Mkapa awapa neno wanaotaka Magufuli aongoze mihula mitatu

Mh. Rais alishalizungumzia hili mara kadhaa, hataongeza muhula mwingine zaidi ya hiii iliyopo kwenye katiba yetu.
 
CCM MSITUDANGANYE! suala la kuongeza muda wa uraisi ni mpango wenu wa muda mrefu, mlikuwa mnasubiri tu muda uwadie mbadilishe katiba muongeze muda wa uraisi. Hichi kitu hata mizengo pinda amezungumza mara apewe miaka 7 ......... .. sasa nyie msitubeep beep fanyeni tu sawa sawa na matakwa yenu tumeshawaelewa
 
Hawa watu bwana, na heshima zao wanazopewa na wananchi, sijui akili zao wanaziweka wapi.

Mseveni sio rais, na changamoto hizo anazozungumzia Mkapa hazimhusu?

Kagame je, Nkurunziza, Mgabe na wengine wengi.

Wote hawa changamoto za urais hawakuwa nazo?

Yeye Mkapa, anaona dalili zote, na juhudi kubwa anazofanya kijana wake, halafu anaibuka na komedi za aina yake!

Hapo kijana wake atakapokuwa ametimiza matakwa yake ya kubaki madarakani, tena sio kwa kuongeza ngwe ya tatu tu, bali na zaidi na zaidi..., hapo Mkapa mwenyewe atakuja na maelezo mengine ya kuhalalisha hali hiyo, na kuwaona waTanzania kama mazuzu hivi.

Mtu anafanya juhudi zote kuua upinzani. Anataka ushindi wa asili mia 99..., anataka hayo kwa sabau zipi kama sio kutafuta njia za kuhalalisha nia ovu hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…