Mkanganyiko wa biashara ya kamari: Mitandao vs vyombo vya habari

Mkanganyiko wa biashara ya kamari: Mitandao vs vyombo vya habari

Linapokuja suala la betting mchezaji anapoteza zaidi ya anavyopata. Mtu yoyote mwenye avarage iq ataliona hilo kupitia set ups za odds, unless hapa unafanya marketing kwa malipo basi jua utapoteza zaidi ya utakachokipata kadri unavyocheza.

Hii michezo haikupaswa kuwa promoted. Ilitakiwa ibaki kuwa burudani tu kwenye maeneo ya starehe.
100,000x28=2.8M ukitoa kodi anabaki na kama 2.3M

Ila anazungumzia breakfast ya wiki moja,mafuta ya wiki moja na mtungi mkubwa wa gas vitu ambavyo vinanunulika bila kubet. Labda aje anyooshe maelezo vizuri.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
100,000x28=2.8M ukitoa kodi anabaki na kama 2.3M

Ila anazungumzia breakfast ya wiki moja,mafuta ya wiki moja na mtungi mkubwa wa gas vitu ambavyo vinanunulika bila kubet. Labda aje anyooshe maelezo vizuri.
Hahaha
 
Ni ukweli usiopingika kwamba (kwa mujibu wa uislamu) hakuna mtu mkamilifu yaani kwamba asitende dhambi; huyo hayupo na Wala hatotokea. Lakini Hilo halitunyimi kukemea na kujizuia na dhambi ambazo ni za wazi kabisa

Kuna dhambi tunafanya bila kukusudia na nyingine hata ukikusudia bado moyo haushituki sana lakini Kuna mijidhambi hata wewe mwenyewe unafanya halafu unashika kichwa unajuta unaona ni uzembe tu mpaka ukaifanya.

Naandika haya kwa feeling sana kwakuwa sasahivi redio na chaneli karibia zote (ukiacha imaan media) na media nyingine za dini, wote habari ni Moja tu ya kubet. Utasikia mpunga, mtonyo, mshiko, na maneno mengine mengi yote yakimaanisha pesa tu.

Ilianza kwa baadhi ya media tu kwa vipindi fulanifulani ikahamia media nyingi na sasa ni media zote na vipindi vyote takribani ukiangalia hawakawii kukutangazia biashara Yao ya kubet

Kwa wale waislamu naomba tukumbushane tu kuwa kubet (na michezo yote mingine ya kubahatisha) ni miongoni mwa KAMARI na KAMARI ni haramu kwa mujibu wa uislamu kwahiyo wewe mfanyakazi muislam usitangaze na kupromote kamari ukaangamiza watu Bure eti kisa unapewa kaposho kwa kufanya hivyo

Kumbuka; kukumbushana ni jambo jema na kupokea na kuufanyia kazi ukumbusho ni hiari ya mtu mwenyewe


Acha kubet epuka kamari
 
Umetimiza wajibu wako kazi kwao sasa

Lkn hakika hayo matangazo siku hizi ni tooo much,hlf serikali inasema vijana waache kubet wkt kila kukicha wanahamasishwa kubet hii ni hatar sana
 
Ni ukweli usiopingika kwamba (kwa mujibu wa uislamu) hakuna mtu mkamilifu yaani kwamba asitende dhambi; huyo hayupo na Wala hatotokea. Lakini Hilo halitunyimi kukemea na kujizuia na dhambi ambazo ni za wazi kabisa..
Hebu fanya kama umepotea njia hivi uupeleke huu ujumbe wako kwenye ule uzi wa betting uuone mooto!
 
Kweli vyombo vya habari Tanzania vina hali mbaya sana, vinapumulia mashine.

Wiki nzima hii niko nyumbani siendi kwenye mihangaiko ya kila siku, mihangaiko naifanyia nyumbani.

Kwa kua kwangu nyumbani na kifurushi cha dstv kikaisha muda wake hivyo nimejikuta muda wote naangalia tv za bure, eatv, itv, tbc1, upendo tv, clouds tv. Nina miaka mingi sana sijawahi kuangalia hizi tv stations za ndani, miaka mingi.

Hivyo kwa kuangalia hizi tv stations kwa muda wa wiki nzima, nimegundua kua hizi media zetu kubwa Tanzania zina hali mbaya sana ya kifedha, ni matangazo ya waganga wa Jadi, watenda miujiza na kamari.

Hizo kamari sio kutoka kwenye kampuni za kamari kama labda sports pesa ana mbet, bali ni kamari za clouds tv, itv, Chanel ten, eatv n.k.

Wale mnaodaiwa na hivi vyombo vya habari walipeni, vyombo vya habari Tanzania vinapumulia mashine. Watangazaji wana hali mbaya, star tv wafanyakazi wana miaka 2 hawajalipwa mishahara. Hali ni mbaya. Sasa wanategemea kamari kulipa mishahara.

Hawa wasiposaidiwa miaka5 ijayo vituo hivi vitafungwa.
 
Kama wewe uendi kwenye mihangaiko unataka na wao wiki nzima wasifanye kazi? Kuanzisha kama nao ni ubunifu na ni kazi kama kazi nyingine….

Hao watu wanapata pesa nyingi sana kupitia kamari bila kuwasahau TRA wanapata pesa na kodi kubwa sana hivyo unatakiwa kujua serikali ndiyo mdau mkubwa wa kamari kupitia TRA!

Vyombo haviwezi kuwa na hali mbaya ikiwa kuna wajinga wanashiriki mshindo millionaire na Tatu mzuka
 
Mtandao ya kijamii ndo imeua main stream media, hata wenyewe wanatoa habari kitoka social media.
Uko sahihi sana mkuu.

Leo watu hawapeleki tena kula Matangazo ya bidhaa zao. Ni mitandaoni tu.

Zamani ili uwe na matangazo ya moja kwa moja ilikua lazima tv, sasa unaweza kufanya kwa WhatsApp, insta live, Facebook, twitter space, teams, zoom call nk. Yaani hali ni mbaya sana.

Millard ayo hana tv stations ila kwa kugundua fursa ya mitandao anapiga hela kama kawaida kuwazidi itv.
 
Back
Top Bottom