anareport bila kupepesa macho..
Taarifa ya habari ilikuwa ni ITV tu, sasa ni hovyo hovyo hata marumbano ya hoja yamekuwa ya mchongo Lazima Wafe njaa
Mzee mkinga au?Malumbano yalikua ya enzi zile za mzee mbishi Mtikila na yule mbishi wa masuala ya meli,, nasikia alifariki mwaka jana.
Hakuwahi kuwa na nidhamu kwenye midahalo ya moja kwa moja! Alitaka kuongea yeye tu! Ukimkatisha twende mapumziko (ni takwa la kiutaratibu after every 15 minutes) yeye ana foka! Mtu kama huyo anatakiwa anunue airtime yake , azungumze anayotaka sio kuvuruga utaratibu! (Tabia hii anayo pia Heche)Mzee mkinga au?
Mh agizo!!?Kama ulikua hujui ndio ujue sasa izo kamali unazoziskia kwenye redio na ma tv ni mpango mpya wa serikali kutafuta pesa ni maagizo
Bora vikafungwa, nchi yenye vyombo imara vya habari hauwezi kusikia ufisadi wa aina yoyote, vinawaandishi mlegezo sana hawawezi hata kuuliza swali.Kweli vyombo vya habari Tanzania vina hali mbaya sana, vinapumulia mashine.
Wiki nzima hii niko nyumbani siendi kwenye mihangaiko ya kila siku, mihangaiko naifanyia nyumbani.
Kwa kua kwangu nyumbani na kifurushi cha dstv kikaisha muda wake hivyo nimejikuta muda wote naangalia tv za bure, eatv, itv, tbc1, upendo tv, clouds tv. Nina miaka mingi sana sijawahi kuangalia hizi tv stations za ndani, miaka mingi.
Hivyo kwa kuangalia hizi tv stations kwa muda wa wiki nzima, nimegundua kua hizi media zetu kubwa Tanzania zina hali mbaya sana ya kifedha, ni matangazo ya waganga wa Jadi, watenda miujiza na kamari.
Hizo kamari sio kutoka kwenye kampuni za kamari kama labda sports pesa ana mbet, bali ni kamari za clouds tv, itv, Chanel ten, eatv n.k.
Wale mnaodaiwa na hivi vyombo vya habari walipeni, vyombo vya habari Tanzania vinapumulia mashine. Watangazaji wana hali mbaya, star tv wafanyakazi wana miaka 2 hawajalipwa mishahara. Hali ni mbaya. Sasa wanategemea kamari kulipa mishahara.
Hawa wasiposaidiwa miaka5 ijayo vituo hivi vitafungwa.