Mkanganyiko wa biashara ya kamari: Mitandao vs vyombo vya habari

Tatizo Siasa. Wasingeegemea Siasa wangefanya vizuri tu.

Issue za kubalance balance habari zinawaponza hawana mijadala yenye Akili kubwa
Mkuu watabalance vipi wakati wana njaa. Njaa inaharibu kabisa msimamo wako.

Kila media Duniani iko biased kiasi chake kwa sababu ni mali ya mtu na inafanya yale mtu yule anayotaka.

Sasa chombo cha habari kikiwa na njaa ndio ile biasness inaongezeka mara dufu.

Juzi juzi hapa kiongozi wangu aliita media, akawapiga bahasha kila mtu, yaani walimuuliza maswali ya ajabu ajabu sijawahi kuona. Ni balaa.

Nakumbuka Lowasa aliita media Dodoma, walikua wanauliza maswali ya ajabu ajabu sijawahi kuona. Hata akijibu utumbo wanapiga makofi na kucheka meno yote nje. Pesa hatari sana.
 
Hakuna Uhuru wa habari. ITV alikuwa wa moto sana kipindi Fulani before JPM Kwa sababu alikiwa anareport bila kupepesa macho..

Taarifa ya habari ilikuwa ni ITV tu, sasa ni hovyo hovyo hata marumbano ya hoja yamekuwa ya mchongo Lazima Wafe njaa
 
Sio kweli, sheria, sera na taratibu mbovu ndio zimeua mainstream media hapa kwetu. Huko nchi zilizoendela ambako mitandao ya kijamii ndio nyumbani kwake mainstream media bado ina nguvu kubwa sana.
Wanasiasa wameua media ZETU.

Hata Hapa Jamii forum kuna nyuzi huwezi kupost ikakaa Tofauti na zamani.
 
Hakuna Uhuru wa habari. ITV alikuwa wa moto sana kipindi Fulani before JPM Kwa sababu alikiwa anareport bila kupepesa macho..

Taarifa ya habari ilikuwa ni ITV tu, sasa ni hovyo hovyo hata marumbano ya hoja yamekuwa ya mchongo Lazima Wafe njaa
Malumbano yalikua ya enzi zile za mzee mbishi Mtikila na yule mbishi wa masuala ya meli,, nasikia alifariki mwaka jana.
 
Kama ulikua hujui ndio ujue sasa izo kamali unazoziskia kwenye redio na ma tv ni mpango mpya wa serikali kutafuta pesa ni maagizo
 
Vikufe tuu wakati wa dikteta Magu vilikuwa Bize naye. Ktk uchaguzi mkuu kampeni za vyama vya upinzani hususani Chadema zilikuwa hazitangazwi.

Watu wakaamua kutumia mbinu mbadala kupata taarifa za Chadema kupitia mitandao ya kijamii na wakashangaa umati mkubwa wa watu ktk mikutano yao.
Sasa leo wao wanalilia nani awaonee huruma? Hakuna tena mwananchi mwenye akili timamu anaweza kuziamini hizo Tv uchwara.
 
Mzee mkinga au?
Hakuwahi kuwa na nidhamu kwenye midahalo ya moja kwa moja! Alitaka kuongea yeye tu! Ukimkatisha twende mapumziko (ni takwa la kiutaratibu after every 15 minutes) yeye ana foka! Mtu kama huyo anatakiwa anunue airtime yake , azungumze anayotaka sio kuvuruga utaratibu! (Tabia hii anayo pia Heche)
:
Mtikila (RIP Champ) alikua na jambo moja, ukihudhuria press yake usipokua Mwandishi/ reporter makini, hutotoka na taarifa yoyote! Alikua ana tukana vibaya sana!
 
Hili Kwa sasa ni janga la taifa, yaani tbc chombo Cha umma ambacho kinaendeshwa na serikali na chenyewe kinapiga ramli( kamali) muda wote. Kweli inawezekana kuwa ni kampeni ya Mama kuongeza mapato ya serikali kupitia Tra.
 
Bora vikafungwa, nchi yenye vyombo imara vya habari hauwezi kusikia ufisadi wa aina yoyote, vinawaandishi mlegezo sana hawawezi hata kuuliza swali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…