Kweli vyombo vya habari Tanzania vina hali mbaya sana, vinapumulia mashine.
Wiki nzima hii niko nyumbani siendi kwenye mihangaiko ya kila siku, mihangaiko naifanyia nyumbani.
Kwa kua kwangu nyumbani na kifurushi cha dstv kikaisha muda wake hivyo nimejikuta muda wote naangalia tv za bure, eatv, itv, tbc1, upendo tv, clouds tv. Nina miaka mingi sana sijawahi kuangalia hizi tv stations za ndani, miaka mingi.
Hivyo kwa kuangalia hizi tv stations kwa muda wa wiki nzima, nimegundua kua hizi media zetu kubwa Tanzania zina hali mbaya sana ya kifedha, ni matangazo ya waganga wa Jadi, watenda miujiza na kamari.
Hizo kamari sio kutoka kwenye kampuni za kamari kama labda sports pesa ana mbet, bali ni kamari za clouds tv, itv, Chanel ten, eatv n.k.
Wale mnaodaiwa na hivi vyombo vya habari walipeni, vyombo vya habari Tanzania vinapumulia mashine. Watangazaji wana hali mbaya, star tv wafanyakazi wana miaka 2 hawajalipwa mishahara. Hali ni mbaya. Sasa wanategemea kamari kulipa mishahara.
Hawa wasiposaidiwa miaka5 ijayo vituo hivi vitafungwa.